Fununu muundo wa serikali mbili ulioboreshwa

Fununu muundo wa serikali mbili ulioboreshwa

Birds in bush

Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
42
Reaction score
23
Ndg wanaJF. Naomba mnijuze muundo was serikali mbili zilizoboreshwa ambazo serikali yetu inazipigia chapuo. Nimefuatilia mapendekezo hayo ila sijawahi kuona popote namna muudno huo utakavyokuwa. Huenda ukawa mzuri na ni muda muaafaka kwa watanzania kuujua na kuona faida zake zitakuwaje. Wasiwasi wangu ninaouna hapa huenda muundo huu ukawapendelea zaidi wazanzibari ili kuwanyamazisha na hapo kuwanyima haki watanganyika. Tujadili na mwenye fununu atujuze.
 
weka mezani basi tuuone, tutajadili hewa
 
Kamuuliza Nape maana yeye anaropoka tuu ulioboreshwa bila kuweka mezani mboresho huo,na miaka yote alikua wapi kumuona waziri wa muungano kumpa majibu ya kero 21 za muungano?
 
CCM hawataki kuweka wazi maboresho hayo, lakini serikali yao si imekuwa na bado ipo madarakani? Muda wote walikuwa wapi kuleta hayo maboresho?

Muda umefika wa serikali tatu wananchi tusiwe wajinga kwa sababu serikali moja haiwezekani, basi ziwe tatu.

Kurudi kwenye kero zile zile za muungano, tutaonekana watu wa ajabu sana, tusikubali kuburuzwa na wachache wa ndani ya CCM. Nasema wachache kwa sababu sio CCM wote wanaridhia kurudi tena kwenye kero za Muungano, tunaogopa nini serikali tatu?
 
Back
Top Bottom