CCM hawataki kuweka wazi maboresho hayo, lakini serikali yao si imekuwa na bado ipo madarakani? Muda wote walikuwa wapi kuleta hayo maboresho?
Muda umefika wa serikali tatu wananchi tusiwe wajinga kwa sababu serikali moja haiwezekani, basi ziwe tatu.
Kurudi kwenye kero zile zile za muungano, tutaonekana watu wa ajabu sana, tusikubali kuburuzwa na wachache wa ndani ya CCM. Nasema wachache kwa sababu sio CCM wote wanaridhia kurudi tena kwenye kero za Muungano, tunaogopa nini serikali tatu?