Uchaguzi 2020 Funzo kwa CHADEMA: Next time msiandae mikutano yenu sambamba na ya CCM!

Uchaguzi 2020 Funzo kwa CHADEMA: Next time msiandae mikutano yenu sambamba na ya CCM!

jingalao: Kama bajeti ya dawa umeongezeka wale watu kule kwenye meli ya Mchina walikuwa wanaenda kufanya nini? Eti bajeti imeongezeka, je, huduma zimeboreshwa? Watu kukimbilia matibabu kwenye meli ya Mchina ni ishara ya uduni wa huduma za jamii ilkiwemo afya.
 
Napenda kuwapa somo dogo ndugu zangu wa Chadema kwa kuwa mnaendelea kujifunza siasa.

Kuna msemo wa kiswahili unaoonya kuhusu kumuiga Tembo Kunya....Mtamalizia wenyewe!!

Nimefuatilia mara kadhaa kamati kuu ya Chadema hasa katika kipindi hiki baada ya uchaguzi mkuu wa 2015 wakijaribu kupanga mikutano na matamko katika siku au wiki ambazo kamati kuu ya CCM au jumuiya zake muhimu zinapofanya mikutano.

Style hii ni mpya kidogo pengine ni katika juhudi za kuongeza ushindani dhidi ya Chama tawala CCM.Utaratibu huu unaelekea umeletwa na mmoja wa makapi kutoka CCM anayejaribu kuifanya Chadema ionekane kama Chama kinachoongoza dola CCM.

Sio mbaya kuiga mambo mengi na mazuri kutoka CCM kwani CCM ni chama kikongwe na chenye hazina kubwa ya ubunifu.

Hoja yangu ni moja tu siku ya leo..kwamba mnapoona mbinu mliyocopy na kupaste inagoma kuwaletea matokeo tarajali hamna budi mara moja kuachana nayo kwa kuwa bila kufanya hivyo mntaishia kupata aibu na kuwapunguzia morali.

Juma hili kamati kuu ya Chadema imekutana na ilitarajiwa kwa mujibu wa wanapropaganda wa Chadema mitandaoni kuja na maazimio au matamko mazito kama ilivyo desturi yao ya kututia kamba.

Ninachojiuliza ni kimoja tu....je kiherehere cha kupanga mkutano wao sambamba na mikutano kadhaa ya jumuiya za CCM walikitoa wapi?mimi sina jibu ila wanabavicha mnaeeza kunisaidia.

Ni aibu kubwa kwa mara nyingine kamati kuu ya Chadema inajizolea kwa kujaribu kujilinganisha na Chama kubwa CCM katika mazingira ambayo yanaonesha wazi utofauti wa kiwango cha Mbingu na Ardhi kati ya vyama hivi iwe ni kwa coverage,support,agenda na organisation.

Mfano:Mkutano mmoja tu wa jumuiya za CCM yaani mkutano wa UVCCM uliweza kuzima kabisa mjadala wa kikao cha kamati kuu ya Chadema.Hii ni aibu inayohitaji tathmini.

Niendelee kuwaasa ndugu zangu wa CDM kuwa wabunifu na kuja kivingine ili kweli kuonesha kuwa kama wapinzani mna jipya la kuiletea nchi.

Achaneni kupokea mawazo ya makapi ya CCM na mafisadi waliofanya Chadema kuwa chaka lao...watawapotosha.

KWA LEO NI HAYA TU...

HAPA KAZI TU!
Chadema huwa hawajifunzi...na wakikosolewa wanaporomosha matusi.
Kadhia iliyowakuta 2015 wakati CCM wanapitisha mgombea wao wa Urais ilikuwa kubwa.
Mkutano wa kamati kuu Chadema ikasambaratika..
Wakabaki kuangalia TV mambo ya Ccm...ikabaki tutatangaza mgombea jumamosi ijayo...baada ya hapo wakaingia mitini kwa kipindi kirefu sana [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Niwashauri mara 2? Hakuna mtu ana muda wa kushiriki huo upuuzi.
2020 wakiacha shiriki uchaguzi mkuu najitoa JF!...hawana uwezo susia uchaguzi mkuu level zao hizi tuu!..
 
Haaa haaa me nilishasahau kama walifanya mikutano na kuja na matamko!Ni ngumu kujipambanua kati ya tasisi na kikundi cha wanaharakati full stop!aya ni mapicha picha tu movie kamili inakuja
 
2020 wakiacha shiriki uchaguzi mkuu najitoa JF!...hawana uwezo susia uchaguzi mkuu level zao hizi tuu!..

Kwani hata sasa una impact gani wakati wewe mwenyewe umejiunga juzi.
 
CCM hamna lolote zaidi ya kutegemea nguvu za Jeshi lakini ktk medani za kisiasa hamna lolote. Ni kama Zimbabwe jeshi likiwaacha mmekwisha hata huyu bwana ameingia kwa nguvu za jeshi ktk Kura alipigwa vibaya.
 
Back
Top Bottom