Habari wanajamii bila shaka mko vizuri, japo kuna changamoto za hapa na pale kama report ya CAG na mengineyo. Ila leo nakuja kwa kuwashauri na kuwahimiza kufanya mabadiliko na siyo kuwa na mazoea.
Nikianza na viongozi wa idara ya Maji Mwanza (MWAUWASA), jamani mjifunzeni kwa wenzenu wa SHUWASA-Shinyanga. Mwanza kumekuwa na changamoto za maji sana, hata kwenye wilaya ambazo zipo mjini kabisa, kama vile Busweru wilaya ya Ilemela.
Miaka nenda rudi tatizo la maji limekuwa changamoto kutatuka, japo serikali imeweka nguvu kwa miradi ya matank lakini mpaka sasa ni miaka inaendelea, ukiachilia mbali wilaya hiyo kuendelea na kukua kwa kasi lakini bado changamoto ya maji ipo. Wakurugenzi wa idara hizo jamani mpo wapi au ndiyo yale magari yanawachanganya mnaosahau shida za Watanzania na kuzama kwenye ofisi za vioyoyozi na kushindwa kwenda site kujua nini kinaendelea mpaka pale mtakaposhitushwa na ziara za mawaziri husika, hapo ndipo mnapotunga ripoti za uongo na ujinga mwingi.
Jifunzeni kwa wenzenu wa Shinyanga, mifumo ya maji imeenea kila mtaa mpaka sehemu ambazo wananchi hawajaanza ujenzi, lakini kwenye viwanja kuna mabomba ya maji. Lakini Mwanza, ambapo karibu nusu ya eneo limezungukwa na ziwa, lakini miundombinu ya maji imekuwa changamoto.
Watumikieni wananchi, acheni kubweteka kula pesa ya watozwa ushuru bure, badilikeni umo maofisini. Mnafanya upumbavu ambao hauna maana, ambao ukiwekwa hadharani hapa mtavikimbia viti hivyo.