FUNZO LA NDUGAI: Kuna haja kisheria kwa Tanzania kuwa na Spika asiyetokana na chama cha siasa?

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Ni wazi kuwa Spika Ndugai imejiuzuru uspika wa bunge la Tanzania kwa shinikizo la chama chake cha CCM baada ya kutofautiana kimtazamo na Rais Samia Suluhu ambaye ndio mwenyekiti wa CCM taifa.

Upande wa pili pia, utendaji wa Ndugai akiwa spika wa bunge la Tanzania kwa sehemu kubwa ulikuwa umelenga kukibeba chama chake cha mapinduzi (CCM) kwa hila, hali na mali kwa sababu ya mashinikizo ya chama chake.

Yaani CCM ilimuweka Ndugai kuwa spika pale bungeni ili kuibeba serikali na CCM, na ghafla alipokuja na msimamo tofauti na serikali na CCM ikamshinikiza kuachia ngazi.

Kwa kuwa bunge ni mali ya wananchi, na spika wa bunge ni kiongozi wa chombo hicho kimamlaka, ni vyema na busara kuwa na sheria itakayohakikisha Spika wa bunge hakishinikizwi na mamlaka nyingine yoyote ya nje ya bunge katika utendaji wake wa kila siku ikiwemo chama cha siasa. Na njia rais, spika asiwe mwanachama chochote cha siasa.

Haya ya Ndugai yatuamshe sasa kuwaza mbali, maana yataendelea kujirudia tena na tena ikiwa tutaendelea na utaratibu huu wa sasa wa kuwa na spika anayetokana na chama cha siasa.

Katiba mpya ni jambo la lazima kwa sasa.
 
Pillar moja ni giant zaidi ya zingine hapo tuna safari ndefu.
 
La muhimu Katiba Mpya isukwe such that kwanza haki za msingi za wananchi hazichezewi ovyo then pili ihakikishe hakuna vitisho kwa mihimili mmoja dhidi ya mwingine kwa kisingizio cha kujichimbia zaidi no matter wakuu au watendaji wa mihimili wowote wnatokana na chama au vinginevyo.

This also applies to other state organs that are supposed to be independent including NEC, CAG, etc. Kwa sakata la Ndugai tunaamini kabisa hicho kinachoitwa Tume Huru ni huru kweli kama sio kiini macho! Na kuna mchakato umeanza wa kuiongezea uhuru nje ya Katiba! Ha ha ha! Kama mhimili umetikiswa what is Tume nje ya ulinzi wa Katiba?
 
Ukiwa na bunge lenye wabunge wengi kutoka vyama tofauti visivyopishana idadi kwa kiasi kikubwa spika hata akiwa na chama hakuna tatizo.
 
Haya ya Ndugai yatuamshe sasa kuwaza mbali, maana yataendelea kujirudia tena na tena ikiwa tutaendelea na utaratibu huu wa sasa wa kuwa na spika anayetokana na chama cha siasa.
Mchawi ni katiba mbovu tuliyo nayo
 
Tatizo kumpata Mtanzania ambaye hana chama na anafaa kuwa Spika ni ngumu sana.

Kwa bahati mbaya sana hata akipatikana lazima baada ya mda atajifungamanisha na chama chenye dola!

Hii ndo shida ya “hejemonia” ya mfumo wa kisiasa kwa nchi yetu.

Hata hivyo kama hili lingewezekana basi ingekuwa ni hatua nzuri sana ktk kukuza demokrasia nchini@Pascal Mayalla and Meneja Wa Makampuni

La Aquila non capit muscas!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…