UCHAMBUZI MZURI WA MTU MMOJA KUHUSU KATUNI YA LEO YA KIPANYA.
Mtu kwenye katuni anajitahidi kufunika makaburi kwa red carpet!
The meaning:
1. Red carpet ni zuria la hesima ya Kifalme (royal honour) lakini mtu hajikunjulii mwenyewe bali linakunjuliwa na wanaompa heshima ili yeye apite (raia wanaochagua mtawala) ila hapo kwenye picha mhusika anajikunjulia mwenyewe (amejipa madaraka mwenyewe).
This means haeshimiwi na watu ila ni yeye tu analazimisha heshima. Watu watamheshimu yule tu waliyemchagua kuwaongoza! Nje ya hapo itakulazimu kuitaka heshima kwa nguvu, na utachoka sana (matone ya jasho),
2. Kingine Mtu kwenye picha anatumia hiyo heshima ya kujipa (kujikunjulia red carpet) kufunika makaburi, lakini makaburi yalivyochongoka kama pembe la ng'ombe yamegoma kufichika, yanatoboa tu hilo zuria na kuchomoza juu!. Anaonekana kujitahidi kufunika kweli, lakini waaapi!
Maana yake: Mtu kwenye picha anajaribu kuficha ukweli mzito kwa kutumia mamlaka yake ya kiuongozi
3. Kingine zuria ni jembamba tu kwa ajili ya grand entrance tuuu, so hata likijitahidi kufunika makaburi machache bado kuna makaburi mengi yako pembeni yamelizunguka hilo zuria la heshima pande zote kama mawimbi!
Maana yake: Mtu kwenye picha amezungukwa na madudu na uchafu, ambao hakuna nguvu ya kimamlaka inaweza kuusafisha au kuuficha, inapelekea kila mtu anaona kwa uwazi, hakuna siri tena!
4. Mtu kwenye picha anayefunika amepambana sana ila anaonekana kuchoka sana ndio maana ya matone ya jasho. Amechoka kwa sababu yupo pekeyake....kwa kifupi kila kitu ni yeye anafanya hana msaada. Yaani yeye mdiye polisi, ndiye mahakama, ndiye magereza ndiye mratibu wa kila kitu.
Maana: Taasisi ya Mtu kwenye picha imeziua, kuziteka nyara taasisi nyingine zote nyeti za nchi, matokeo yake kuna mpasuko na mgawanyiko wa kutisha! Na wasaidizi wameingia mitini, wamemtelekezea mtu kwenye picha kila kitu apambane nacho!
Wengine ongezeni uchambuzi wenu twende sawa!!!