Furaha ni haki yako

Furaha ni haki yako

D Metakelfin

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
3,399
Reaction score
3,666
anaandika zingo

Mawazo ya HOFU ndani ya mtu hayana uhalisia na ni kitu cha muda tu, bali ni zao la TABIA za hofu tulizorithi au tulizolishwa kwenye jamii kupitia milango yako ya ufahamu na ambazo mtu anaweza kuziacha akipata UFAHAMU.

Mfano: Watoto huogopa kulala gizani na pia huogopa baadhi ya picha kwa sababu hawana ufahamu kuwa kulala gizani hakuna hatari, pia picha ni picha tu haina uhalisia.

NI MUHIMU KUTAMBUA: Safari yetu ya Makuzi na mazingira ndio matokeo ya Jinsi tulivyo leo kifikra, kimtizamo na ki-imani.

Kiukweli kuna watu hawaishi kwa FURAHA NA AMANI kutokana na madhara ya mazingira ya makuzi yetu kuanzia utotoni.

Mfano: Jamii imetuaminisha utu wa mtu na pengine heshima yake inajengwa kutegemea jinsi watu wanavyokutazama, kukukubali, kukusifia, mali, hali, n.k. Hii inasababisha baadhi ya watu kuumia wanapokosolewa, mitazamo yao kutokubalika au kuwa tofauti na wengine kihali na mali.

MTU KUKUTHAMINI AU KUTOKUTHAMINI haikuongezei wala kukupunguzia kitu bali ni mtazamo tu.
JITHAMINI MWENYEWE HAIHITAJI IDHINI YA MTU MWINGINE.

Wengine walikuzwa kwenye malezi ya woga, Hofu, pengine kutishwa, etc. KIMSINGI Imani nyingi za watu walizonazo ikiwa ni pamoja na imani potofu (mfano uoga wa kulogwa, hofu, n.k) zimerithiwa kwenye jamii. Tunatakiwa kutambua SIO KILA KITU ULICHOAMINISHWA NA JAMII NI KWELI.

Wengine wamekuzwa katika mazingira ya magomvi,Chuki,kulipizana visasi,kushindana, kupigana, kuumizana nk.

Hii pia imejenga tabia za baadhi ya watu kuwa hivyo.

Kimsingi Tabia za mtu zimejengwa na jamii na mazingira. Hivyo ulivyo kitabia SIO WEWE UKO HIVYO BALI NI JINSI ULIVYOAMINISHWA.

Kwa kutambua baadhi ya tuliyoaminishwa na kurithishwa tangu utotoni mengi yamegeuka kuwa sehemu ya Tabia zetu na kutuletea matatizo mengi kama HOFU, MSONGO WA MAWAZO, HUZUNI, CHUKI, WIVU, MATUKANO, DHARAU, NA MAMBO MENGINE YANAYOFANANA NA HAYO....
 
Back
Top Bottom