Furaha ya taifa stars imeondoka na Serengeti boys

Furaha ya taifa stars imeondoka na Serengeti boys

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Watu walikuwa na Imani kubwa na Serengeti boys kufanya vizuri kwenye mashindo Yale ya Afcon lakini matokeo yake ikashindwa kuwaaminisha watanzania kuwa kile kichwa cha wendawazimu kimetoweka kwenye awamu hii.

watu wengi walijiapisha Kwa timu Yao kuwa ingefanya vizuri kwenye mashindo Yale kutokana na matokeo iliyokuwa inayapata waki wa maandalizi. Watu wengi waliwaahidi na wengine kuingia mifukoni mwao kuwapa chochote kitu ili kuchagiza ushindi wao wakwenda world cup.


Muanguko huu wa Serengeti umesababisha watu wengi kuogopa kuishobokea timu kubwa ya taifa stars ingawa imefuzu kwenda misri. Watu hawana furaha wala matumaini tena na timu Yao kuogopa kilichotokea Kwa wapwa zao Serengeti boys.
Watu wako kimya kana kwamba wanafahamu kuwa yatakuwa yaleyaleee ya Serengeti boys.

Nini kifanyike ili kuwarudishia watanzania Imani Yao Kwa timu Yao ya wakubwa?
 
Back
Top Bottom