Furaha yako itarejea au kuongezeka, ukifanya mambo haya 15

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Watu wengi wamepoteza furaha maishani mwao kwa sababu mbalimbali za kimaisha. Kama na wewe huna furaha, furaha yako inaweza kurejea ukifanya mambo yafuatayo:
  1. Kuna aliyekukosea? Usimchukie, msamehe – Chuki huiba furaha, lakini msamaha huleta amani.
  2. Kuna jambo limeishaharibika? Acha kulalamika – Acha kulalamikia mambo yasiyoweza kubadilika. Malalamiko huongeza huzuni.
  3. Mshahara hautoshi? Jifunze kuridhika – Kukubali hali uliyo nayo huondoa msongo wa mawazo.
  4. Watu wamekuvunja moyo? Kaa na watu wanaokutia moyo – Marafiki wazuri huongeza furaha maishani.
  5. Tenga muda wa kukaa na familia yako – Kukaa na familia ni baraka na chanzo cha furaha.
  6. Fanya mazoezi ya mwili – Mwili wenye afya nzuri unachochea akili yenye furaha.
  7. Una chakula au nguo za ziada? Wasaidie wenye mahitaji – Mtu anayewasaidia maskini au wajane hupata furaha zaidi.
  8. Uliosoma nao wana nyumba na magari lakini wewe huna? Acha kujilinganisha na wengine – Furahia baraka ulizo nazo badala ya kutamani za wengine. Kwa wakati uliokubalika na wewe utayapata hayo.
  9. Ukitukanwa, cheka! Usikasirike wala usinune – Kicheko huondoa msongo wa mawazo.
  10. Kuna mambo hayakuenda vizuri huko nyuma? Sahau mabaya ya zamani – Usiruhusu yaliyopita “yakunyonge.”
  11. Jitahidi kuwa na upendo kwa wengine – Kuwapenda wengine huleta furaha.
  12. Soma Biblia, utashangaa ukianza kuisoma – Ina maneno mengi ya faraja na yenye kutia moyo.
  13. Mueleze Mungu hitaji lako – Watu wanadharau maombi, lakini ukweli ni kwamba Mungu anasikia na kujibu maombi. Mimi, Mungu amenipa vitu vingi baada ya kumuomba.
    Yesu anasema: "Hata sasa hamjaomba jambo lolote kwa Jina langu. Ombeni nanyi mtapewa, ili furaha yenu ipate kuwa kamili"(Yohana 16:24).
  14. Unasikitika kwa kuwa unachelewa kufikia lengo lako? – Mshukuru Mungu kwa kila jambo (1 Thes 5:18). Furahia kila hatua unayopiga kikazi au kibiashara. Usihuzunike kwakuwa unakawia kufika kileleni, utafika!
  15. Epuka kufanya dhambi – Dhambi huleta dhamiri mbaya na kukufanya ujisikie una hatia; lakini utakatifu huleta amani na furaha. Ukitubu dhambi na kumwamini Yesu, kisha ukaendelea kuishi maisha matakatifu, siku inakuja utaingia mbinguni kwenye furaha na raha ya milele!
"Nimewaambia hayo, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe." (Yohana 15:11).
 
Sawa Mkuu!
 
Usiwe na haki kupita kiasi usiwe mwovu kupita kiasi wala usiwe mpumbavu, kwanini ufe kabla ya wakati wako!
Mhu 7:16-17
 
Furaha Yako Irejee.png

Nitamfurahia Bwana kwa moyo wangu wote(Zaburi 9:2)
 
  1. Epuka kufanya dhambi Dhambi huleta dhamiri mbaya na kukufanya ujisikie una hatia; lakini utakatifu huleta amani na furaha. Ukitubu dhambi na kumwamini Yesu, kisha ukaendelea kuishi maisha matakatifu, siku inakuja utaingia mbinguni kwenye furaha na raha ya milele!

"Nimewaambia hayo, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe." (Yohana 15:11).

DHAMBI
Mpaka leo sijawahi kuelewa dhambi ni kitu gani? Nimekusoma vitu vingine vyote ila hapa, dhambi ni nini?
 
ukionewa tabasamu,ukikata tamaa tabasamu,ukiwa na shida ,huzuni, njaa nk tabasamu,ukiwa na furaha tabasamu!!👿 muda wote onesha tabasamu!! MAISHA NI MARA MOJA TU
 
Back
Top Bottom