Furaha yangu ya Yanga kuchukua kombe imekatishwa na kauli tata ya kocha msaidizi Cedric kaze

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Natoa pongezi za dhati kabisa kwa Yanga sc kubeba kombe la Azam shirikisho baada ya kuichapa Azam FC kwa bao moja kwa mtungi.

NALIA NGWENA nilikua nafuraha kubwa lakini furaha yangu imekatishwa na kocha msaidizi wa Yanga Cedric.

Mwandishi: Msimu ujao tutegemee mtihani mkubwa wa kufikia/ kufanya zaidi ya hapa kwa kupata mafanikio Kama haya mliyoyapata mwaka huu?

Cedric Kaze: Mtihani watakuwepo nao hao watakao kuja maana sisi tumemaliza mkataba nafikiri hao watakao kuja Yanga sc ndiyo watakua na mtihani."

Hilo jibu la Kaze limenifanya nigundue kuwa, mwamba anasepa, na kama anasepa ni peke yake au Nabi nae kiukweli furaha yangu imepotea gafla.

Nawasilisha hoja.
 
Kwanza asingeweza kusema kuwa atahusika msimu ujao ilihali mkataba huo hawana.

Lakini la pili, Dunia Ina watu wengi na vipaji tofauti kwa nyakati tofauti, nadhani sio vizuri kudhani hamuwezi kufanikiwa kisa ni Fulani.

Ila Imani yangu, basing kwa kazi nzuri walioyofanya, sidhani kama klabu itawaacha, labda waamue kupandisha dau la kukomoa.
 
Kama uliangalia vizuri baada ya mechi Kocha Nabi alikwenda kuwapa mkono wa kwaheri mashabiki wa Yanga.Hiyo ni ishara kuwa Nabi anaondoka Yanga pamoja na Kaze...destination yao inaweza kuwa south Africa au Africa ya kaskazini.
 
Kuondoka ama kutoondoka itategemea na mazungumzo ya mikataba mipya, msimu ndiyo umekwisha na uongozi wote ulikuwa bize na ratiba ngumu ya michuano mbalimbali isingewezekana kupata muda wa kuzungumzia mambo ya mikataba ya makocha au wachezaji, Sasa kazi imekwisha watakaa watayajenga na ikitokea wameshindwana basi wataenda kutafuta malisho sehemu nyingine na yanga watatafuta kocha mpya ambae atakuja kuanzia walipoishia wao!
 
Ngoja tuone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…