Furaha yatoweka CCM, ushindi kama msiba, wapinzani washangilia. Rais ageuka kauli zake za awali kanisani Dodoma

Furaha yatoweka CCM, ushindi kama msiba, wapinzani washangilia. Rais ageuka kauli zake za awali kanisani Dodoma

watu hatuna furaha, aliyeshinda ana hofu , aliyejitoa anaogopa kutekwa na kuuwawa na "walinzi wa kijani" , walio kaa kimya wanahofu hata kuonyehs uchama wao, nchi hii kwa sasa ili uwe na amani kuwa mshabiki wa KWAYA tu
Mbona mimi nina furaha! Nasubiri msusie na ubunge mwakani,na urais pia msusie,hatuna habarii..
 
Hahaha Mkuu unaandika vitu visivyokwepo

Watanzania wanaendelea na shughuli zao wala hawana mawazo mgando km yako
Watu hawajali tena hizo siasa uchwara aisee...kila mtu anapambana kwa ajili ya hali yake na familia yake.....
 
Hongereni Ccm kwa kuwabwaga Wapinzani wenu

Hawataki kuamini kama Wananchi wamewapuuza, wamejificha kwenye kivuli cha kulaumu Rais
Mmmmh....mbona hata mimi sina furaha wakati ni mwanaCCM tena hai?? Uchaguzi ulivurundwa na kufanywa wa kidhuluma ya kidemokrasia na ubabe wa kidola kupitia wizara husika. Waliopitishwa hata wao hawana ujasiri wa kujisifia au kifurahia kupachikwa kwao.
Mambo yakiwa hivi kwa 2020, haina haja ya kufanya uchaguzi wowote bali ufanyike uteuzi tu tuache demokrasia ya kimaigizo na machukizo.
 
Kama ukatoliki siyo madhabahu ya Mungu basi hata Biblia inapoteza sifa za neno la Mungu,
Panua akili usipanue mdomo
Wewe ndo nikushauri upanue mawazo yako think beyond , hivi unajua kuna tofauti kati ya kumtumikia MUNGU na dini kama taasisi??
 
Jamaa mnafiki sana eti"mkawachague watu mnaowataka"watu gani hao?
 
Wakati mwingine wanampa nafasi ili aonekane alivyo mchovu kiakili!! Werevu tunamchora tu na wapumbavu wanashangilia
 
Tangu lini katoliki ikawa na madhabahu ya bwana?hapo ndipo mnachanganya kati dola ya kirumi iliyonajisi kanisa na kanisa takatifu la mungu!!!
ww ni msabato, ? sitii neno hapo, ila magufuli kajitahidi sana hadi CHaDEMA wamemkimbia kuogop aibu hongera sana jpm hongera ccm kwa ushidi mnono
 
Tusali kwanza
tapatalk_1574626010455.jpeg
 
Katika hali ya kindumilakuwili, RAISI akiwa kanisani Dodoma, kanisa katoliki lile linalomwimbia nyimbo za sifa na kuabudu, baada ya kusali alikabidhiwa kipaza sauti aseme neno, alizungumza siasa japo huwa yeye anasema siasa na dini zisichanganywe tena huenda mabili zaidi na kukutanisha wanasiasa wamuombee.

Alipopewa kinasa sauti, alisema ... watanzania wakachague viongozi wao wanaowataka ili wawaletee maendeleo bila KUJALI CHAMA WALA DINI! huu ni unafiki wa Phd ya UDOM, juzi tu hapa alisema wapinzani wanachelewesha maendeleo na wasichaguliwe na yule mama kule Sumbawanga alikuwa anamlilia akamwambie aende kwa huyo mbunge wa upinzani akamwombe!

KATOLIKI MNACHEZEA MADHABAHU YA BWANA, kumbuka mfalme mmoja alifia madhabahuni baada ya kuuza kipande cha ardhi na kudanganya.

Endeleeni tu kumdhihaki Mungu, msifikiri watanzania ni wajinga kama ninyi, tunawaheshimu tu,
NIMEIKUTA KWENYE PAGE YA BABA ASKOFU DR BENSON BAGONZA ALFAJIRI HII

FURAHA KAENDA WAPI?

Waliopiga kura hawana furaha

Waliosusa/suswa hawana furaha

Waliopita bila kupingwa hawana furaha

Waliosimamia kura hawana furaha

Walioshinda hawana furaha

Walioshindwa hawana furaha

Waliopanga yaliyotokea hawana furaha

Waliopangiwa yaliyotokea hawana furaha

Walioshauri hekima hawana furaha

Waliokaa kimya hawana furaha

Wanaounga mkono nilichoandika hapa, hawana furaha

Wanaopinga nilichoandika hapa, hawana furaha

Wanaodhani wana furaha hawana furaha

Wapinzani hawana furaha
Wapinzani wa wapinzani, hawana furaha.

ILA wanaodhani hawana furaha, ni KWELI hawana furaha.

Ni bora kujiuliza huyu furaha yuko wapi?
cleardot.gif
ndugu yangu kuna watu wanafiki humu duniani huwezi amini, hv mtu ukikalia kile kiti unajiona upo juu ya MUNGU ama? Mungu hataniwi mazee, unasema wakuombee kwa Mungu saa hyo hyo unamdhihaki Mungu. Mwingine alilia kinafiki sana church. Wachungaji mtumie nyumba za ibada vizuri siku mtakiona kidole kinaandika madhabahuni ndo mtapo jamba cheche
 
Tujikumbushe kitabu cha fasihi kilichoitwa Tambueni hakizetu! Mwandishi wake alikuwa mhadhiri wa chuo kikuu Dar. Penina Mhando. Alimlilia mwanae daudi aliyepelikwa kumpiga Dyamini. Anauliza dyamini ni mnyama gani? Dyamini kanichukulia daudi wangualiyekuwa ananitunza!

Dyamini litachukua furaha za kila mtu. Dyamini ziko nyingi sasa na zinatamba kuanzia Dar mpaka Rukwa. Dyamini zinatumbua na kutengua kila kukicha bila maswali. Furaha haiwezi kuwepo mpaka huyu/hawa wanyama watoweke.
 
Furaha siyo uwezo wa kutumia nguvu uliyonayo, bali uwezo wa kuhimili nguvu zako ili zisiumize wengine.. [emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji109][emoji109][emoji109][emoji123][emoji123][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
Furaha siyo uwezo wa kutumia nguvu uliyonayo, bali uwezo wa kuhimili nguvu zako ili zisiumize wengine..
 
Huko makanisani kumebaki unafiki mtupu, akifa maskini atahojiwa ndugu wa marehemu maswali kibao kama marehemu alikuwa anasali au kushiriki michango, akitaka kuoa maskini utasinkia kunapingamizi alisha oa akaacha, sijui vitu gani huko, maskini hata kama ana jambo la kusema huwezi kusikia mapadre wakihoji kama kuna mtu ana la kusema ili apewe kipaza sauti aseme, bali mwenye hela na madaraka hahojiwi jambo anapata huduma zote. Hawa kina pengo and CO. Bure kabisa.
 
Hongereni Ccm kwa kuwabwaga Wapinzani wenu

Hawataki kuamini kama Wananchi wamewapuuza, wamejificha kwenye kivuli cha kulaumu Rais

Wewe upo kundi la mimba za utotoni, na mimba zisizo tarajiwa.
Mtu aliyetungishwa mimba kwa kudhamiria hawezi kuwa na akili yako, unahitaji ukombozi wa kifikra
 
Huko makanisani kumebaki unafiki mtupu, akifa maskini atahojiwa ndugu wa marehemu maswali kibao kama marehemu alikuwa anasali au kushiriki michango, akitaka kuoa maskini utasinkia kunapingamizi alisha oa akaacha, sijui vitu gani huko, maskini hata kama ana jambo la kusema huwezi kusikia mapadre wakihoji kama kuna mtu ana la kusema ili apewe kipaza sauti aseme, bali mwenye hela na madaraka hahojiwi jambo anapata huduma zote. Hawa kina pengo and CO. Bure kabisa.

Umegusa pabaya sana, Ukifa kama ni tajiri kanisa linangangania maiti yako, kumbuka kingunge hajawahi kuwa na dini, ni mkomunisti lakini kanisa fiulani likateka msiba, likamzika, Mungu anawachora tu
 
Huko makanisani kumebaki unafiki mtupu, akifa maskini atahojiwa ndugu wa marehemu maswali kibao kama marehemu alikuwa anasali au kushiriki michango, akitaka kuoa maskini utasinkia kunapingamizi alisha oa akaacha, sijui vitu gani huko, maskini hata kama ana jambo la kusema huwezi kusikia mapadre wakihoji kama kuna mtu ana la kusema ili apewe kipaza sauti aseme, bali mwenye hela na madaraka hahojiwi jambo anapata huduma zote. Hawa kina pengo and CO. Bure kabisa.
Katoliki ndio wanaongoza kwa tabia hii, sijasema wa hapa Tanzania, ila wao
 
Back
Top Bottom