TODAYS
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 14,747
- 24,250
Mdau amani kwako.
Nimepita sehemu mbalimbali nchini na kujifunza vitu kadhaa vyenye hasara na faida ikiwepo.
Kila mkoa kuna aina ya maisha wanayoishi na huwezi kuyabeba and kuyapeleka mkoa mwingine ili waishi kama mkoa ulipoyatoa.
Twende pamoja.
Mkoa wa Arusha ni mkoa wenye watu watafutaji kwa muda mwingi hii inamuhusu Ke na Me, ukienda maeneo mengi wamama ni wengi wakifanya biashara, sokoni ni zaidi.
Ukipita Kilombero utaona wamama wakiwa bize na mboga ya mnyavu huku mtoto/watoto wake wakizurula jirani na hapo alipo, ukienda Samunge ndiyo usiseme na tuegemee hapo samunge.
Baada ya kuona rundo la watoto wakizagaa na kucheza pale sokoni, nimewauliza wazazi baadhi wakaniambia kitu kimoja, "hawana mtu wa kulea nyumbani".
Wale watoto kwa eneo dogo niliowaona ni kuanzia umri wa mwak 1 - 4 years na walikuwa wanacheza sehemu isiyo salama na hatarishi kiafya.
Niliwaambia wazazi "naanzisha darasa humo humo sokoni ili muwalete washinde hapo".
Jibu lilikuwa "mbona utakuwa umetusaidia sana" nadhani hii ni fursa hasa mdau wa jf unayetafuta kazi, biashara and kipato, usiiache hii kitu ipite hivihivi kwa 2020.
Kama wazazi wameonyesha ukubali kulipa 1000 kwa siku na watoto wapo zaidi ya 40, nani aje atupe mtaji?
Fanya maamuzi 2020 mwaka wa furaha. Ni hayo tu kwa leo.
"UMASIKINI NI DHAMBI"