Fursa gani ipo kwenye Halmashauri uliyopo?

Mkwawe

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2016
Posts
3,132
Reaction score
5,508
Aisee maisha yalinipiga wadau miaka kadhaa iliyopita, nilikuwa Dar kwa kipindi kirefu hela nilikuwa nashika lakini ni Kama nawatafutia watu. Kodi ya nyumba, nauli za daladala kila siku, kifungua kinywa, chamcha na chajio, kubet (sababu ya msongo), kodi ya taka, hela ya ulinzi shirikishi Ankara za maji, umeme wa TANESCO (Huu ni mzimu)... yaani mambo yalikuwa lukuki kuliko hata kipato nikichokuwa naingiza.

Tena tangu uongozi mpya uingie ndiyo nilianza kuiona dar ni jehanamu.
Mwanangu mmoja yeye ni mjasiriamali halmashauri ya Babati alinichorea ramani niende nikaangalie fursa, kufika huko nikakaa Kama wiki kadhaa nikapta wazo la nini cha kufanya na baada ya kupitia nyuzi kadhaa humu JamiiForums wazo la biashara likaja na kuzingatia mazingira ya pale nilipofikia nikaona biashara ya dagaa inaweza kuwa makini kwangu.

Nilifikia Babati sehemu moja inaitwa Bonga, akiba yangu niliyokuwa nayo nikaipeleka mwanza kwa mdau wangu mmoja akanisafirishia gunia mbili za dagaa. Niliuza rejareja namshukuru Mungu ilipatikana kwa muda mfupi tu ukizingatia na hulka yangu ya maneno mengi ya watu wa mashariki biasha ikasonga.

Sahivi Kuna baadhi ya watu nimekuwa kama wakala wao kwa kuwaketea mizigo ya dagaa na kusema ukweli hatua niliyopuga ni kubwa japo bado sijafika ninapotarajia. Kipindi hiki pia maparachichi ni mengi sana naweza nunua paleti hata nne za parachichi Naenda Dom kwa wauzaji rejareja nawapa mzigo wananipa changu maisha yanasonga.

Babati Kuna hela wanangu asiwaambie mtu hapa kuna fursa nyingi sana maana huu mji unachipukia kwa kasi, nitazitaja baadhi...

•Migahawa ya hadhi ya Kati
Kama mtu una mtaji njoo uwekeze hapa maana migahawa mingi ni ile ya kawaida hivyo ukiongeza standards kidogo tu unakuwa wa tofauti na pesa itakufuata

• Maduka ya vifaa vya ujenzi
Huu mji ndio unakuwa kuwa kwahiyo hayo mazaga yanahitajika Sana

•Maduka ya Pembejeo za kilimo
Kilimo kina nafasi kubwa huku, wengi nimeona wanalima alizeti, karanga na mahindi kwa hiyo mazaga Kama hayo yanahitajika

•Duka la mifugo na utaalamu
Kama umesomea mifugo na uko mtaani unalalamika ajira nakusanua Sasa njoo huku shehe wangu hutajuta, ukipuuza huu ujumbe na kung'ang'ani mjini wewe ni mbuzi. Mwanangu mmoja alisoma Tropical animal health production Yuko simanjiro nilimchorea ramani sasa hivi kila muda anakenua tu

ANGALIZO;
Kama ukija huku kutafuta hakikisha unatafuta kweli mambo ya wanawake huku achana nao kwa sababu ukiingia tu kwenye mtego wa wanawake wa kimbulu umeumia watakukomba hadi mav*z* maana hata hii huku nayo ni biashara kubwa tu.

Kingine usiwe mkorofi, ukiuifanya mkurya sijui mnani wanakutahiri vizuri huku, Mimi huku kinachonibeba ni msingi mdomo masihara mengi lakini nina mipaka, watu wengi wananikubali kwa hulka yangu ya kuongea Sana na kuwaheshimu wenyeji.

Nikipata muda nitarudi Dar ila kwa sasa bado nipo nipo saaana aisee, maana hata bei ya vyakula ni kitonga

I LOVE BABATIII ❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️😘😘😘😘😘😍
 
I LOVE BABATIII [emoji3590][emoji3590][emoji3590][emoji3590][emoji3590][emoji3590][emoji3590][emoji3590][emoji8][emoji8][emoji8][emoji8][emoji8][emoji7]
Mkuu kati ya dar es salaam na mwanza wapi kuna fursa nyingi??
Mana nipo njia panda
 
Inategemea unaongelea fursa gani, kwa mfano mwanza uuzaji wa dagaa sio wa tija Sana kulinganisha na dar au nguo kwa dar sio Kama mwanza. Kwa hiyo kwa hii miji mikubwa miwili unaangalia wapi Kuna malighafi nyingi kuliko pengine hivyo unachofanya ni kuhamisha
 
Mimi ni dereva Bajaj
Ila mkoani naona fursa nyingi hasa kwa kilimo
Uko sahihi ila kwenye kilimo ni lazima uwe na mtandao na utashi wa kufanya mazao yako yawe na tija, kinachowaangusha wakulima wengi kwa mtazamo wangu baada ya kukaa nao ni kuwa hawana chanzo kingine cha mapato hivyo wanasubiri mavuno na wakivuna tu changamoto zote zinategemea hela aliyoipata

Kwa huku aisee wakivuna wanachanja gomba Kama hawana akili nzuri
 
Back
Top Bottom