Fursa gani zinadharauliwa lakini zinaweza kukutoa kimaisha?

Fursa gani zinadharauliwa lakini zinaweza kukutoa kimaisha?

Biashara zote zina uzito sawa kiuwajibikaji. Biashara zote zina fursa sawa za kukupa mafanikio. Biashara zote zinahitaji kiwango sawa cha uwekezaji ili kukupa kiwango cha mafanikio unayoyataka. Biashara zote zina nafasi ya kukua kutoka hatua moja hadi nyingine. Biashara zote zinawezekana kufanikisha malengo yangu kwa kuzingatia wakati, mazingira, soko lengwa na jinsi ulivyojidhatiti kuiendesha biashara yako.
Kwa kuchangia ufafanuzi uliyotolewa na wengi wengine; 1. ni vyema kuitazama biashara yako kwa mapana na marefu kabla hata hujaanza utelekezaji kwa kiwango kidogo. Lengo hapa ni kukupa picha pana ya wapi unaelekea kibiashara na fursa, uwezo, vikwazo na udhaifu uliyonao kuikabiri mikikimikiki ya kuiendesha hiyo biashara. 2. uwe na tamaa ya kuchambua takwimu (number crunching) sababu kuna mabilioni ya pesa yanatupiga chenga kwa sababu tu hatutaki kuchanganua hesabu za biashara zetu (analytics) kwa uzembe wa kufikiri. 3. uwe na utayari ya kuwashirikisha wenye uwezo wa kushauri hata ikibidi kwa gharama fulani unayodhani utaimudu au hata zawadi ya kitu ulichonacho kuonyesha ukarimu wako na kwamba unathamini ujuzi wao. 3. kama wengine walivyoshauri, tambua tabia na mwenendo wa soko, hasa hasa kwa vitendo zaidi mfano unataka kuuza matunda basi ni vyema kuanza kwa kuonjesha wateja watarajiwa kwa malipo kidogo au hata ikibidi bure na kuwaomba wakupe mrejesho wa ubora na kuendelea kununua kwako. 4. jaribu kwa udi na uvumba kufungamanisha bidhaa au huduma unayotoa ambayo mara nyingi inaendana na tabia ya soko. 5. jitangaze kwa njia ya mojakwamoja kutokana na ubora wa bidhaa na huduma kwa wateja kwa kuhakikisha gharama za matangazo ni sehemu ya ubora wa bidhaa(ufungishaji) na huduma nzuri kwa wateja kwani huduma nzuri pekee huchangia takriban 60% ya mafanikio ya biashara nyingi.
 
Biashara haitaki maneno mengi,analysis nyiingiii mwisho wa siku unakata tamaa,we jilipue tu,ukiingiza huo utaalam wako utafeli.
 
Haha ha ha ha ha Watu wanawachukulia kuku Rahisi sana!! Kuku wanalipa sana lakini
sio mtaji wa kitoto ule, Inatakiwa ukaze msuli kwelikweli uache mambo yako mengi na
uwe na 'usiriasi' hautaki masihara, nikianza kuelezea hapa ninavyowajua wanJF wataanza
kuniuliza kwanini umeacha kufuga.
kuna boss wngu hapa mbezi makabe alikuwa na banda la kuku ana kuku kama 200 walipofikia umri wa kutaga wakaanza kufa mmoja mmoja alichanganykiwa sana kila nikienda kufata gar asubuh nakuta kuku c chin ya wawil wamekufa had wakaisha
 
Nimefuga kuku aina ya kroiler aisee wale ndege wanakula sijapata kuona nashukuru nimeweza kuwatoa wote na sasa nataka nihamie kwenye kuku wa nyama(broiler).
mkuu nimeogopa gafla,maana mwenyewe nimenunua seheemu vifarnga 35 bado sijavichua nasubiri vifikishe walaumwezi mmoja.ni wale kuku chotala
 
Industry yenye moto ss iv ni e-sports ( online video game competition) video games kwa ujumla, artificial intelligence na crypto currencies, kwa kifupi kutatua changamoto za watu kwa kutumia technolojia.Kati ya hizi nilizotaja mm nimewekeza kwenye video games, zina addiction viby kwaiyo pesa zinanifata tu zenyewe. Toka nimeanza hii wiki ya tatu nahisi, minimum kwa siku haishuki chini ya 40k.
mkuu samahani hpo mimi umeniacha,kama utajali ngoja nikuibox unieleweshe vizuri hizo video game online compatition ndo zipo vp na hayo mazagazaga mengine ulioyamention hapo.
 
Kuuza Sokoni,najua hutaki kuamini,ila kuna watu wanatoka na wana nyumba na magari,tembelea soko moja pale Mbezi mwisho Dar,utapewa hiyo hadithi na utaonyeshwa wahusika,ila ni wale wale wachaga,nadhani kikubwa hapa ni discipline tu..
 
Sijampa vitisho Mkuu!
Ila angenijibu ningempa mchanganuo!
Unajua Kuna vitu ambavyo Huwa hatuambiani ukweli, unakuta mtu anaaminishwa na hawa mamotivational speaker wa kibongo kama kuku rahisi na wanalipa ila hawatoi changamoto mapema mpaka mtu unakuta ameshaunguza mtaji wote!

Na siunajua kwa sisi Vijana ukijipinda kupata hela ya kuanzia ukaunguza unavyouma?

Ndio lilikuwa lengo langu sio kumtisha,sorry kama alinielewa vibaya
mkuu we tushushie nondohizo mi nna vifaranga 35ila bado sijavichua hd mwezi ufike.
 
Namshukuru mtoa maada umenisaidia kujua nifanye biashara gan kwa kuanzia kutengeneza mtaji
 
Dhana ya bendera hufuata upepo inapojidhihirisha dhahiri.lile kusudio kuu la uumbwaji wako unapolipuuza!
 
Kila sIku nafikiria kuanzisha biashara ya kukaanga mihogo maeneo ya Posta. Mihogo yenyewe inaweza kuwa sio fursa sana ila fursa itakuwa kwenye matangazo ya hiyo muhogo.Nitatangaza kuwa mihogo hii inaongeza nguvu za kiume. Hapo ndipo fursa ilipo..
😀😀
 
Kuuza Sokoni,najua hutaki kuamini,ila kuna watu wanatoka na wana nyumba na magari,tembelea soko moja pale Mbezi mwisho Dar,utapewa hiyo hadithi na utaonyeshwa wahusika,ila ni wale wale wachaga,nadhani kikubwa hapa ni discipline tu..
Mbezi mwisho hamna soko la kueleweka lipo soko koko njia ya ghoba pale shule ya msingi na hamna biashara nzur sijui soko gan unazungumzia ww mkuu
 
Kufanya biashara kunahitaji uwe na uthubutu wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na kujinyima, bila kusahau nidhamu ya pesa.

Kwa mtu ambaye alikuwa anachukua salary yake kila mwisho wa mwezi na kuanza kufanya "pattern" za maisha ni ngumu sana kukuelewa hasa unapo mwambia ukweli wa hizi fursa. Katika mawazo yake anaamini biashara kubwa kubwa tu ndizo za kufanya ili amantain "pattern" zake za maisha kama kawaida.

A. Chips
B. Kuziba pancha/ lubricants ndogo ndogo za magari.
C.Games
D. Chakula/ mama ntilie/ baba ntilie.
E. Karanga.
F. Genge
G. Banda la kuonyesha mpira

Hizi ni biashara ambazo zinauwezo wa kukupa pesa kila siku na hasa kama unategemewa au kuweza kufanya marejesho ya mkopo wako wa mwezi au week, na ukawa unasukuma maisha yako vizuri tu na ukasahau mambo ya redundancy kabisa na vyeti feki.

Ili uweze kufanikiwa kwenye hayo makundi ya biashara unahitaji uwe na nidhamu ya pesa sana, ujitoe haswa na kuna mambo unahitaji kuyakacha kabisa.

1. Chura
2. Gambe
3. Kuvaa/ nguo mpya
4. Simu ya tachi
5. Marafiki wasio na mpango.

Kama umejenga inakuwa safi sana, ila kama umepanga inabidi uangalie namna ya kulihandle hilo ili kwendana na huo mziki unaochezwa muda huo hapo juu.

Si shauri mtu achukue mkopo halafu ukalime, ukafuge, hizo ni biashara zinazohitaji muda mwingi sana mpaka zije kukupa pesa mkononi na zina story zake pia na sidhani kama aliyekukopesha ataweza vumilia muda huo wote labda awe ndugu yako au mzee wako. Lakini kama ni hawa Bayport, finca na wengineo, mzee!! Hakuna rangi utaacha kuona..!

Lakini pia usisahau kwamba wewe ni binadamu una mahitaji yako ya kila siku ambayo unahitaji kuyasukuma kwa pesa kidogo au unawategemezi wanaotegemea kitu kutoka kwako kila siku, anza na hizo hapo juu halafu nenda shamba kalime, kafuge!

Biashara inayoanza inahitaji sana uangalizi wako na muda wako pia ni kama malezi ya mtoto mchanga, ipe muda wako wa kutosha. Hivyo changamoto kama hasara za siku ni sehemu ya biashara. Usipaniki Pambana!! Hata mbuyu ulianza kama mchicha.

Kwenye kufuga:-
1. Kitimoto
2. Mbwa ( siyo mbwa koko)

Kilimo:-
1. Mihogo, (hasa hii mbegu ya kisasa)
2. Tango

Makundi haya huwa hayasumbui sokoni na demand yake ni kubwa sana.

N.B
Huku mtaani kuna changamoto ya chuma ulete, inasumbua sana hasa kwa mtu mgeni kwenye biashara jipange katika haya;-
1; kamati ya ufundi
2; Maombi.

Shukrani..!
asante mkuu hapo mwisho umemalizia vyema kabisa
 
Biashara haitaki maneno mengi,analysis nyiingiii mwisho wa siku unakata tamaa,we jilipue tu,ukiingiza huo utaalam wako utafeli.
Hahahaha! kwanini sasa unauliza nataka kuanza biashara, mnishauri nifanyeje wakati unaweza KUJILIPUA tu?
 
Hahahaha! kwanini sasa unauliza nataka kuanza biashara, mnishauri nifanyeje wakati unaweza KUJILIPUA tu?
Siyo busara KUJILIPUA tu kwa sababu wengi wetu tumekuwa tukijilipua. Kumbuka kwamba hizi biashara hata japo ni ndogo kimtaji au hata kimapato zinwakilisha ndoto kubwa sana za wajasiriamali. Pia kwa hali ya sasa mitaji ni shida sana kupatikana hata kwa kiwango kidogo cha fedha. Muda mwingi wajasiriamali wanaotumia kuanzisha biashara hizi pia ni mali. Soko unaloanza kulijenga katika mauzo yako ya mwanzo, hata kwa kujilipua, yana athari chanya kwa wateja unaowauzia. Ni vyema kuwa makini katika hizi hatua unazochukua kuanzisha biashara ili kulinda haya yote niliyoorodhesha.

Sababu hasa ya zile hoja 5 nilizoandika hapo awali ni KWANZA kukupa picha ya ugumu wa kazi yenyewe japo wengi tunaichukulia poa sana. PILI kukuchagiza ili uone mapana na marefu yanayopaswa kufikiriwa. TATU kama mjasiriamali, uanze na yale yanayotekelezeka kwa urahisi halafu baadaye uyashughulikie yale ya kiufundi zaidi wakati biashara inaendelea. NI VYEMA ukijua kwamba kiutendaji, yote yanawezekana kufanyika kwa awamu au kwa mtawalio ili mradi kichwani mwako unakumbuka endapo nitakwama mahali, huenda ni kwasababu fulani na huenda nikichukua hatua fulani naweza kutoboa.

Tangu ni miaka kumi na nane nimekuwa nikisikia ndugu zangu wakisema biashara zetu zinazaliwa na kufa haraka sana sababu ndivyo ilivyo ada. Nilipoanzisha biashara miaka kumi iliyopita nikajifunza kwamba kufa au kuendelea kwa biashara zetu kuna hitaji sana mbinu na jitahada za hali ya juu kuendelea kuwepo kama nilivyoshauri.

Siyo ajabu wapo wanaopenda KUJILIPUA kama sehemu ya majaribio. Huo pia ni uchaguzi binafsi.
 
Back
Top Bottom