Fursa gani zinadharauliwa lakini zinaweza kukutoa kimaisha?

Kwa kuchangia ufafanuzi uliyotolewa na wengi wengine; 1. ni vyema kuitazama biashara yako kwa mapana na marefu kabla hata hujaanza utelekezaji kwa kiwango kidogo. Lengo hapa ni kukupa picha pana ya wapi unaelekea kibiashara na fursa, uwezo, vikwazo na udhaifu uliyonao kuikabiri mikikimikiki ya kuiendesha hiyo biashara. 2. uwe na tamaa ya kuchambua takwimu (number crunching) sababu kuna mabilioni ya pesa yanatupiga chenga kwa sababu tu hatutaki kuchanganua hesabu za biashara zetu (analytics) kwa uzembe wa kufikiri. 3. uwe na utayari ya kuwashirikisha wenye uwezo wa kushauri hata ikibidi kwa gharama fulani unayodhani utaimudu au hata zawadi ya kitu ulichonacho kuonyesha ukarimu wako na kwamba unathamini ujuzi wao. 3. kama wengine walivyoshauri, tambua tabia na mwenendo wa soko, hasa hasa kwa vitendo zaidi mfano unataka kuuza matunda basi ni vyema kuanza kwa kuonjesha wateja watarajiwa kwa malipo kidogo au hata ikibidi bure na kuwaomba wakupe mrejesho wa ubora na kuendelea kununua kwako. 4. jaribu kwa udi na uvumba kufungamanisha bidhaa au huduma unayotoa ambayo mara nyingi inaendana na tabia ya soko. 5. jitangaze kwa njia ya mojakwamoja kutokana na ubora wa bidhaa na huduma kwa wateja kwa kuhakikisha gharama za matangazo ni sehemu ya ubora wa bidhaa(ufungishaji) na huduma nzuri kwa wateja kwani huduma nzuri pekee huchangia takriban 60% ya mafanikio ya biashara nyingi.
 
Biashara haitaki maneno mengi,analysis nyiingiii mwisho wa siku unakata tamaa,we jilipue tu,ukiingiza huo utaalam wako utafeli.
 
kuna boss wngu hapa mbezi makabe alikuwa na banda la kuku ana kuku kama 200 walipofikia umri wa kutaga wakaanza kufa mmoja mmoja alichanganykiwa sana kila nikienda kufata gar asubuh nakuta kuku c chin ya wawil wamekufa had wakaisha
 
Nimefuga kuku aina ya kroiler aisee wale ndege wanakula sijapata kuona nashukuru nimeweza kuwatoa wote na sasa nataka nihamie kwenye kuku wa nyama(broiler).
mkuu nimeogopa gafla,maana mwenyewe nimenunua seheemu vifarnga 35 bado sijavichua nasubiri vifikishe walaumwezi mmoja.ni wale kuku chotala
 
mkuu samahani hpo mimi umeniacha,kama utajali ngoja nikuibox unieleweshe vizuri hizo video game online compatition ndo zipo vp na hayo mazagazaga mengine ulioyamention hapo.
 
Kuuza Sokoni,najua hutaki kuamini,ila kuna watu wanatoka na wana nyumba na magari,tembelea soko moja pale Mbezi mwisho Dar,utapewa hiyo hadithi na utaonyeshwa wahusika,ila ni wale wale wachaga,nadhani kikubwa hapa ni discipline tu..
 
mkuu we tushushie nondohizo mi nna vifaranga 35ila bado sijavichua hd mwezi ufike.
 
Namshukuru mtoa maada umenisaidia kujua nifanye biashara gan kwa kuanzia kutengeneza mtaji
 
Dhana ya bendera hufuata upepo inapojidhihirisha dhahiri.lile kusudio kuu la uumbwaji wako unapolipuuza!
 
Kila sIku nafikiria kuanzisha biashara ya kukaanga mihogo maeneo ya Posta. Mihogo yenyewe inaweza kuwa sio fursa sana ila fursa itakuwa kwenye matangazo ya hiyo muhogo.Nitatangaza kuwa mihogo hii inaongeza nguvu za kiume. Hapo ndipo fursa ilipo..
😀😀
 
Kuuza Sokoni,najua hutaki kuamini,ila kuna watu wanatoka na wana nyumba na magari,tembelea soko moja pale Mbezi mwisho Dar,utapewa hiyo hadithi na utaonyeshwa wahusika,ila ni wale wale wachaga,nadhani kikubwa hapa ni discipline tu..
Mbezi mwisho hamna soko la kueleweka lipo soko koko njia ya ghoba pale shule ya msingi na hamna biashara nzur sijui soko gan unazungumzia ww mkuu
 
asante mkuu hapo mwisho umemalizia vyema kabisa
 
Biashara haitaki maneno mengi,analysis nyiingiii mwisho wa siku unakata tamaa,we jilipue tu,ukiingiza huo utaalam wako utafeli.
Hahahaha! kwanini sasa unauliza nataka kuanza biashara, mnishauri nifanyeje wakati unaweza KUJILIPUA tu?
 
Hahahaha! kwanini sasa unauliza nataka kuanza biashara, mnishauri nifanyeje wakati unaweza KUJILIPUA tu?
Siyo busara KUJILIPUA tu kwa sababu wengi wetu tumekuwa tukijilipua. Kumbuka kwamba hizi biashara hata japo ni ndogo kimtaji au hata kimapato zinwakilisha ndoto kubwa sana za wajasiriamali. Pia kwa hali ya sasa mitaji ni shida sana kupatikana hata kwa kiwango kidogo cha fedha. Muda mwingi wajasiriamali wanaotumia kuanzisha biashara hizi pia ni mali. Soko unaloanza kulijenga katika mauzo yako ya mwanzo, hata kwa kujilipua, yana athari chanya kwa wateja unaowauzia. Ni vyema kuwa makini katika hizi hatua unazochukua kuanzisha biashara ili kulinda haya yote niliyoorodhesha.

Sababu hasa ya zile hoja 5 nilizoandika hapo awali ni KWANZA kukupa picha ya ugumu wa kazi yenyewe japo wengi tunaichukulia poa sana. PILI kukuchagiza ili uone mapana na marefu yanayopaswa kufikiriwa. TATU kama mjasiriamali, uanze na yale yanayotekelezeka kwa urahisi halafu baadaye uyashughulikie yale ya kiufundi zaidi wakati biashara inaendelea. NI VYEMA ukijua kwamba kiutendaji, yote yanawezekana kufanyika kwa awamu au kwa mtawalio ili mradi kichwani mwako unakumbuka endapo nitakwama mahali, huenda ni kwasababu fulani na huenda nikichukua hatua fulani naweza kutoboa.

Tangu ni miaka kumi na nane nimekuwa nikisikia ndugu zangu wakisema biashara zetu zinazaliwa na kufa haraka sana sababu ndivyo ilivyo ada. Nilipoanzisha biashara miaka kumi iliyopita nikajifunza kwamba kufa au kuendelea kwa biashara zetu kuna hitaji sana mbinu na jitahada za hali ya juu kuendelea kuwepo kama nilivyoshauri.

Siyo ajabu wapo wanaopenda KUJILIPUA kama sehemu ya majaribio. Huo pia ni uchaguzi binafsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…