Fursa gani zinadharauliwa lakini zinaweza kukutoa kimaisha?

Mkuu hii project vipi unauzoefu au utaalamu nayo?

Maana zamani sana marehemu Mzee alikuwa anajiandaa kufanya!
kidogo maana sijawahi kuitengeneza ila kujifunza na kuifuatilia kwa ukaribu hasa baada ya kupata wazo la kusambaza ges ka maji
 
Ma
Hongera kwa kujaribu..
Hiyo maeneo gani mkuu..?
 
Mnaifahamu INTERNET???
Basi INTERNET ina fursa nyingi sana basi tu watu tunaitumia kuingia JF, instagram na WhatsApp.
Fursa mojawapo ni kuwekeza katika Cryptos. Watu wanaziita scam business, basi tu ni vile hawana right information at the right time.
Wewe na jiran yako mumefaidikaje!!?
 
Mkuu hio e-sports unaifanyaje kaka? Hrbu nipe udau sijaielewa vyema?
 
mkuu hii biashara ya chips naifanya dah naona 2 watu wanadharau ila mapato yake ni sawa na mfanyakaz anaelipwa 1.5 net income , ila nawaonaga wakitoka ofisin wanadharau hawajui kitu gani napata
Mkuu mboro hebu nihabarishe kinagaubaga, nataka niweke vyeti pembeni niingie biasharani hasa katika mkondo wa kuuza kiepe safi na salama, unapatikana wapi mkuu?
 
Wekeni degree zenu kabatini, tafuteni mitaji mtatoka.

Biashara ya kusafirisha mkaa tu peke yako inakutowa, cha msingi hakikisha unapata vibali vya mali asili.

Pili Kilimo ingawa hii ndio namba one, inategemea na mtaji wako wa kuwekeza kwenye kilimo, kinalipa sasa hivi.
 
mkuu hii ni kwel?
Jaribu ku google most expensive liquid/scorpion vernom wanatumia kutengenezea insulin na mambo kibao nikikutajia bei ya lita tano ya hiyo sumu ya n'nge hutoamini kwa kifupi wanunuzi wanakufata wenyewe sasa kuna mibongo naielezea hapo juu hainielewi imekariri biashara ni kuuza mitumba inasikitisha sana
 
Mkuu,tupeane maujanja ya hii biashara.
 
Kufanya biashara kunahitaji uwe na uthubutu wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na kujinyima, bila kusahau nidhamu ya pesa.

Kwa mtu ambaye alikuwa anachukua salary yake kila mwisho wa mwezi na kuanza kufanya "pattern" za maisha ni ngumu sana kukuelewa hasa unapo mwambia ukweli wa hizi fursa. Katika mawazo yake anaamini biashara kubwa kubwa tu ndizo za kufanya ili amantain "pattern" zake za matumizi kama kawaida.

A. Chips
B. Kuziba pancha/ lubricants ndogo ndogo za magari.
C.Games
D. Chakula/ mama ntilie/ baba ntilie.
E. Karanga.
F. Genge
G. Banda la kuonyesha mpira

Hizi ni biashara ambazo zinauwezo wa kukupa pesa kila siku na hasa kama unategemewa (bread winner) au kuweza kufanya marejesho ya mkopo wako wa mwezi au week, na ukawa unasukuma maisha yako vizuri tu na ukasahau mambo ya redundancy kabisa na vyeti feki.

Ili uweze kufanikiwa kwenye hayo makundi ya biashara unahitaji uwe na nidhamu ya pesa sana, ujitoe haswa na kuna mambo unahitaji kuyakacha kabisa.

1. Chura
2. Gambe
3. Kuvaa/ nguo mpya
4. Simu ya tachi
5. Marafiki wasio na mpango.

Kama umejenga inakuwa safi sana, ila kama umepanga inabidi uangalie namna ya kulihandle hilo ili kwendana na huo mziki unaochezwa muda huo hapo juu.

Si shauri mtu achukue mkopo halafu ukalime, ukafuge, hizo ni biashara zinazohitaji muda mwingi sana mpaka zije kukupa pesa mkononi na zina story zake pia na sidhani kama aliyekukopesha ataweza vumilia muda huo wote labda awe ndugu yako au mzee wako. Lakini kama ni hawa Bayport, finca na wengineo, mzee!! Hakuna rangi utaacha kuona..!

Lakini pia usisahau kwamba wewe ni binadamu una mahitaji yako ya kila siku ambayo unahitaji kuyasukuma kwa pesa kidogo au unawategemezi wanaotegemea kitu kutoka kwako kila siku, anza na hizo hapo juu halafu nenda shamba kalime, kafuge!

Biashara inayoanza inahitaji sana uangalizi wako na muda wako ni kama malezi ya mtoto mchanga, ipe muda wako wa kutosha. Hivyo changamoto kama hasara za siku ni sehemu ya biashara. Usipaniki Pambana!! Hata mbuyu ulianza kama mchicha.

Kwenye kufuga:-
1. Kitimoto
2. Mbwa ( siyo mbwa koko)

Kilimo:-
1. Mihogo, (hasa hii mbegu ya kisasa)
2. Tango

Makundi haya huwa hayasumbui sokoni na demand yake ni kubwa sana.

N.B
Huku mtaani kuna changamoto ya chuma ulete, inasumbua sana hasa kwa mtu mgeni kwenye biashara jipange katika haya;-
1; kamati ya ufundi
2; Maombi.

Shukrani..!
 
Yaani mkuu kila ninapofikiria kuhusu hiyo Project naiona kama ngumu sana
nimewahi kuwaza kujaribu lakini naiona kama inahitaji utaalamu mkubwa
lakini nitaifuatilia.
Nitafte mkuu nikusaidie kama upo serious
 
Kuwa mr kucha... yan kuosha miguu ya wanawake na kucha kwa siku kama position nzuri hasa vyuoni unaondoka na si chin ya 70 kwa siku
Tatizo wanaJF wengi humu wanaweza kumaliza siku wakiwa wamewapiga wadada
Bure hizo Rangi za Kucha by the way ni Fursa mzuri pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…