Kufanya biashara kunahitaji uwe na uthubutu wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na kujinyima, bila kusahau nidhamu ya pesa.
Kwa mtu ambaye alikuwa anachukua salary yake kila mwisho wa mwezi na kuanza kufanya "pattern" za maisha ni ngumu sana kukuelewa hasa unapo mwambia ukweli wa hizi fursa. Katika mawazo yake anaamini biashara kubwa kubwa tu ndizo za kufanya ili amantain "pattern" zake za matumizi kama kawaida.
A. Chips
B. Kuziba pancha/ lubricants ndogo ndogo za magari.
C.Games
D. Chakula/ mama ntilie/ baba ntilie.
E. Karanga.
F. Genge
G. Banda la kuonyesha mpira
Hizi ni biashara ambazo zinauwezo wa kukupa pesa kila siku na hasa kama unategemewa (bread winner) au kuweza kufanya marejesho ya mkopo wako wa mwezi au week, na ukawa unasukuma maisha yako vizuri tu na ukasahau mambo ya redundancy kabisa na vyeti feki.
Ili uweze kufanikiwa kwenye hayo makundi ya biashara unahitaji uwe na nidhamu ya pesa sana, ujitoe haswa na kuna mambo unahitaji kuyakacha kabisa.
1. Chura
2. Gambe
3. Kuvaa/ nguo mpya
4. Simu ya tachi
5. Marafiki wasio na mpango.
Kama umejenga inakuwa safi sana, ila kama umepanga inabidi uangalie namna ya kulihandle hilo ili kwendana na huo mziki unaochezwa muda huo hapo juu.
Si shauri mtu achukue mkopo halafu ukalime, ukafuge, hizo ni biashara zinazohitaji muda mwingi sana mpaka zije kukupa pesa mkononi na zina story zake pia na sidhani kama aliyekukopesha ataweza vumilia muda huo wote labda awe ndugu yako au mzee wako. Lakini kama ni hawa Bayport, finca na wengineo, mzee!! Hakuna rangi utaacha kuona..!
Lakini pia usisahau kwamba wewe ni binadamu una mahitaji yako ya kila siku ambayo unahitaji kuyasukuma kwa pesa kidogo au unawategemezi wanaotegemea kitu kutoka kwako kila siku, anza na hizo hapo juu halafu nenda shamba kalime, kafuge!
Biashara inayoanza inahitaji sana uangalizi wako na muda wako ni kama malezi ya mtoto mchanga, ipe muda wako wa kutosha. Hivyo changamoto kama hasara za siku ni sehemu ya biashara. Usipaniki Pambana!! Hata mbuyu ulianza kama mchicha.
Kwenye kufuga:-
1. Kitimoto
2. Mbwa ( siyo mbwa koko)
Kilimo:-
1. Mihogo, (hasa hii mbegu ya kisasa)
2. Tango
Makundi haya huwa hayasumbui sokoni na demand yake ni kubwa sana.
N.B
Huku mtaani kuna changamoto ya chuma ulete, inasumbua sana hasa kwa mtu mgeni kwenye biashara jipange katika haya;-
1; kamati ya ufundi
2; Maombi.
Shukrani..!