Ivi wewe unawajua wabongo kwa kukopi na kupaste. Hiyo biashara utaifanya wiki 2 tu ikilipa wiki ya 3 mtajikuta mko 6 mtaani hapo ndipo utakapoanza kuuza maamdazi 10:kwa Siku.Wakuu Leo nimeona nije na Mada hii ili ndugu zangu mlioko mjini mnufaike kupitia mawazo yangu!
Iko hivi mjini Kuna watu wengi tofauti na kijijni. Yaani Unakuta nyumba 1 Ina watu zaidi ya 20 wakiwemo wapangaji including watoto.
Kuna biashara ya vitafunwa yani maandazi ama chapati ama keki nk. Leo nije na maandazi.. Ukitengeneza maandazi 500. @1.Tsh 100 zidisha Mara 500 unapata 50000
Hapo ukitoa garama za Mafuta, mkaa ama kuni, Nguvu nk. Unakuta faida 20000 kwa siku. Zidisha siku 10 una laki mbili pembeni ya mtaji iko pale pale.
Swali unawezaje kuuza maandazi Mia 5 kwa siku?
Jibu: ukipita nyumba 1 yenye wapangaji let say 7.. Kila mtu akanunua maandazi 5 tayari 35 ukizunguka nyumba 20 tayari umemaliza kazi tena asubuhi asubui hapo hujauza wale wa njiani.
Kwa Leo naona niishie hapo
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha hatariIvi wewe unawajua wabongo kwa kukopi na kupaste. Hiyo biashara utaifanya wiki 2 tu ikilipa wiki ya 3 mtajikuta mko 6 mtaani hapo ndipo utakapoanza kuuza maamdazi 10:kwa Siku.
Mkuu wewe una tazama kwa Macho tatizo Lako fikiria boss upyaMaandazi 500 hicho ni kiwanda sasa....hapa Mwananyamala Pamechangamka hivi lakini kina mama wanalaza maandazi yao ya kwenye vibobo vya kg 8 sembuse uko kijijini wanapoamkia viporo na ndizi za kuchoma andazi linanunuliwa lipelekwe kwa mgonjwa aliyelazwa utamaliza 500 baada ya Mwaka!
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa iyo boss wewe una afiki au unapigaWazo Ni Zuri! Lakini Liko Over rated, Ila Ukiwa Nje Utaona Simple, Katika Biashara Wazo Linalo Fanikiwa Ni Lile Utakalo Buni Mwenyewe Sio La Kuelekezwa, Ngumu Kuamini Lakini Ndio Ukweli,
Sawa boss lakini uzi hatuzungumzii kutazama kwa Macho ni akili tu.. Neno akili Lina uwanja mpana SanaSijui watu huwa tunachukuliaje/fafanuaje tukisikia neno biashara/ujasiliamali!mleta mada sina nia kukupinga but hapa inabidi ujue jambo moja.
Hizo nyumba za kupanga siyo wote wanaoshinda majumbani,pia hata wale wanaobaki nyumbani ni kina mama na watoto ambapo hawa kile kiporo kilicholala jana ndo wataamkia kama kitafunwa cha chai huku wakiitafuta saa sita wale chakula shibe.
Ingekuwa rahisi hivyo kila mama mtaani angefanya hii kazi,20K siyo ndogo hii biashala ina changamoto zake.
Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
Mh hesabu zako mkuu hakuna ambae angefanya hizo biasharaLet say unatoa 20 kwa kilo,hapo utahitaji mfuko mmoja wa kg 25 kutengeza maandazi 500,
mfuko mmoja tsh 28000,
mafuta ya kukaangia hata uweke lita 5,hiyo ni tsh 15000,hapo tayari inahesabu 43,000,
ukiweka na mkaa wa 2000,tayari gharama ni 45,000,
unauza unapata 50,000,faida 5000,
hujaweka gharama za hamira,ha ha ha,na umetembea kinondoni nzima kwa miguu kwa faida chini ya 5000,
cost benefit analysis imegoma kutick hapa
[emoji23] Hapa ukitumia Macho lazima ufeli tuNimecheka kdogo....nyumba wapngaj 7 kila 1 akinunu a mandaz 5= 35 apo umeassume bt mambo hayapo hvyo.
Wapangaji WA uswaz huwajui mkuu labda hyo hesabu iwe ya mkopo,
Binafsi nilishafanya biasha kama hizo..cha msingi ni kutafta eneo lenye watu wengi.mm nilianzia mtaani nikajikuta nipo shuleni..nilikuwa natengeneza chapati 100,maandazi 200,sambusa 200,ndizi mzuzu 200,mihogo roba LA kg 50,na ndoo mbili za chips per day..nilitumia kachumbari za aina tofauti ,ukwaju na rosti la mifupa nililokuwa nanunua 2000 kwa kilo katika kunogeshea vitafunwa.Maandazi 500 hicho ni kiwanda sasa....hapa Mwananyamala Pamechangamka hivi lakini kina mama wanalaza maandazi yao ya kwenye vibobo vya kg 8 sembuse uko kijijini wanapoamkia viporo na ndizi za kuchoma andazi linanunuliwa lipelekwe kwa mgonjwa aliyelazwa utamaliza 500 baada ya Mwaka!
Sent using Jamii Forums mobile app