Fursa haionekani kwa Macho bali kwa akili

Fursa haionekani kwa Macho bali kwa akili

Sijui watu huwa tunachukuliaje/fafanuaje tukisikia neno biashara/ujasiliamali!mleta mada sina nia kukupinga but hapa inabidi ujue jambo moja.

Hizo nyumba za kupanga siyo wote wanaoshinda majumbani,pia hata wale wanaobaki nyumbani ni kina mama na watoto ambapo hawa kile kiporo kilicholala jana ndo wataamkia kama kitafunwa cha chai huku wakiitafuta saa sita wale chakula shibe.

Ingekuwa rahisi hivyo kila mama mtaani angefanya hii kazi,20K siyo ndogo hii biashala ina changamoto zake.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Wakuu Leo nimeona nije na Mada hii ili ndugu zangu mlioko mjini mnufaike kupitia mawazo yangu!

Iko hivi mjini Kuna watu wengi tofauti na kijijni. Yaani Unakuta nyumba 1 Ina watu zaidi ya 20 wakiwemo wapangaji including watoto.

Kuna biashara ya vitafunwa yani maandazi ama chapati ama keki nk. Leo nije na maandazi.. Ukitengeneza maandazi 500. @1.Tsh 100 zidisha Mara 500 unapata 50000

Hapo ukitoa garama za Mafuta, mkaa ama kuni, Nguvu nk. Unakuta faida 20000 kwa siku. Zidisha siku 10 una laki mbili pembeni ya mtaji iko pale pale.

Swali unawezaje kuuza maandazi Mia 5 kwa siku?

Jibu: ukipita nyumba 1 yenye wapangaji let say 7.. Kila mtu akanunua maandazi 5 tayari 35 ukizunguka nyumba 20 tayari umemaliza kazi tena asubuhi asubui hapo hujauza wale wa njiani.

Kwa Leo naona niishie hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
Ivi wewe unawajua wabongo kwa kukopi na kupaste. Hiyo biashara utaifanya wiki 2 tu ikilipa wiki ya 3 mtajikuta mko 6 mtaani hapo ndipo utakapoanza kuuza maamdazi 10:kwa Siku.
 
Uswazi kaanga mihogo, weka kachumbali. Kipande 100, utapiga sana hela. Tegesha sehemu ya njiani inayopita watu wengi kwenda au kutoka kwenye shughuli mbalim ali.

2015 nilienda Mwanza, jamaa yangu alinipeleka sehemu inaitwa mabatini. Pembeni ya lile daraja la waenda kwa miguu kunajamaa anakaanga pumbu za mbuzi, ng'ombe na kondoo. Vile vidude ni vitamu sana aisee.

Nb: zingatia usafi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maandazi 500 hicho ni kiwanda sasa....hapa Mwananyamala Pamechangamka hivi lakini kina mama wanalaza maandazi yao ya kwenye vibobo vya kg 8 sembuse uko kijijini wanapoamkia viporo na ndizi za kuchoma andazi linanunuliwa lipelekwe kwa mgonjwa aliyelazwa utamaliza 500 baada ya Mwaka!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu wewe una tazama kwa Macho tatizo Lako fikiria boss upya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui watu huwa tunachukuliaje/fafanuaje tukisikia neno biashara/ujasiliamali!mleta mada sina nia kukupinga but hapa inabidi ujue jambo moja.

Hizo nyumba za kupanga siyo wote wanaoshinda majumbani,pia hata wale wanaobaki nyumbani ni kina mama na watoto ambapo hawa kile kiporo kilicholala jana ndo wataamkia kama kitafunwa cha chai huku wakiitafuta saa sita wale chakula shibe.

Ingekuwa rahisi hivyo kila mama mtaani angefanya hii kazi,20K siyo ndogo hii biashala ina changamoto zake.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
Sawa boss lakini uzi hatuzungumzii kutazama kwa Macho ni akili tu.. Neno akili Lina uwanja mpana Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa upande mwingine wa shilingi hiyo survey yako haijakaa vyema,umesema ukipita kwenye nyumba ya kupanga hapo tayar ni uswahilini, na ki uhalisia ni nadra sana kwa mtu wa uswahilini kununua kitafuno kimoja kwa sh.500. Nawasilisha
 
Ni ubunifu tu kwa kutumia akili Mungu aliyokupa kama haijachakaliwa na binadanu . Mf. Mwalimu ukionekana unauza maandazi kwa wasioelewa watamcheka eti biashara uchwara ! Kwa mwenye busara atapiga mzigo bila kuangalia makunyanzi . Kwa mf . uliotoa wa maandazi kwa kuzingatia kauli nzuri na kanuni za biashara utamuacha mtu aliyeajiriwa mbali .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni wazo zuri,kwa kupanga inawezekana ila ukiingia field ndio changamoto zinaonekana.leo utauza,kesho hautauza utayapeleka wapi?
 
Ishu hapo yanatoka maandazi mangapi kwa kilo moja ya ngano?,
kwa bei hiyo ya sh 100 ni wazi kuwa yatachangamkiwa sana tu na mji kama dar mfano sidhani kama nyumba hapo hazizidi 50,
lakini sasa unatoa mangapi katika kilo ili faida tuione?
 
Let say unatoa 20 kwa kilo,hapo utahitaji mfuko mmoja wa kg 25 kutengeza maandazi 500,
mfuko mmoja tsh 28000,
mafuta ya kukaangia hata uweke lita 5,hiyo ni tsh 15000,hapo tayari inahesabu 43,000,
ukiweka na mkaa wa 2000,tayari gharama ni 45,000,
unauza unapata 50,000,faida 5000,

hujaweka gharama za hamira,ha ha ha,na umetembea kinondoni nzima kwa miguu kwa faida chini ya 5000,
cost benefit analysis imegoma kutick hapa
 
Nimecheka kdogo....nyumba wapngaj 7 kila 1 akinunu a mandaz 5= 35 apo umeassume bt mambo hayapo hvyo.

Wapangaji WA uswaz huwajui mkuu labda hyo hesabu iwe ya mkopo,
 
Let say unatoa 20 kwa kilo,hapo utahitaji mfuko mmoja wa kg 25 kutengeza maandazi 500,
mfuko mmoja tsh 28000,
mafuta ya kukaangia hata uweke lita 5,hiyo ni tsh 15000,hapo tayari inahesabu 43,000,
ukiweka na mkaa wa 2000,tayari gharama ni 45,000,
unauza unapata 50,000,faida 5000,

hujaweka gharama za hamira,ha ha ha,na umetembea kinondoni nzima kwa miguu kwa faida chini ya 5000,
cost benefit analysis imegoma kutick hapa
Mh hesabu zako mkuu hakuna ambae angefanya hizo biashara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maandazi 500 hicho ni kiwanda sasa....hapa Mwananyamala Pamechangamka hivi lakini kina mama wanalaza maandazi yao ya kwenye vibobo vya kg 8 sembuse uko kijijini wanapoamkia viporo na ndizi za kuchoma andazi linanunuliwa lipelekwe kwa mgonjwa aliyelazwa utamaliza 500 baada ya Mwaka!

Sent using Jamii Forums mobile app
Binafsi nilishafanya biasha kama hizo..cha msingi ni kutafta eneo lenye watu wengi.mm nilianzia mtaani nikajikuta nipo shuleni..nilikuwa natengeneza chapati 100,maandazi 200,sambusa 200,ndizi mzuzu 200,mihogo roba LA kg 50,na ndoo mbili za chips per day..nilitumia kachumbari za aina tofauti ,ukwaju na rosti la mifupa nililokuwa nanunua 2000 kwa kilo katika kunogeshea vitafunwa.
 
kutengeneza vitu tofauti tofauti kuna push sana biashara..ila changamoto yake in wasaidizi..na kitu kingine ni kusimamis recipe yako isiweze kubadilika
 
Biashara za whatssap groups huwa ni nyepesi njoo katika uhalisia ujionee tofauti
 
Back
Top Bottom