Money Stunna
JF-Expert Member
- Aug 9, 2011
- 13,053
- 6,304
Kwa yeyote mwenye swali kuhusu fursa za aina mbalimbali katika jiji la mombasa (msa) na kenya in general aniulize hapa.mimi ni mtz mwenzenu niko hapa kwa mwaka wa tano na napenda kumeet na wapiganaji wenzangu wa maisha.
biashara ni mingi ila inategemea ni mtaji wa kiasi gani ulio nao
Vipi pipi kifua(Tropical) box moja wanauzaje?
Nina samaki wa mapambo naweza kupata soko la uhakika?
Wewe chalii ungeanza kwanza kutwambia fursa ambazo zipo uko kenya,acha maneno mingi weka fursa hapa sio mambo za pm utaonekana mkola tu
leta vitunguu saumu kutoka manyara utapiga pesa
samaki hapana usilete kama uko arusha leta majani ya tumbaku ya kutoka ARUSHA hata kontena tatu kama unaweza
VP kuhusu majani ya tumbaku kutoka kilindi tanga hayana soko halo msa? mi nataka niwe naleta Ugolo na iriki je inalipa?
mambo si hayo,la kuongezea ata ukipeleka Uganda pia inalipa sana,kuna mdada alikuwa anafanya hizo biashara alikuwa anasema alikuwa anatoa morogoro,alipiga sana pesa sema nilipoteza mawasiliano naye
usipeleka uganda pesa yao haina maana,labda rwanda
hiriki ndo biashara yangu,kwa mgen itakugharimu muda na pesa, tumbaku leta ya kutoka arusha au tabora,hizo ndizo zijulikanazo. , , ,, , ,
ukilinganisha na dollar rate iko ivi sasa
1 USD =3040 UGsh
na inazidi kuporomoka,kwa sasa hivi bora ununue kule,uko sahihi si muda wa kupeleka kule,labda kununua vitu vya UG
Nashukuru Mkuu. Ila tumbaku ninayoongelea hapa ni ile ya kienyeji wanayisindika Ugolo. Ntakucheki bàadae unipe muongozo kwa kina.
wacha nikupm namba ya dealer mmoja wapo wa tumbaku,ako mtaa waitwa gurshan street mombasa near masjid mussa
Kenyan detected..
asante kwa fursa..ninaswali. hii tumbaku unayosema ya kusindika kienyeji ikoje?pili kwa nini ya arusha na tabora?
MSILETE KARANGA HUKU, KARANGA ZA HUKU NI KUBWA KULIKO ZA TANZANIA,NINA HAKIKA HAMJAWAH KUZIONA,LETENI KOROSHO ,wenyewe wanaita chaoro
jadili mada sio kujadili utaifa wa mtu....!!