FURSA: Kama unataka kufanikiwa pita hapa

ForeverMore

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2014
Posts
812
Reaction score
1,939
Tanzania tuna shida kubwa sana la ajira. Haswa kwa sisi vijana. Na kila mtu anakwambia jiajiri, na karibia wote wanaokwambia ujiajiri wanasema ujiajiri kwenye kilimo. Wakati huo huo bado kuna malalamiko makubwa sana kutoka kwa wakulima kwa kukosa masoko au bei za mazao kushuka.

Sasa unajiuliza hivi kweli niingie kwenye kilimo? Je fursa ya kujiajiri ipo kwenye kilimo tu? Mtazamo wangu ni kwamba kichwa chako ni mtaji wako, ujuzi wako ni mtaji wako, utundu wako ni mtaji wako na elimu yako ni mtaji wako. Tatizo ni kwamba unautumiaje huo mtaji wako kujipatia hela? Hapo ndo kwenye utata.

Kila mtu atasema lake na wala sipo hapa kupingana na yoyote na wala kukwambia usiingie kwenye kilimo ama kilimo hakilipi, hapana, kila mtu anazali lake na ana njia zake zinazoweza kumtoa kwenye ishu yoyote atayoamua kufanya.

Ila sasa, ningependa kuongelea fursa ya kujiajili kutumia mtaji ulionao (kichwa, ujuzi, elimu na hobi). Uwezekano mkubwa ni kuwa freelancer, yaani kujiajiri binafsi.

Kwa mfano, wewe upo vizuri kwenye kuchoma nyama, je ujuzi wako unawezaje kuutumia kujipatia ama kuongeza kipata? Ukiangalia kuna watu wengi wanafanya sherehe ndogo ndogo majumbani, hawa watu wanaweza kukuita kuwachomea nyama. Tatizo ni kuwa utapata wapi mtu anayetarajia kufanya sherehe akupe kazi? Jibu lipo mwishoni.

Wewe mwanachuo au muhitimu wa chuo, ukiangalia vizuri, elimu uliyo nayo unaweza wafanyia watu kazi mbali mbali. Tatizo ni kama la hapo juu, kupata wateja.

Kila mnaweza fanya kazi ya freelancing kama hauna ujuzi unaweza kujifunza jinsi ya kufanya chochote kama upigaji picha, graphic designing na kadhalika.

Sasa basi bongo, kuna hii site ya freelancing inaitwa ajiras.com ambayo unaruhusu upost kazi yoyote unayoweza kufanya ili watu wanao hitaji wakupate hapo.

Leo nipo hapa uniulize chcote kuhusiana na hiyo site na inawezaje kukusaidia. Uwanja wenu.
 
Ok mnafadikaje ninyi endapo mtu atapata tenda kupitia platform yen
 
Nimeipenda
 
Ok mnafadikaje ninyi endapo mtu atapata tenda kupitia platform yen
Swali zuri, Kampuni inachukua 10% ya mauzo, asilimia hiyo siyo yote faida ya kampuni.
Mfano: 1. mteja anaponunua kwa tigopesa (nyingine zinaongezwa soon) hatokatwa ila ada ya kutumia tigopesa, kwenye 10% sisi tunawalipa tigo.
2. Kuna huduma ya sms utakayokuwa unapokea kila utakapo tumiwa message mtandaoni (hii inasadia kama hauna bundle) na pia utapokea sms upipata order mtandaoni pia.
3. Kuna program ya referral (affiliate) ambayo mtu anaweza kuitangaza website, na kama mtu atabonyeza link na kununua au kuuza huduma ndani ya miezi 3 kwanzia alivyobonyeza link, tunakupa commission Pia unaweza tangaza kazi ya mtu aliyoweka mtandaoni, mtu akinunua hiyo kazi kwa kupitia link yako ndani ya miezi mitatu pia tunakupa commission kutoka kwenye 10% ilele.

Kwahiyo unakuta sisi kama kampuni tutabaki labda na asilimia 3 au 2. Ukiangalia hii pia ni fursa, Tangaza website au kazi za watu mtandaoni na utapata commission na pia utakuwa umemsaidia mtanzania mwenzio kupata mteja.

Kama una blog au group la facebook, hii fursa inakuhusu sana. wenye blog wanaweza ongeza category (niche) ya wajasiliamali na kuwa unapost maelezo kuhusu kazi za watu toka ajiras na kuweka link. Wateja wako watabonyeza link na utapata commission. Kwa hiyo badala ya kutegemea adsense peke yake unaweza ingiza hela kwa njia hii nyingine pia.
 
Maelezo yote hayo bila kuweka hata link mkuu?, nice idea nmeipenda hii ngoja ni digest kwanza i will be back kuuliza maswali!
 
Link ipo, angalia paragraph ya pili kutoka mwisho utaona ajiras.com. Nikiweka. Link. Kabisa moderators wanafuta post.
 
Nyuz kma hiz wachangiaji huwa wachache..ila zile za wakina zari, mobeto, gmoney wachanhmgiaj lukuki.
 
Kweli kabisa, tunapenda kulalamika zaidi kuliko kufanyia kazi fursa zinazojitokeza. Tunapenda starehe kuliko kazi. Utashangaa mwezi mzima page bado ina comments za kutosha.
 
Back
Top Bottom