Fursa katika kilimo cha viazi lishe, tuchangamkieni upesi

Mkuu unaweka tanagzo afu ukitumie txt kwenye simu yako hujibu.
Umakua naana gani?
 
Aman, hebu fafanua hili. Kwenye andiko la kwanza kuhusu upandaji wa mbegu shambani ulisema kutoka tuta hadi tuta ni FUTI MOJA; katika andiko hili la pili unasema ni MITA MOJA! Which is which, FAFANUA TAFADHALI.
 
Vil
Demand take ni majanga bora mihogo,songea kule yangu miaka ya2000s vinalimwa tumekula sana tukiwa shule na njiani along songea njombe road wakulima walikuwa wanapanga magunia kutafuta Wateja kwa bei chee sijui kwa sasa
Vile viazi vya Songea si viazi lishe ni viazi tu vya kawaida
 
*USIPITWE NA FURSA YA KILIMO CHA VIAZI LISHE*

Je unapenda kuzalisha Viazi lishe katika msimu huu wa kilimo? Kinasoru Easta Africa Tanzania Ltd, iko tayari kukuuzia mbegu bora za viazi hivyo kwa bei ya shilingi 50 tu kwa mbegu moja.

Ekari moja kubwa yenye Mita
70 X 70 inahitaji mbegu 16,310. Wakati ekari moja ndogo ya Square Mita 4000 inapanda mbegu 12,000. Upandaji kati ya shina na shina ni futi moja sawa na sm 30 wakati kati ya tuta na tuta ni mita moja sawa na sentimita 100.

Tuta la linalotakiwa kupandwa viazi lishe linapaswa liinuke juu angalau sentimeta 20 na ujazo wake unapaswa uwe na sentimita 30. Kadiri tuta linavyokuwa kubwa ndivyo linavyotengeneza viazi vikubwa.

Viazi lishe toka kupandwa hadi kuvunwa huchukua muda wa miezi mitatu.

Viazi lishe ni aina ya viazi vitamu vyenye rangi kama ya karoti kwa ndani ukivimenya. Viazi hivi vina vitamini A kwa wingi ambayo ni muhimu sana kwa akina mama wajawazito, wanaonyonyesha, watoto wadogo na hata wazee kwa ajilibya uimarishaji wa afya.

Unga unaotokana na viazi lishe licha ya kutumika kwa ajili ya kutengenezea unga wa lishe na kupikia ugali, lakini pia unatumika pia kwenye utengezaji wa bidhaa zote ambazo unga wa ngano unatengeneza. Mfano cake, chapati, maandazi, mkate, sambusa nk.

Tunakukaribisha sana ndugu mteja wetu kama utahitaji viazi lishe vyenyewe ama mbegu zake. Tuna mbegu za kutosha na viazi vingi. Tupe oda yako sasa tukuhudumie popote ulipo.

Huna haja ya kuchelewa, changamkia upesi fursa hiyo. Kwa oda tafadhali piga simu namba 0767989713 au 0715989713

Asante sana.
 
KULA VIAZI LISHE, LIMA VIAZI LISHE

Mzigo huo. Hivi ndivyo viazi lishe vyenye matumizi kedekede katika mwili wa mwanaadamu. Unaweza kutumia viazi hivi katika utengenezaji wa cake, maandazi, ungalishe, ugali, biscut, crisps, ama kula vyenyewe kwa kuchomwa, kukaangwa au kuchemshwa.

Viazi lishe ni katika vyakula vyenye vitamin A kwa wingi. Vinawafaa sana akina mama wajawazito, wanaonyonyesha, watoto pamoja wazee.

Kazi kubwa ya vitamin A katika mwili wa Binaadamu ni pamoja na kusaidia katika utengenezaji na uimarishaji wa meno na mifupa. Pia husaidia katika uchocheaji wa uonaji wa macho hasa kwenye mwanga hafifu.

Vitamin A inasaidia vilevile kwenye ukuaji wa kitoto kichanga kiwapo tumboni mwa mama yake, inasaidia pia kwenye uumbikaji wa miguu na utengenezaji wa moyo, macho na masikio. Kwa hiyo ulaji wa viazi lishe una manufaa makubwa kwetu sote bila kujali umri. Viazi lishe ni katika vyakula bora sana.

Unga wa viazi lishe kwa siku za hivi karibuni umekuwa hitajio kubwa kwa akinamama wajawazito, watoto wanaonyonya na wezee wenye Kisukali. Lakini pia chanzo kikubwa cha kipato kwa wadau waliyojitumbukiza kwenye mnyororo mzima wa thamani wa kilimo hiki.

Kula viazi lishe, Lima viazi lishe, hii ndiyo kuuli mbiu yetu.

Ukitaka kula viazi lishe tuone tutakuuzia viazi hivyo na ukitaka kupanda viazi hivyo halikadhalika tutakuuzia mbegu za viazi hivyo zitakazokuwezesha kuwa mdau wa kilimo hicho. Na hii ndiyo kazi moja wapo ya Kinasoru East Africa Tanzania Ltd

Aman Ng'oma
0767989713
Dodoma
 
Yaani nyie wakulima wa laptop expenditure umeficha au umeacha maksudi ili kuwaadaa watu waone kama Ni fursa nway pambana Na Hali yako
 
Ma viazi yenyewe hayana soko, Nyie jidanganyeni muingie kichwa kichwa.
 
mkuu tunaomba kamrejesho kidogo
Mavuno hayakuwa mazuri, wataalaam wakaniambia nilichelewa kupanda na mvua za mwisho. Nimeandaa mbegu nitawahi mvua za awali mwaka huu.
Karibu nikuuzie mbegu Mdau
 
Mna mawakala mikoa mingine? Maana sisi huku huu ndo msimu wa mvua.
 
mkuu tunaomba kamrejesho kidogo
Aiseh calculator ni tamu sana kwakuiangalia ikiwa na mahesabu ya makisio matharani ma figure ya sufulisufuli yakigeuka kuwa reality basi unaweza ukaamka ukizani umekuwa tajiri kumbe ilikuwa ni makisio ya JF uliokuwa umeota ndotoni
 
weldone Chaps
soko lake linapatikanaje? tunataka tuwe na uhakika ili tukiweka mtaji wetu tujiamini, ni masoko haya ya kawaida ama kuna soko maalumu?
 
Ninavyo hivi ,mbegu ilitoka Dar,pia niliona Nakumat wakiuza bidhaa zake,wengine huita viazi vya Msumbiji,tatizo ni kuwa wengi hawajui manufaa na utofauti wa viazi hivi na hivyo vingine
 
kilimo cha karatasi na namba kinavutia sana.
ukiingia field sasa!!
tunaomba mrejesho kwa waliolima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…