Fursa katika kilimo cha viazi lishe, tuchangamkieni upesi

Fursa katika kilimo cha viazi lishe, tuchangamkieni upesi

Mkuu umetoa ufafanuzi upande wa mbegu na mavuno Je vipi kuhusu mahitaji mengine kama madawa & mbolea yanaendaje kwa ekari...
 
FURSA KATIKA KILIMO CHA VIAZI LISHE, TUCHANGAMKIENI UPESI – 2

Kama ilivyo ada ya kampuni yetu ya Kinasoru East Africa Tanzania Ltd kuwa mstari wa mbele katika kuwaonyesha watu fursa, leo hii tutaendelea na sehemu ya pili ya ile fursa yetu katika kilimo cha Viazi Lishe. Nashukuru sehemu ya kwanza iliweza kuvuta hisia za watu wengi kutokana na idada ya simu tulizopigiwa na simu hizo kwakeli zilikuwa zikitoka kwa watu na maeneo mbalimbali ya nchi yetu na wengi wao walihitaji kujua zaidi kuhusu kilimo hiki, namna kinavyolimwa na fursa yake kibiashara.

Leo nimeona niendelee na sehemu ya pili ili kutoa elimu zaidi juu ya kilimo hiki cha Viazi Lishe.

Kilimo chochote siku zote lazima kilenge biashara. Na unapolima unapaswa kujua kuwa unalima kwa lengo la biashara na si vingivyo. Lazima gharama zote zinazohusika katika kilimo chako uzinakili pembeni katika daftari lako la kutunzia kumbukumbu ili mwishowe ziweze kukusaidia kujua kama umepata faida au hasara katika kilimo hicho.

Kimsingi Viazi lishe ni chakula kizuri, kitamu na chenye vitamin A kwa wingi ambayo ni muhimu sana kwa akina Mama wajawazito, wanaonyeshesha , watoto na hata wazee. Pamoja na hali ngumu ya kiichumi iliyopo sasa bado Viazi lishe vina uhakika mkubwa wa kupata soko kutokana na vyenyewe kuwa sehemu muhimu ya chakula cha watu. Siku zote watu watajinyima kwenye baadhi ya mahitaji lakini kamwe hawawezi kujinyima kwenye suala la chakula. Chakula watu watakula katika hali yoyote ile iwavyo.

Upekee wa viazi hivyo unaongeza soko zaidi. Rangi yake ya njano kwa ndani kama ya karoti inamvuto wa kipekee kwa walaji. Ndiyo maana kukiwa na wakulima wawili tofauti, mmoja kalima viazi lishe na mwingine kalima viazi vitamu vya kawaida, pamoja na kwamba vyote ni viazi vitamu, wakienda sokoni kwa pamoja, mkulima atakayeanza kuuza viazi vyake mapema ni yule aliyelima Viazi Lishe na huu ndiyo ukweli. Viazi Lishe vina mvuto wa aina yake machoni kwa watu, ladha nzuri mdomoni, kuwa na unga wa kutosha pale vinapopikwa ni katika vitu vinavyoongeza thamani ya viazi hivyo. Mahitaji ya viazi hivi ni makubwa sana, si kwa kwa soko la ndani pekee bali hata soko la nje ya nchi vinahitajika sana kutokana na kuwa na mchango mkubwa wa vitamin A kwa mlaji. Vilevile viazi hivi vina matumizi mengi kama nilivyoanisha katika makala yangu ya sehemu ya kwanza niliyoelezea fursa hii ambapo kwa ufupi unga wa Viazi Lishe unatengeza bidhaa zote zinazotengenezwa na unga wa ngano. Lakini ziada iliyonayo Viazi Lishe, unga wake unatumika kwa ajili ya kupikia ugali. Haya ni mapinduzi katika kilimo. Kilimo cha aina moja lakini kina faida lukuki.

Kilimo cha Viazi Lishe si kigumu kuendesha na vilevile hakihitaji sana maji mengi kutokana na kuwa Viazi ni miongoni mwa mazao yanayostahimili ukame. Viazi Lishe vinaweza kulimwa kwa kutumia mvua katika kile kipindi cha mvua au kama mkulima ana vyanzo vya maji anaweza kuendesha kilimo hiki kwa njia ya umwagiliaji. Ikiwa njia ya umwagiliaji itatumika, mkulima ataweza kuzalisha Viazi mara nyingi zaidi kwa mwaka. Na kwa kawaida Vazi Lishe hutumia miezi mitatu toka kupandwa hadi kuvunwa kwake.

Katika ekari moja ya mita 70 x 70 ambayo ni sqm 4900 yenyewe itapanda mbegu 16310, kwa maaana kwamba nafasi kati ya shina na shina ni futi moja yaani sentimeta 30 sawa ukubwa wa rula moja na kati ya mstari na mstari au tuta na tu ni mita moja yaani sentimeta 100. Lakini kitaalamu ekari moja ina ukubwa wa sqm. 4000 ambayo karibu mita 65 x 61.6 ambapo yenyewe itapanda mbegu 12,000. Ekari moja ina uwezo wa kutoa mavuna zaidi ya tano 20 huku tani moja ikiwa sawasawa na kilo 1000, kwa hiyo kwa tani 20 ni sawasawa na kilo 20,000. Na kila kilo moja inauzwa kwa wastani wa Tsh. 1000. Hii ndiyo fursa katika kilimo cha viazi lishe.
Karibu uingie katika hii fursa. Tuna mbegu za kutosha tena zile daraja la kwanza yaani F1. Mbegu zenye kukuhakikishia mavuno ya kutosha.

Aman Ng’oma
Mkurugenzi Mtendaji
Kinasoru East Africa Tanzania LTD
DODOMA
0767989713/0786989713
 
CHANGAMOTO zinazolikumba zao la viazi lishe Wilayani Sengerema zinaathiri biashara ya zao hili, kama ilivyobainishwa na wafanyabiashara katika eneo hilo.

Changamoto hizo ni kama ukosefu wa soko la uhakika, gharama za usafirishaji na gharama za maandalizi ya shamba, matunzo hadi mavuno na uhaba wa zao hilo.

Wafanyabishara wanasema kuwa kutotatuliwa kwa changamoto hizi kunakwamisha maendeleo ya zao hili kwa mkulima na wafanyabiashra.

Mabura Kisinza, ambaye ni mfanyabiashara anasema kuwa kila gunia moja la viazi lishe hutozwa shilingi 3000 kila linapopita katika halmashauri na pia linapokuwa sokoni.

“Kwa jumla tunatoa shilingi elfu 9000 kwa kila gunia,” alisema Kisinza.

Hata hivyo hizi ni sehemu ya gharama nyingi zinazolikumba zao hilo, nyingine zikiwa ni nauli ya gunia moja ambayo ni shilingi 5,000, malazi ya mfanyabiashara ni shilingi 10,000 kwa siku moja.

Gharama nyingine ni mbegu za zao hili, gharama za kulima shamba, kuvuna, vyombo vya kuwekea mazao na pia kuanika na kuanua.

Mfano pisi mia 3000 zenye urefu wa futi moja , huuzwa kwa shilingi elfu 5000, gharama za mavuno ekari moja ni shilingi elf 40000, malipo ya vibarua, gharama za kuanika viazi lishe na kuanua shilingi elfu 30000 kwa siku moja.

Gharama za mifuko ya kuwekea viazi kila mguko wanaununua shilingi elfu 2500,.

Pamoja na changamoto hizo, ilibainika kwa zao hili bado lina soko kuwa hii hutokana na kuwa gunia moja huuzwa kwa shilingi 40000 na kufanya mkulima kupata shilingi 1200000 kwa ekari.

Hii ni kwa sababu ikiwa ekari moja itasitawi zivuri, inaweza kutoa gunia 30 za viazi ambazo kila moja huuzwa shilingi 40000 kutegemea bei ya zao hilo.

Katika Wilaya ya Sengerema ,Viazi lishe vinalimwa katika kijiji cha Tunyenye kata ya Kishinda , kata ya Nyampande, Ngoma , Nyakalilo, Nyanzenda, Iligamba, na kata ya Itabagumba.

Kilimo cha viazi katika Wilaya ya Sengerema kipo chini ya mkakati uitwao Mradi wa malando bora kutoka kwa wafadhili kwa kushirikiana na Tanzania Home Economics.

Kupitia mradi huo, 2008 wakulima walipatiwa elimu kuhusu kilimo hicho ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wake.

‘’Elimu ya ushawishi wa kuanzisha kilimo hicho hulifanyika katika wilaya nzima ambapo sisi kikundi cha Manyara tulikuwa jumla ya wanachama 16, wakiume wakiwa 6- wakike 10,’’ Anasema mwenyekiti kutoka kijiji cha Tunyenye Justace . N. Kabipi .

Mafunzo hayo wanasema yalitolewa mara tatu kwa vipindi tofuti , walifundishwa mafunzo ya mbegu za malando Bora kwenye vitaru, upandaji na utunzaji baada ya kuvuna.
“Baada ya zoezi la kufyeka shamba kukamilika , viazi uchimbwa kwa kutumia majembe ya mkono baada ya hapo wanachambua vibovu na vilivyokatakatwa ,vibovu utupwa huku vilivyokatwa katwa na jembe wakati wa kuvuna humenywa na kutengezwa machembe “ wanasema Saimon . S. Igogoti na Zurupha .H.Hamza.

“Viazi vinavyobaki hutunzawa ndani ya shimo linalochimbwa nje kama chakula cha ziada ,na ukaa zaidi ya miezi sita bila kualibika , njia hii hutusaidia kuhifadhi chakula wakati wa njaa na kwa matumizi ya badae” wanasema. Makankabila .J. Mabura na Veridiana .p. Ngaya.

Kufikia mwaka 2014 mwezi wa tatu idadi ya wanakikundi ilishuka na kufikia wanachama 5 , hali hii ni kufuatia na tamaduni Mbovu zilizotanda katika kabila ya wasukuma kuwa mwanaume kulima malando ni jambo la aibu katika jamii inayowazunguka ,na hiyo hali inavikabili vikundi vyote ambavyo vinalima viazi lishe katika wilaya hii.

Hata hivyo walioendelea na kilimo hicho wanasema kimewaongeze kipato katika familia zoa ,wamejenga , wanasomesha wototo pia wanunua vitendea kazi vya kisasa ,mfano power tiler,water pampu, wamesajiri vikundi vyao .

Mafanikio hayo yanatokana na juudi zao binafsi kwa kushirikiana na ushauri kutoka kwa wataalamu wanaopatiwa na maofisa ugani wa vituo vya ukiriguru kwa kushirikiana na ofsa kilimo wa mazao ya mizizi, Piusi . Z. Nhunda wa Halmashauri wilaya ya Sengerema.

Katika Mafanikio hapakosi changamoto , ambapo wanakabiliwa na ukosefu wa soko la uhakika , hata hayo machache yaliyopo sio ya uhakika ,wanaitaka serikali iwasaidie kuondoa kero hizo ili waweze kwendana na kilimo biashara.

Masoko hayo ni soko la kilumba na soko kuu la jijini yaliyopo mkoani Mwamza pamoja na soko kuu lilipo mkoani Geita.

Hata hivyo kumekuwa na upinzani wa mbegu hizi kutoka kwa walaji kwani wanasema asili ya zao hili ni tofauti na lile walilolizoea.

‘’Kwanza sio vitamu ,pili havina radha ya kuliwa kama radha ya viazi vitamu tulivyovizoe tangu tumekuwepo,tunasema asilimia kubwa kwanza viazi lishe havijulikani katika jamii ya wengi , hata hawa wanaovilima vinawashinda kuvitumia kama chakula badala yake wanatangangata kuchanganya na viazi vitamu kwaajiri ya chakula’’ wanasema walaji. Editha .S. Silivesta na Godifry .M.Nestory.

Watumiaji wanasema serikali inatakiwa kuwa makini kwa kuwazui wafadhili kupitia mashirika mbalimbali yanayopokea mbegu za kisasa na kuathiri mbengu za kizamani ,na kusabaisha kuwanufaisha wa simamizi ya mamiradi na sio jamii.

Ofisa kutoka Tahea Mohemed Bundara kwa kushirikiana na Deusi Peter, mtaalam mwelekezi wa zao hili ,wanaonekana kuficha ukweli juu ya faida ya viazi lishe na kusema kuwa ni zao ambalo linakubalika kwenye jamii ,tofauti na uhalisia baada ya uchunguzi kufanyika na mwandishi wa habari hizi na kubaini asilimia 55 viazi lishe havina mapokea kwenye jamii na asilimia 45 ya wananchi wa kanda ya ziwa vinapolimwa hawavijui.

Katika hali ya kushangaza zao hili halijafanyiwa utafiti tangu mwaka 2010 mavuno yalipoanza.

“siwezi kujua ni asilimia ngapi sasa kimeongeza uchumi wa nchi ,na kwa upande wa soko lipo igawa bado halijaimalika pia hatujafanyautafiti” anasema Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka chuo cha utafiti Ukirigulu (Mwanza) Maliana Mathayo

Mathayo,anasema viazi lishe usaidia kurudisha afya za watoto wadogo wenye umri wa chini ya miaka mitano ,pia vina vitamini A, vinasaidia kuboresha afya za akina mama wajawazito na kuongeza kinga kwa watu wenaoshi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi .

Mwaka 2008 tangu mradi huo unaanza ulilenga wakulima zao hilo kama kinga ya njaa ,kuboresha afya na biashara ,ambapo wakulima wanauza mbegu na bidhaa zilizosindikwa, mfano andazi, chichili, donate,na unga,ambazo uhuzwa migahawani, mashuleni na madukani.

Mradi huo ulianzishwa Mkoa wa Mwanza katika wilaya za Sengerema ,misungwi Ukelewe , Mkoa wa kagera wilaya ya Bukoba maeneo hayo pia wanazalisha kilimo hiki .

Wataalam wa wazoa hili wanasema zao hilo hustawi katika sehemu tambarale zenye udongo tifutifu unaoruhusu maji kupenya.

Udongo wanasema usiofaa kwa kilimo ni udongo wa mfinyanzi na wenye kokoto, ambapo zinatajazwa mbegu bora za malando zinazolimwa kwa asilimia 75 nchini kuwa ni mbegu ya kabonde, kaloti c,kaloti d, na polista.

Viazi vya njano(viazi lishe) niana ya viazi vitamu ni kati ya mazao ya mizizi yenye vitakaloti ambayo ni plikacha ya vitamin A ,kiwango kinachotokana na lishe ya zao hili bado wataalam hawajawa na takwimu sahii za kubaini thamani ya lishe ya zao hili.

Mkakati serikali kwa kushirikiana na wataalamu kutoka chuo cha utafiti wa mazao Ukiliguru ,wanasema kutokana na umuhimu wa viazi lishe katika jamii ya sasa watanaendelea kuwamasisha wakulima na wanachi kwa ujumla kuendelea ili watambue faida za zao hilo.

Mradi wa marando bora ni mzuri na mbegu zake ni zuri pia soko lipo japo sio la huhakika .,Endapo serikali inamkakati wa kuendeleza mradi huu haina budi kuondoa changamoto zinazolikabili zao hii ili kwendana na makakati wa kuleta matokeo chanya(BRN) katika sekta ya kilimo.
MWISHO.
 
Mkuu Naona umeanza vizuri lkn mwishoni kumbe Ni tangazo la biashara. Kuna kitu kikubwa hujakiongelea kiundani kikaeleweka. Unasema vinalipa Na ukaweka hesabu Za gharama Na faida Kwa ekari moja Ila hili soko unalosema hujaliongelea Kwa undani. Embu tuambie huko sokoni Ni wapi exactly? Ina maana Leo Hii nikivuna nikaenda kariakoo Au Mabibo Au Temeke sterio naviuza vyote fasta?
 
FURSA KATIKA KILIMO CHA VIAZI LISHE, TUCHANGAMKIENI UPESI - 3

Niliamua kwa dhati kabisa kuileta fursa hii kwa Watanzania wenzangu kama njia mojawapo ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na yenye biashara kubwa hasa kutokana na viazi hivyo kuwa na vitamini A kwa wingi kwa ajili ya kuimarisha afya ya watoto, wamama wajawazito, wanaonyonyesha na wazee. Pili nililenga kufungua milango ya fursa mpya kwa wakulima. Na tatu nilenga kuongeza wigo wa uzalishaji wa mazao ya kilimo biashara yenye uwezo wa kumuinua haraka mkulima kiuchumi. Viazi lishe ni miongoni mwa mazao ya chakula yenye ustahimilivu mkubwa dhidi ya ukame, kama vitawekewa msukumo katika uzalishaji wake nchini Tanzania tutasahau tatizo la njaa kwa baadhi ya maeneo ya nchi yetu kutokana na viazi hivyo kutumika katika matumizi mbalimbali kama vile unga wake kutumika kupikia Ugali, kutengenezea vitafunwa vya aina mbalimbali na majani yake kwa upande mwingine hutumika kama mboga.

Toka nilipoanza kutoa mfululizo wa makala zangu za fursa katika kilimo cha viazi lishe, watu wengi wamevutiwa na kilimo hiki ingawa wengi wao wameingiwa na hofu kidogo juu ya upatikanaji wa masoko. Na wasiwasi huu umetokana na hasa sababu kuwa wakulima wengi hawana taaluma ya masoko. Wao wakisha lima wanasubiri majaliwa ya wateja. Matokeo yake wakulima wanaangukia kwenye mikono ya madalali ambao hulangua mazao yao kwa bei ndogo nakuuza kwa bei kubwa. Kimsingi anayenufaika na kilimo cha mkulima ni dalali na si mkulima mwenyewe.

Nakumbuka mwaka jana kufuatia kauli ya Mheshimiwa Rais kuwataka watanzania waache kucheza pool table, bao na kunywa pombe nyakati za kazi na badala yake wachape kazi. Vijana wengi waliitikia wito huo na kuamua kuachana na mambo yote yasiyokuwa na msingi kwao na kutafuta kazi zenye tija za kufanya, kuna wale walioamua kujishughulisha na kilimo cha Matigiti Maji, kuna wengine Nyanya na wakati wengine waliamua wajishughulishe na ufugaji wa Kuku ilimradi tu kila kijana kila mtanzania anakuwa na shughuli ya kufanya. Na matatizo yaliyojitokeza katika kilimo cha Nyanya na Matigiti Maji nadhani sote tuliyaona, wakulima walikosa soko, Nyanya zilikuwa zinaoza hovyo, huku Matigiti Maji yakiuzwa chini bei inayoruhusu mkulima kupata faida.

Tatizo letu kubwa Watanzania ni kuwa tukishaambiwa kitu fulani ni fursa basi wote tunahamia huko matokeo yake uzalishaji unakuwa mkubwa kuliko uwezo wa soko letu na maafisa biashara na masoko na Mabalozi wetu mbalimbali wanaowakilisha nchi yetu nchi za nje hawajaamua kwa dhati kusaidia upatikanaji wa masoko kwa ajili ya wakulima wetu pamoja na kwamba uwezo huo wanao kutokana na kuwa na taarifa za kutosha za masoko.

Kwa mantiki hiyo ni muhimu kwa wakulima wetu kupata maarifa na ujuzi wa kutafuta wenyewe masoko. Ili kupata masoko ya uhakika kwanza lazima uwe na taarifa muhimu ya mahitaji ya bidhaa yako unayozalisha, wapi hasa inahitajika na kiwango gani, gharama za kusafirisha hadi sokoni zikoje, bei ya kuuzia nayo ikoje. Je kuna umuhimu wa kutafuta wakala atakayechukua mzigo wako wote kwa bei ya jumla au utapeleka mtu wako na kumfungulia ofisi kisha kumpeleka mzigo na akauuza kidogo kidogo kwa niaba yako ? Hapo utaangalia wewe kama mkulima namna itakavyokulipa. Kwa kawaida soko halimfuati mkulima ila mkulima anatakiwa kulifuata soko. Lazima uwe na namna ya kuwafikishia wateja wako taarifa sahihi juu ya bidhaa uliyonayo au unayoizalisha. Hupaswi kuogopa kuzalisha kwa kukuhofia soko, tengeneza mtandao watafute wenye ujuzi wa kutafuta masoko wakusaidie.

Kitu kingine ambacho ni muhimu katika masoko ni kuwa na umoja miongoni mwa wakulima. Umoja unasaidia kwanza kufahamiana, nani ni nani na anazalisha katika kiwango gani na pia kusaidiana pale mkulima mmoja anapokuwa na tatizo liwe la kitaalamu au jingine na kitu kingine umoja unasaidia kwenye upatikana wa soko la uhakika. Kwasababu wakati mwingine soko linakuja kubwa na mkulima mmoja hawezi kulitosheleza lakini kunapokuwa na umoja miongoni mwa wakulima ni rahisi kukusanya mzigo kutoka kwa kila mkulima na hatimaye kutimiza mahitaji ya soko.

Umoja unasaidia pia kwa maafisa masoko na biashara kujua uzalishaji wa zao fulani uko katika kiwango gani na hivyo kurahisisha kutafuta soko kadiri ya uzalishaji uliopo.

Kwa mfano sisi tunahamasisha kilimo cha viazi lishe na mara nyingi kama kampuni huwa tuna wajibu wa kumsaidia mkulima wetu kupata soko la uhakika la mazao yake, kwa watu wa Dodoma na Morogoro wanalijua hili. Soko ni kubwa tatizo ni kukosa taarifa sahihi za masoko. Ofisi yetu kwasababu inafahamika inajihusisha na shughuli za kilimo biashara, wateja wengi wakubwa wanapokuwa wanahitaji bidhaa fulani huwa wanakuja ofisini kwetu na kuulizia uwezekano wa kupatikana kwa bidhaa husika. Na kwasababu tunakuwa na wakulima wetu outgrowers wengi hivyo inakuwa rahisi kuwa na majibu ya haraka ya upatikanaji wa mzigo unaohitajika.

Kwa kawaida unapofanya kilimo lazima uwe na hesabu, usilime tu. Kila zao lina wakati wake ambao linakuwa na uhitaji mkubwa, kwa mfano mazao yenye jamii ya mizizi katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani mahitaji yake ni makubwa sana. Kwahiyo ukizalisha kwa hesabu hutajuta kukosa soko. Lakini vilevile kwa sababu ni chakula cha bei ya chini watu wengi wanahitaji kama chanzo cha chakula kwa famila hivyo kuongeza wigo wake wa soko.

Kitu kingine muhimu katika masoko usizalishe kwa kufuata mkumbo maadam watu wengi wanazalisha au wanasema kilimo fulani ni pesa nawe ukajiingiza huko, fanya utafiti wa kutosha na ukijiridhisha anza sasa kuzalisha. Katika kufanya utafiti ni muhimu ukawatumia wataalam wakusaidie kufanya upembuzi yakinifu juu ya mradi wako. Usifanye mwenyewe.

Halikadhalika, katika kuimarisha masoko ya mazao yetu muhimu kuyaongezea thamani yake. Fanya usindikikazi. Kilimo kama cha viazi lishe kina matumizi mengi. Usindikaji utaongeza soko zaidi kwa mazao yetu. Lazima wakulima tujifunze elimu ya usindikaji. Yaani wengine walime na wengine wasindike na hivyo kuongeza thamani ya bidhaa husika na hivyo kutengeza masoko ya uhakika.

Aman Ng'oma
Mkurugenzi Mtendaji
Kinasoru East Africa Tanzania Ltd
Dodoma.
0767989713/0786989713
 
Mkuu Naona umeanza vizuri lkn mwishoni kumbe Ni tangazo la biashara. Kuna kitu kikubwa hujakiongelea kiundani kikaeleweka. Unasema vinalipa Na ukaweka hesabu Za gharama Na faida Kwa ekari moja Ila hili soko unalosema hujaliongelea Kwa undani. Embu tuambie huko sokoni Ni wapi exactly? Ina maana Leo Hii nikivuna nikaenda kariakoo Au Mabibo Au Temeke sterio naviuza vyote fasta?
Mkuu yaani tuseme tupo kwenye mtihani na niliahidi kukusaidia, sasa nimekuwekea mtihani wangu uibie vizuri alafu bado uniulize kwamba hayo majibu ni ya swali gani na swali gani,,,,!?*@$ hiyo sio Sawa wakati nawe una mtihani huo huo.

Chukua kama mtu kakutajia kuwa viazi lishe ni dili alafu nenda kafanye tafiti zaidi mwenyewe. Kwani hata angeweka kila kitu bado si sahihi kutofanya tafiti zako kujiridhisha.
 
Hahahaaaa umepiga siasa mkuu. Wewe unataka kufanya biashara Kwahiyo Unakuwa hututendei haki Kama hautoweka evidence ya kwamba hili zao linalipa kweli.

Tutajie japo hata kiwanda basi kimoja ambacho kinanunua hivyo viazi Au ukishindwa kabisa basi weka hata bei ya kununulia Za hivyo viazi Kwenye masoko makubwa kadhaa Kwa msimu uliopita. Isije kuonekana Kama vile unavutia biashara yako

kumekuwa Na kasumba ya watu kusema zao Fulani linalipa halafu hakuna taarifa Za kutosha kuhusu hilo soko. Wewe Kama umeamua kutushirikisha Neema Na umefanya research ya kutosha kuhusu soko tuwekee tu Hapa kila kitu sio tena mpaka Mimi nikafanye utafiti tena
 
Mkuu naona tuna mitazamo tofauti, binafsi nitalifanyia utafiti kivyangu alafu nitaamua,yaani wewe unataka ulishwe kabisa Duhhh.

Kwa mfano nikikutajia mkoa wa mbeya ardhi yake ina rutuba wakulima nendeni mkajilimie, kwa mtazamo wako nisipokutajia wilaya, kata, kijiji na aina ya zao ntakuwa sijakusaidia!!?? $@
 
Mkuu mfano wako sio hai, Hapa tunaongelea masoko. Kama yeye kafanya utafiti Kwanini asiweke taarifa Za kina kuhusu soko? Huko sio kutafuniwa bali Ni kumfanya yeye Asiwe mchoyo lakini pia kuvutia zaidi Hiyo biashara Yake.

Nikutakie utafiti mwema japo nahofu sijui utaanzia wapi
 
Uzi mzuri... ila post #24 hapo juu imeibua maswali kadhaa yanayohitaji majibu
 
Viazi lishe ni aina ya viazi vitamu vyenye mwonekano wa rangi ya njano kwa ndani vikimenywa. Viazi lishe ni biashara mpya katika kilimo biashara ambacho hakijamulikwa vyema na wakulima wetu. Hii ni fursa muhimu na ya kipekee kwa wakulima wanaolenga utajiri kutokana na kilimo. Kwa kifupi huku kuna pesa kuliko kawaida. Ni muhimu tukaichangamkia fursa hii. Kilimo cha viazi lishe ni kama ilivyo kwa viazi vingine vitamu ni rahisi sana ukilinganisha na aina nyingine ya kilimo.

Viazi lishe hutumia muda wa miezi mitatu toka kupandwa hadi kuvunwa. Na kama vikilimwa kwa ajili ya mbegu, vyazi hivyo hutumia miezi miwili tu na vinakuwa tayari kuvunwa na kupelekwa shambani.

Viazi lishe vina beta karotini ambayo ni chanzo muhimu cha vitamini A. Viazi lishe vinatengeneza bidhaa mbalimbali zikiwemo Chipsi, Kripsi pamoja na Unga ambao hutumika kutengenezea bidhaa mbalimbali kama vile Mikate, Keki, Maandazi, chapati, Biskuti na vitafunwa vinginevyo. Kwa kifupi, kwa kutumia viazi lishe, tunaweza kutengeza bedhaa zote ambazo unga wa ngano unatengeneza. Majani ya viazi lishe hutumika kama mboga.

Ekari moja huitaji mbegu elfu 12 na kila mbegu moja tunaiuza kwa tsh 60/= kwa mteja anayechukua mbegu kuanzia elfu 12 na kuendelea lakini chini ya hapo mbegu moja inauzwa kwa tsh 100/=. Tunatoa huduma ya kukusafirisha hadi ulipo kwa kukupostia mzigo kwenye gari na huduma yetu ni bora sana .

Katika ekari moja una uwezo wa kuvuna tani 19 hadi 24 kutegemeana na matunzo yako. Kwa kawaida mbegu moja ya viazi lishe iliyopandwa inatoa kilo 2 za viazi. Kadiri unavyoweka matuta makubwa ndivyo unatakavyovuna viazi vikubwa zaidi. Upandaji wa viazi lishe kati ya shina moja na jingine ni futi moja moja na kati ya tuta moja na tuta jingine pia ni futi moja.

Viazi lishe ni vitamu sana. Vina unga wa kutosha na mwonekano wake huwavutia wateja wengi sokoni ukilininganisha na viazi vitamu vya kawaidi. Lakini vilevile viazi hivi vimepewa chapuo kubwa na wenzetu wataalam wa lishe kwa ajili kuboresha afya ya watoto, akina mama wajawazito pamoja na wazee.

Kilo moja ya viazi lishe inakwenda kwa tsh 1000/= sokoni. Na shina moja linatoa wastani wa kilo mbili na ekari moja ina mashina 12,000. Kwa haraka haraka ekari moja ikiwa utafuata na kuzingatia masharti yote muhimu utaweza kuvuna tani hadi 24. Sasa wewe rudisha nyuma hiyo hesabu, fanya utavuna tani 20 tu ambayo ni sawa na kilogramu 20,000. Je wajua kwa hiyo ekari moja utaweza kutengeneza tsh ngapi? Hapa utachukua 1000/= X 20,000KGS itakuwa sawasawa na tsh. 20 milioni. Hebu niambie kuna biashara gani unaweza kufanya kwa miezi michache tu ukaibuka na kiwango hicho cha pesa. Fursa ni nyingi mtaani tuzichangamkieni.

Hapo hatujaongealea biashara ya mbegu za viazi hivyo. Navyo ni hela pia. Ukiamua kuzalisha mbegu za viazi lishe kama nilivyosema hapo awali vyenyewe huchukua miezi miwili tu hadi kuvunwa. Katika ekari moja inatoa mbegu laki moja 1,046,000 na kila mbegu kwa mkulima shambani inanunuliwa kwa tsh 30/= na sokoni kwa wale wateja wakubwa kabisa wanaochukua kuanzia mbegu 360,000 zinauzwa kwa tsh 50/=. Sasa ukichukua mbegu 1,046,000 x 30/= mkulima ataweza kupata jumla ya tsh 31,380,000/= . Je kuna biashara yeyote unayoweza kufananisha na kilimo hiki cha uzalishaji wa mbegu na viazi vyake?

Ni muhimu kukumbuka viazi ni miongoni mwa mazao yanayostahimili sana ukame hivyo vinamuhakikishia mkulima chakula cha uhakika. Vilevile kilimo hiki cha viazi lishe, hakina usumbufu kama ilivyo kwa aina nyingine ya kilimo. Ukipitisha trakta likavuruga ardhi, ukapanda mbegu kitakachofuata ni palizi tu. Kwa baadhi ya maeneo huhitaji mbolea lakini kuna baadhi ya maeneo mengine kama vile Morogoro hayahitaji hata mbolea, ukivichomeka tu basi utasubiri palizi kisha kuvuna.

Viazi lishe hustawi katika maeneo mengi ya nchi yetu lakini hustawi zaidi katika maeneo ya joto kwa mfano maeneo yote ya mikoa ya Pwani na Morogoro, maeneo yote ya Kanda ya ziwa na mikoa ya magharibi kama vile Tabora na Kigoma, Mikoa ya Kanda ya kati Singida na Dodoma pamoja na mikoa ya nyanda za juu kusini hasa Ruvuma, Rukwa na Katavi. Kwahiyo wakulima waliyo kwenye maeneo hayo wana fursa zaidi ya kuendesha kilimo hiki cha viazi lishe pamoja na mbegu zake.

Hii ndiyo fursa niliyoona niwashirikishe siku ya leo.
Kwa mahitaji yako ya Viazi lishe au Mbegu zake tafadhali wasiliana nami

Aman Ng'oma
Mkurugenzi Mtendaji
Kinasoru East Africa Tanzania Ltd
0767989713/0786989713
amanngoma@gmail.com
Dodoma.
View attachment 486804 View attachment 486805 View attachment 486806 View attachment 486807 View attachment 486810 View attachment 486811

Mbegu moja ya kiazi ina urefu gani (yaani hilo jani)
 
Shukrani kwa elimu na fursa nzuri
 
nimepanda hizi mbegu nasikilizia kama hisabati zako ni sahihi baada ya kuvuna
 
Soko la hivyo viazi ni wapi?!! Hakuna soko la uhakika, hakuna muamko waw watu kusisitiza kiazi lishe anapokwenda sokoni, utalima kiazi lishe lakini utauza kama kiazi cha kawaida!
 
Soko la hivyo viazi ni wapi?!! Hakuna soko la uhakika, hakuna muamko waw watu kusisitiza kiazi lishe anapokwenda sokoni, utalima kiazi lishe lakini utauza kama kiazi cha kawaida!
Sisi tunalo Soko la uhajika
 
watu wanasoma kwenye vitabu Wanakuja kunukuu huku tunataka mtu Aeleze kile alicho kifanya na kupata mafanikio sio kuleta stori
 
Back
Top Bottom