FURSA KUTOKA HELPING HANDS INTERNATIONAL

FURSA KUTOKA HELPING HANDS INTERNATIONAL

chuma jr

Member
Joined
Oct 17, 2015
Posts
88
Reaction score
135
H2i NI NINI??

H2i (Helping Hands Interntional) ni Taasisi isiyo ya Kiserikali yenye dhumuni kuu la kuweka tabasam kwenye nyuso za watu wasiojiweza na wale ambao ni wanachama.

⚡Haiuzi wala kununua bidhaa yoyote.
⚡Ina husika na kutoa huduma tu.
⚡ Ni ya kuamimika na yenye uhakika

Inahitaji mchango/kiingilio cha elfu 90 ambacho kinalipwa mara moja tu.

INAFANYAJE KAZI??
Ni mpango wa kushirikisha watu.
Kuna zawadi kwa kila Hatua.
Ziko Hatua (stages) 5 zianazokupa zawadi.
Unahitaji kushirikisha watu wawili tu nao watashirikisha wengine wawili,kila mtu atashirikisha watu wawili tu na unalipwa kila unaposajili mtu chini yako muda huohuo.

FAIDA ZAKE
1. Hatua ya kwanza
Utalipwa $ 26=57,200/=

2. Hatua ya Pili
Utalipwa $ 1,000 = 2,200,000/=
Apple iPad au hp laptop mpya.
Laini ya simu CUG
kwa.ajili y kuwasiliana na wanachama wa h2i bure.

3. Hatua ya Tatu
talipwa $ 3,000 = 6,600,000/=
Gari mpya Hyundai elantra yenye thamani ya $ 22,000.
Kupendekeza watu 2 wasio jiweza kutoka eneo lako ambao sio wanachama ambao watasaidiwa $ 1,000 kila mmoja sawa na.tsh 4,400,000/=
✈ Safari za nje ya nchi ambazo zimelipiwa gharama zote na h2i.

4. Hatua ya Nne
Utalipwa $ 6,000 = 13,200,000/=
Gari mpya ya kifahari hyundai ix35 Jeep yenye thamani ya $ 27,000.
‍‍‍ Kupendekeza kituo kimoja cha watu wasiojiweza ili kisaidiwe na h2i.

5. Hatua ya Tano
Utalipwa $ 12,000 = 26,400,000/=
Kudhaminiwa gharama za ujenzi wa nyumba $ 40,000
Kulipiwa gharama za.masomo kwa watoto wako = $ 2,000.

Nakushauri uielewe vyema fursa hii kisha ujiunge kwa ajili ya manufaa yako na jamii inayokuzunguka.

Vision

Poverty is an insult to humanity. Financial empowerment eventually becomes the desire of every living soul. This is why we are here to bring your desires to live. It is our vision and no obstacle will deny you of your happiness.
Je ungependa kujiunga nasi?
Contact:
Call/Whatsapp +255621039453
Email;chumazerubabel13@gmail.com
 

Attachments

Shughuli IMEANZA, haya tens MAPUNGAZEZETA saa ya KULIWA NI SASA, hivi ni kweli mtaingia katika ujinga huu halafu muanze kulalamika TUMETAPELIWA? WEKENI AKILI ZENU SAWA ,HUU NI UTAPELI !!
 
Niling'atwa na DECI na sitakubali kuwa mburula tena, jameni Waafrika tufanye kazi na kula kwa jasho letu, haya mambo ya kupiga watu hela zao yataishia kuwa laana tu.
 
Wao wanatoa wapi hizo hela za kunilipa? Na kama wana hela kwa nini waweke kiingilio?
 
Kaka chuma jr kwanini unataka kuwa wakala wa shetani, mlaghai, mwizi ,na muongo?. Hv unaelimu kweli hata ya darasa la saba?. Yaani mtu anajiunga na elfu 90 kisha analipwa mamilioni ya pesa, sawa sikatai ila ungeweka mchanganuo wa hiyo elfu 90 yako itatumia mechanism gani ku generate hayo mamilioni. Ni biashara gani itafanyika kuleta faida itakayokupelekea kulipwa kwa stage hizo?. Vijana msipende utajiri kirahisi lakini pia utapeli wa aina hii mbona ni wa kijinga sana, jifunzeni mbinu za kutapeli zenye kufikirisha na iliyongumu kugundulika kirahisi. Haya unasema utalipwa kwa stage bila kuweka duration ya stage moja na nyingine. Inawezekana stage hiyo ya kwanza ni kuanzia miaka 5 baada ya kujiunga na ya pili ni ni miaka 20. Hebu njoo na mchanganua wa jinsi hizi hela zitakavyozaa na lini unaanza kulipwa toka uweke (stage 1) na gape baina ya stages.
UTAPELI UNAHIAJI WETU WENYE UJUZI NA AKILI SIYO WAJINGAWAJINGA.
 
Kwa hiyo kuna sehemu wenzetu mnapata ruzuku ya bure,mmeamua kuigawa? Kweli MNA MOYO MWEMA ! MUNGU AWABARIKI
 
Shughuli IMEANZA, haya tens MAPUNGAZEZETA saa ya KULIWA NI SASA, hivi ni kweli mtaingia katika ujinga huu halafu muanze kulalamika TUMETAPELIWA? WEKENI AKILI ZENU SAWA ,HUU NI UTAPELI !!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] hiyo inaitwa akili kumkichwa..... Cheza mwenzako anenepe.... Bora ukajihusishe na kilimo tuuu na so kusubiria hela za kizembe zembe namna hii
 
Back
Top Bottom