Fursa kwa kila mtanzania kuonja utamu wa keki ya taifa letu kwa kusafiri na treni ya SGR kwa safari zake za kikazi, kitalii au kibiashara

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Ni usafiri tulivu, salama na wa uhakika sana, muonekano wa mandhari nzuri sana za misitu, milima na mabonde njiani ni burudani tosha, ukiachilia mbali huduma murua ndani ya treni, mazingira bora na ya kisasa sana ndani ya treni yenyewe.

Tanzania imelamba dume kwa kukamilika na kuanza kazi kwa mradi huu muhimu sana wa kimkakati kiuchumi, katika sekta ya usafiri na usafirishaji.

Haya ni sehemu kidogo tu ya matokeo na mafanikio ya kodi, tozo na ushuru tunao kusanya kwa pamoja kama Taifa. Treni ya SGR ni keki ya Taifa, tuitimie na kuifurahia kwa kuitunza kwa kishirikina sote kama Taifa

Furahia keki hii ya taifa kwa kutumia usafiri wa kasi wa Treni ya SGR kwa safari za uhakika kwa muda na wakati sahihi

Well done serikali sikivu ya CCM, chini ya kiongozi madhubuti, comrade Dr. Samia Suluhu Hassan, Raisi wa JMT kwa kukamilisha jambo hili la maana sana na la kimkakati kwenye uchumi wetu πŸ‘ŠπŸ’ͺ
 
Kwani ni ya bure.
 
Tuache tabia ya kuhusianisha mafanikio ya serikali na mtu binafsi, kama ni suala binafsi basi hongera ziende kwa Magufuli.

Vv
 
Ingekuwa bure tungesema ni keki ya Taifa, keki gani ya Taifa hutakiwi kuila ukiwa na shangazi kaja ? Hii keki si keki tena naona ni andazi lilidondoka kwenye mchanga alafu unapewa ule.
 
Tla tlah alikuwa haongelei kabisa mada za kuisifia serikali... sijui nani kamlambisha asali kwa kumpa majukum ya kuisifia serikali mtandaoni na kumpa mkwanja mrefu... Na kuandika thread 3 kwa wiki kuisifia serikali naweza wakuu ripening shavu
 
Sioonashabgazikajaaa
 
Tunaomba bei mkuu ya nauli toka dar to morogoro
gentleman,
mbona bei ziko wazi tu na huduma inaendelea kila siku?

mie nasisitiza tu kwa kila mlipa kodi, keki hii isikupite, ni fursa ya kuitumia kurahisisha safari zako, na ni matokeo ya kodi na tozo ulizotozwa kuchangia ujenzi wake πŸ’

sasa kwanini usienjoy bana, ila siyo Lazima mabasi pia yapo..
 
Kwani ni ya bure.
utaratibu wa kuinjoy keki ya Taifa tunachangia kujenga, lakini pia tunachangia kidogo kuvitunza vidumu zaid. ni utaratibu wa kawaida kwa mali za umma πŸ’
 
Sioonashabgazikajaaa
we uje na shangazi kaja yako, utasafiri kwa treni ya SGR bila tatizo lolote, usibabaike sana na habari za mitandaoni πŸ’
 
Nabeba shangazi kaja ole wao wanikataze
usibabaike, kuutishwa wala kupotoshwa na taarifa za mitandaoni. si tu shangazi kaja, njoo hadi na mfuko wa salfeti utasafiri bila wasiwas wowote na SGR πŸ’
 
Na hapo hapo nisipande na shangazi kaja.
epuka taarifa za mitandaoni,
njoo na mzigo wowote utasafiri kwa treni ya SGR vizuri kwa salama na amani πŸ’
 
Tla tlah alikuwa haongelei kabisa mada za kuisifia serikali... sijui nani kamlambisha asali kwa kumpa majukum ya kuisifia serikali mtandaoni na kumpa mkwanja mrefu... Na kuandika thread 3 kwa wiki kuisifia serikali naweza wakuu ripening shavu
gentleman?
mimi nasifia serikali? tangu lini...

kusema ukweli ndio kusifia serikali sio?πŸ’
 
Tla tlah alikuwa haongelei kabisa mada za kuisifia serikali... sijui nani kamlambisha asali kwa kumpa majukum ya kuisifia serikali mtandaoni na kumpa mkwanja mrefu... Na kuandika thread 3 kwa wiki kuisifia serikali naweza wakuu ripening shavu
Alikuwa anasoma upepo wa members atoke vipi?
 
Ingekuwa bure tungesema ni keki ya Taifa, keki gani ya Taifa hutakiwi kuila ukiwa na shangazi kaja ? Hii keki si keki tena naona ni andazi lilidondoka kwenye mchanga alafu unapewa ule.
usizingatie sana mambo ya mitandaoni gentleman πŸ’

seti za behewa zenyewe zilikuja zikiwa ndani ya shangazi kaja, hayupo wa kuzuia wew usisafiri na shangazi kaja yako uliyoijaza nguo zako za maana za safari πŸ’

so we njoo tu huwezi kataliwa kuingia kwa treni na shangazi kaja yako...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…