Fursa kwa kila mtanzania kuonja utamu wa keki ya taifa letu kwa kusafiri na treni ya SGR kwa safari zake za kikazi, kitalii au kibiashara

Fursa kwa kila mtanzania kuonja utamu wa keki ya taifa letu kwa kusafiri na treni ya SGR kwa safari zake za kikazi, kitalii au kibiashara

Ni usafiri tulivu, salama na wa uhakika sana, muonekano wa mandhari nzuri sana za misitu, milima na mabonde njiani ni burudani tosha, ukiachilia mbali huduma murua ndani ya treni, mazingira bora na ya kisasa sana ndani ya treni yenyewe.

Tanzania imelamba dume kwa kukamilika na kuanza kazi kwa mradi huu muhimu sana wa kimkakati kiuchumi, katika sekta ya usafiri na usafirishaji.

Haya ni sehemu kidogo tu ya matokeo na mafanikio ya kodi, tozo na ushuru tunao kusanya kwa pamoja kama Taifa. Treni ya SGR ni keki ya Taifa, tuitimie na kuifurahia kwa kuitunza kwa kishirikina sote kama Taifa

Furahia keki hii ya taifa kwa kutumia usafiri wa kasi wa Treni ya SGR kwa safari za uhakika kwa muda na wakati sahihi

Well done serikali sikivu ya CCM, chini ya kiongozi madhubuti, comrade Dr. Samia Suluhu Hassan, Raisi wa JMT kwa kukamilisha jambo hili la maana sana na la kimkakati kwenye uchumi wetu 👊💪
Hii ni nzuri. Nakubaliana na mradi huu ingawa changamoto ni kukwama kwa Lots zingine na kusababisha wafanyakazi kurudishwa majumbani kwao kwa muda usiojulikana.
 
Inatakiwe kuwe na chumba cha mizigo
kuna wabia kama vile gsm, Mo, Bakhresa, jambo na wengineo wanaleta treni za kisasa, kutakua na uchaguzi wa ubora wa huduma abiria anayotaka. Itakua kama magufuli terminal tu 🐒
 
Hii ni nzuri. Nakubaliana na mradi huu ingawa changamoto ni kukwama kwa Lots zingine na kusababisha wafanyakazi kurudishwa majumbani kwao kwa muda usiojulikana.
I hope kuna majadiliano na mikakati inafanyika, watarudi kazini tu🐒
 
Hongera wafanyakazi wote wa serikali waliofanikisha mradi huu muhimu.
Wapambane kumaliza maeneo yaliyobakia ili watanzania wengi wafurahie jasho la kodi zao
 
Hapo ashukuriwe Magufuli (RIP) tu!
Mama asifiwe kwa mikopo.
Tunakushukuru Mungu kwaajili ya maisha viongozi wetu hawa wapendwa...

hayati Baba wa Taifa, J.K.Nyerere kwa uhuru wa nchi, Ali Hassan Mwinyi Mzee wa Rukhsa, Benjamin Mkapa Mzee wa ukweli na Uwazi na JPM hapa kazi tu 🐒

wamefanya kaz kubwa na nzuri sana iloyo tukuka kwaajili ya watanzania...
 
Bila kumtaja Mwendazake kwenye hili haya yote yatakosa baraka kwa Mwenyezi Mungu
Tunamshukuru Mungu sana kwa maisha ya Dr.JPM hapa duniani, na kuanzinzisha ujenzi wa mradi huu wa kimkakati wa SGR,

Tunasema asanti kwa Mungu kwa Dr.SSH kukamilisha vizuri mradi huu muhimu.
Tunamshukuru Mungu kwa yote...

CCM iliahidi kwa maneno na imetekeleza kwa vitendo 🐒
 
Keki ya Taifa..?? Au Mimi ndio sielewi maana ya neno keki ya Taifa..??
sina hakika kama kweli huelewi ila huenda ufahamu wa kutosha juu ya mambo haya ndiyo changamoto.....

huduma na bidhaa zote za umma zilizojengwa au zinazotokana na kodi, tozo na ushuru tunao changia mimi, wewe, wananchi na waTanzania wote ni keki ya taifa...

hii ni pamoja na mabarabara, reli, huduma za maji safi na salama, elimu, afya ulinzi na usalama n.k🐒
 
Back
Top Bottom