Fursa mpya zinaonekana katika ushirikiano wa kuvuka mpaka wa BRI wakati mkutano wa FOCAC ukikaribia

Fursa mpya zinaonekana katika ushirikiano wa kuvuka mpaka wa BRI wakati mkutano wa FOCAC ukikaribia

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1724308582581.png
Ushirikiano kati ya China na Afrika, ambao masuala ya uchumi na biashara ndio kiini chake, utaendelea kuwa wa kina zaidi chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) la China, wakati pande hizo mbili zikiwa tayari kukumbatia mtazamo wa pamoja wa kujenga jamii ya ngazi ya juu ya China na Afrika yenye hatma ya pamoja.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la China Xinhua, mtazamo umepewa kipaumbele katika Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utakaofanyika hapa Beijing kuanzia Septemba 4 hadi 6. Viongozi wa nchi wanachama wa FOCAC kutoka Afrika watahudhuria mkutano huo pamoja na wawakilishi kutoka mashirika ya kikanda na ya kimataifa. Mkutano huo wenye kaulimbiu ya “Kuungana kwa mikono Kuendeleza mambo ya kisasa na Kujenga Jumuiya ya Juu ya China na Afrika yenye Mustakabali wa Pamoja,” utakuwa ni tukio la kusherehekea urafiki kati ya China na Afrika, kutafiti ushirikiano na kutafuta mwelekeo wa siku za baadaye.

Profesa Song Wei kutoka Shule ya Uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia katika Chuo Kikuu cha Masomo ya Kigeni anasema, uhusiano kati ya China na Afrika umejengwa kwa msingi wa kuheshimiana na kunufaishana, huku lengo likiwa ni jinsi ya kuleta maendeleo endelevu ya nchi za bara la Afrika. Katika muongo mmoja uliopita, mafanikio makubwa yametimizwa, huku mambo mengi ‘ya kwanza’ yakionekana chini ya ujenzi wa pamoja wa Ukanda Mmoja, Njia Moja. Zaidi ya hayo, uungaji mkono wa China kwa nchi za Afrika hauna masharti yoyote ya ziada, jambo ambalo ni tofauti kabisa na nchi za Magharibi zinazoongozwa na Marekani.

Katika miaka iliyopita, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika umedumisha uhai na kupata matokeo makubwa. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na serikali ya China mwishoni mwa mwaka 2023, chini ya uongozi wa ujenzi wa pamoja wa BRI, miradi kasha mikubwa ya usafiri, nishati na sekta mpya za miundombinu Barani Afrika imetekelezwa.

Pia, kufikia mwishoni mwa mwaka 2022, biashara ya pande mbili kati ya China na Afrika ilichukua zaidi ya asilimia 20 ya biashara ya nje ya jumla barani Afrika, na uwekezaji wa China barani Afrika ulizidi dola za kimarekani bilioni 40. Juhudi hizi za pamoja sio tu zimeboresha maendeleo ya uchumi wa maeneo hayo, bali pia zimepata matokeo makubwa katika kupunguza umasikini barani Afrika.

China imedumu kuwa mshirika mkubwa wa biashara wa Afrika kwa miaka 15 mfululizo, huku nchi 52 za Afrika zikisaini makubaliano ya ushirikiano katika ujenzi wa pamoja wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, ambalo wataalam wanasema linaakisi utambuzi wa nchi za Afrika kwa kile ambacho Pendekezo hilo linaleta kwa uchumi na jamii ya nchi hizo.

Uungaji mkono wa China kwa nchi za Afrika sio wa kipekee. Profesa Song anasema, tofauti kubwa kati ya BRI na mtazamo wa nchi za Magharibi kwa Afrika ni kwamba, ushirikiano wa China na Afrika unajengwa kwa msingi wa usawa, kunufaishana, na kunufaika kwa pamoja, na kwamba ushirikiano huo ni wa kuungana mkono kati ya nchi zinazoendelea, na hivyo kuwa na manufaa kwa pande zote mbili.

Anasema ushirikiano huu sio wa kipekee, ikimaanisha kuwa, China daima iko tayari kuwa na ushirikiano wa pande tatu na nchi nyingine zote, kampuni za kimataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yako tayari kuunga mkono maendeleo ya Afrika.

Mkutano wa Kilele wa FOCAC utakaofanyika mwezi ujao utaangalia zaidi mahitaji ya maendeleo barani Afrika, na unalenga kupata muafaka wa masuala ya kimsingi ya dunia yanayofuatiliwa kwa pamoja na pande hizo mbili. Nchi za Afrika zinapaswa kutumia fursa ya mkutano huo kuingia katika soko kubwa la China kwa kuongeza biashara, hatua ambayo pia itasaidia kutoa fursa za ajira na ustawi kwa watu wa pande hizo.
 
Back
Top Bottom