FURSA nchini COMORO: Mfanya biashara, soma hapa

Ni

Ni hatari hebu tudadavulie hapo? Nna jamaa yangu kaenda Comoro kuuza dawa za nguvu za kiume anasema kuna wateja sana coz wacomoro wanaoa wanawake wengi..Toka aondoke 2014 sijasikia tena kutoka kwake labda na yeye ametekwa na mwanamke wa kingazija
uongo wakomoro hawaoi wake wengi tatizo zinaa ni nyingi
 
comores ni sehemu nzuri ya biashara ila uwe tu muangalifu
hata uwe na mamillion ya hela utatembea wakati unaotaka hakuna uhalifu
usumbufu uliopo ni utoaji wa mzigo bandarini proses ni nyingi ila kuna watu wanaweza kukusaidia
 
Tatizo la comores
Restaurent (migahawa) hutopata vyakula kama vile Tanzania kariakoo
Vyakula vingi ni vitu vikavu muhogo wa kuchoma, ndizi za kukaanga, mashelisheli ya kukaanga na kuchoma. Mapapatiko ya kuku, mishikaki . nyama wenyewe inatoka brazil ishakaa mda sana kwenye friza
Ila kuna restaurent moja moroni inaitwa nassib hapo ndio utapata chips kuku pilau vinywaji bei juu
 
Kama ni mlaji wa pweza utafaidi maana wao hawali pweza ila utajipikia mwenyeo
Wanapenda sana mziki mchukue kiba au blue au mbosso au chibu au mr Nice utapiga hela sana [emoji38][emoji38][emoji38]
 
Fursa nzuri sana kwa wafanya biashara.....Ingekua na muendeleza katika nchi zenye fursa zaidi nakubwa kuliko comoro yenye idadi ndogo ya watu uchumi mdogo tuekeeni bussiness trip nchi kama Sweden UAE nk
Umeona kwa jicho la mbali sana mkuu.
Comoro ni sawa na Unguja tu.
 
tahadhari kwa mwenye kwenda kufanya biashara comores
usije onja penzi la kingazija utapoteza mali yote hurudi na kitu tushawachangia watu nauli ya kurudi
Kwa hyo mkuu unamaanisha wanawake wa Ngazija ni watundu Kama wale wa Tanga?
 
tahadhari kwa mwenye kwenda kufanya biashara comores
usije onja penzi la kingazija utapoteza mali yote hurudi na kitu tushawachangia watu nauli ya kurudi
Hivi Mkuu Moroni kuna Ambiance Club Corner Bar yao kule? Yaan sehemu naweza kiburudishaji nikaburudika nae.
Siku moja nilizunguka mji mzima nikitafuta "Za kununua" nikakosa kabisa.
 
Zipo kama club des amis kule zilmadjou na
Rose noir disco teque wee hujaonana na wenyeji tatizo
Hivi Mkuu Moroni kuna Ambiance Club Corner Bar yao kule? Yaan sehemu naweza kiburudishaji nikaburudika nae.
Siku moja nilizunguka mji mzima nikitafuta "Za kununua" nikakosa kabisa.
 
Hv km nataka kwenda kwa ajili ya research(kwa ndege)ni mzigo gani wa biashara unaweza kua ni light alafu una soko pia ili nisi umie ktk hili swala nauli na malazi
 
Kabla hujaenda ulizia meli inaondoka mda gani dar to comores pakia mzigo mdogo ktk meli kabla siku 2 kuondoka kwa meli
Kata tiket ya ndege ondoka kabla meli kufika comores ukaisubiri meli kule ikifika tu uwepo ili utoe mzigo wako ukijisahau mzigo wako utaibiwa huko huko bandarini au . Kwa safar ya mwanzo ningekushauri upande meli hasara itapungua kuliko kuchukua ndege
 
Meli itakuchukua siku 3 kufika moroni
Ndege masaa 2 tu nauli ni 320euro + 60 euro ya visa na tax to capital city moroni itakubidi uchukue taxi ya peke yako kwa vile huna mwenyeji ni euro 10 taxi ya kushare ni euro 1 from airport to moroni capital city. Hotel euro 20 par day hizo gharama ni kubwa sana kwa mfanya biashara mdogo ila kwa mwenye kwenda kuresearch poa ushauri wasiliana na watanzania waliopo comores ili wakupokee.
 


Mkuu,asilimia ngapi ya waislamu nchini comoro?
 
Wakomoro wote ni waislam kanisa lipo moja lilijengwa na wakoloni wafaransa wanaoabudia ni wageni tu mkubwa wa kanisa la comores ni raia wa Tanzania ambaye ni dokta wa hospital ya msaada wa kanisa anaitwa dr philipo raia wa tz huyo comores ni waislam ila tu wana mila na tamaduni zao na uzungu wameufanya mwingi.
 
Comoro-mayotte-madagascar-reunion island by kwasakwasa.
 
Nakufuta mkuu, inbox me thy number
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…