Fursa nyingine Bagamoyo/Chalinze/Mzenga

Fursa nyingine Bagamoyo/Chalinze/Mzenga

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Posts
5,329
Reaction score
5,024
Kuna fursa nyingine haijavamiwa sana na wenye mitaji mikubwa. Sasa hivi umeme unasambazwa kwa kasi kubwa ktk maeneo mengi ya wilaya ya Bagamoyo na Kisarawe. Kule kuna wafugaji wengi wa ng`ombe na wana maziwa ambayo kwa sababu ya kukosa matunzo yanaishia kuharibika.

Pale Lugoba/Msoga/Msata na Ubena kuna vituo vya kukusanyia maziwa kutoka kwa wafugaji na kuyahifadhi tayari kwa kusafirisha Dar kwa walaji. Mahitaji ya huu mradi ni chumba chenye umeme, kipima maziwa ili kulinda ubora, packaging materials na uwezo wa kuwalinda wateja wako wanaokuletea maziwa na wanaonunua kwako.

Sasa maeneo kama Mzenga/migindu na Gwata hakuna vituo hivi, sababu umeme ulikuwa haujafika, sasa hivi umeme unapelekwa huko. Kwa wenye mitaji wachangamkie fursa hii. Ukipita asubuhi mitaa ya Lugoba utaona wamasai wakipeleka maziwa yao sokoni kwa wingi.
 
Vipi kilimo cha majani ya mifugo?!?

Hii biashara ni nzuri sana mkuu kama unapata shamba na ukaweka kibanda barabarani ambapo wakulima wanaweza kukufikia kirahisi. Pale Temboni kuna jamaa anauza majani makavu, au ukienda Kibaha pia wanauza.
 
Back
Top Bottom