SoC01 Fursa tunazokosa sababu ya ukosefu wa Elimu ya msingi ya Matumizi ya Kompyuta(Computer)

SoC01 Fursa tunazokosa sababu ya ukosefu wa Elimu ya msingi ya Matumizi ya Kompyuta(Computer)

Stories of Change - 2021 Competition

kipenseli2021

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2021
Posts
1,390
Reaction score
1,431
KOMPYUTA NI NINI?

Kompyuta ni kifaa cha kielectroniki kinacho pokea Data ,kuzi hifadhi ,kuzichakata na kutupa majibu au taarifa,

MFUMO WA KOMPYUTA NINI?

Mfumo wa kompyuta ni muunganiko wa vifaa vya kompyuta,programu za kompyuta,data na mtumiaji ambazo kwa pamoja zinaweza kupokea data,kuhifadhi data,kuchakata data na kutupa majibu

Mfumo wa kompyuta unaundwa na sehemu kuu mbili ni Vifaa vya Kompyuta “Hardware” na programu za Kompyuta “Software” mfano wa vifaa vya kompyuta ni Monita,Spika,Kibodi,Mouse,Projekta na vifaa vingine vya ndani ya kompyuta ukifungua kasha kama Ram,Hard disk drive,Mother board,CPU ,pia mfano wa programu za kompyuta ni Microsoft office word,Microsoft excel,Ms access,VLC,Virtual Dj,Games,Adobe page maker,Adobe photoshop ,Recuva,Disk drill na programu nyingine

MATUMIZI YA MSINGI YA KOMPYUTA NI NI NI ?

Matumizi ya msingi ya kompyuta ni matumizi ya kompyuta kwa watu wa kawaida wa Nyanja tofauti kulingana na shughuli wanazo zifanya ambazo zinahitaji ujuzi wa kawaida wa kompyuta ili kuwasaidia kazi zao za kila siku kama kufanya mahesabu,kuandika nyaraka,kuchambua data,kusanifu michoro,kuandaa kadi za mwaliko na vipeperushi,kutumia na kupokea barua pepe,kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao na kuuza bidhaa au huduma,kujisajiri na kutafuta ajira,kufanya mikutano kwa njia ya mtandao zoom

Na matumizi yote ambayo ayahitaji ujuzi mkubwa wa kutumia kompyuta

UKUBWA WA TATIZO LA UKOSEFU WA ELIMU YA MSINGI YA KOMPYUTA

SIMULIZI:
Siku moja kuna kijana mmoja alitoka katika kijiji cha mbali zaidi ya umbali wa kilo mita 70,akiwa na pikipiki(Gharama ya mafuta) anatafuta huduma ya kompyuta,alipofika nikamuuliza una shida gani akaniambia nime downloada file/pakua file kwenye simu yangu lakini nimelitafuta sijui lipo kwenye folder gani nikamuangalia na kumuona alivyo choka na umbali mrefu alio toka basi nikachukua simu yake nikafungua Browser(Mozilla fire fox) nikaenda kwenye sehemu ya Download nika kliki na kumuonesha faili lake nilitumia chini ya Dakika 2,baada ya kumuonesha akaniomba niliamishe na kumuwekea kwenye USB FLASH yake nikafanya ivyo ,akaniuliza bei gani nikamwambia hapana ni bure sioni kazi niliyo ifanya lakini akanishika mkono na kunipa elfu kumi kwa hiyo unakuta mtu anatumia zaidi ya elfu ishirini kwa kazi ndogo kama hiyo “

JE KWANINI NI MUHIMU KWA WATANZANIA WENGI KUJUA MATUMIZI YA MSINGI YA KOMPYUTA

Kuna faida kubwa sana kwa kila mtanzania kujua matumizi ya kawaida ya kompyuta/matumizi ya msingi ya kompyuta kwa sababu zifuatazo

  • Kuongeza pato la Taifa kwa kushiriki katika biashara za Mtandaoni
  • Kurahisisha upatikanaji wa huduma za kiserikali mfano Usajiri wa kampuni (BRELA),Uhakiki wav yeti(RITA),loss report (Tanpol),Ajira porta(ww.ajiraporta.go.tza) na huduma nyingine za serikali mtandao
  • Kupunguza foleni katika kupata huduma kama Bank,BRELA,RITA na TRA ,watanzania wakijua kutumia kompyuta wenyewe wataweza kujihudumia wenye katika huduma kama TIN za TRA,kujiandikisha kwenye vyuo na bodi ya mikopo
  • Kuongeza uwazi na rushwa,ukosefu wa elimu ya msingi ya kompyuta inapelekea watu kushawishi na kutoa rushwa hili wapate huduma ambazo wangeweza kujifanyia wenyewe wakiwa nyumbani mfano kukata TIN na huduma nyingine
  • Kupanua soko la bidhaa na kufanya manunuzi,ingesaidia kuweza kuwa na uwanda mpana wa kuchagua bidhaa katika tovuti na kibiashara (E-commerce) hivyo upatikanaji wa bidhaa na soko la bidha ingekuwa rahisi zaidi
  • Ku save muda /kuokoa muda,watu wengi kutokana na ukosefu wa elimu ya msingi ya matumizi ya kompyuta wanapoteza muda kwa kutafuta huduma umbali mrefu na kwa gharama kubwa lakini wangejua kutumia kompyuta ingekuwa rahisi sana
  • Matumizi sahihi ya mtandao,tumeona tunavyo pata changamoto ya watu kutumia mtandao ovyo kwa matusi na mambo ambayo hayana msingi yote ni sababu ya ukosefu wa elimu ya msingi ya matumizi ya kompyuta na maadaili yake
  • Kujifunza kwa masafa marefu,idadi ya wanafunzi wanao chukua mafunzo kwa masafa marefu yangeongezeka sana
  • Kuongeza kipato na kufanya kazi kwa usanifu ,matumiz ya kompyuta yamekuwa makubwa sana kwenye sekta mbalimbali mfano Uhasibu,Uhalimu,Tabibu na kada mbalimbali
  • Kuongeza uelewa na upana wa kujisomea,watu wanashindwa kutafuta taarifa mbalimbali kwa ajili ya kujisomea na kuingiza teknolojia mpya katika nchi yetu

  • CHANGAMOTO ZA UTOAJI WA ELIMU YA KOMPYUTA MASHULENI (SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI)
  • Ukosefu wa walimu wa TEHAMA
  • Ukosefu wa maabara/chumba cha Kompyuta
  • Ukosefu wa vifaa/kompyuta
NASHAURI NINI KUHUSU ELIMU YA MSINGI YA MATUMIZI YA KOMPYUTA?

  • Kuajiri walimu waliosomea TEHAMA/ICT kwa wingi
  • Kuweka mkazo wa somo la kompyuta katika shule za msingi ,sekondari na chuo kwa kuwa na maabara za kompyuta zenye kompyuta angalau 50
  • Kujenga vitua vya kujifunzia watoto kompyuta wanapo kuwa likizo au muda wa ziada
  • Kushusha kodi katika kompyuta hili Watanzania wengi waweze kumudu kununua na kuwa nazo nyumbani
JE NI PROGRAMU GANI UNATAKIWA UWE NAZO KATIKA KOMPYUTA YAKO?

Kwa Mtanzania ambaye tayari anayo kompyuta yake nyumbani kwa ajili yake na familia basi anatakiwa awe na programu zifuatazo muhimu kwa matumizi ya kila siku

  • Package ya Microsoft office (Microsoft office word,Excel,Access,Outlook,Powe point,publisher)
  • Broswer –hizi ni programu kwa ajili ya kuingia kwenye mtandao mfano Mozilla fire fox,Google chrome na Opera mini,Safari
  • Desktop publishing software-programu za kuandaa material kama kadi,vitabu,vipeperushi,magazeti mfano Adobe page maker
  • Adobe reader and E-book reader/E pub kwa ajili ya kufungulia PDF file na E pub file
  • Antivirus/Anti ware-programu za kudhibiti virus (Malicios software) waziweze kuvamia kompyuta yako na kuharibu utaratibu wa ufanyaji kazi wa kompyuta yako na upotevu wa data
  • Data recovery –hizi ni programu za kurudisha data zilizo potea kwa bahati mbaya/kufutwa kwenye kompyuta yako mfano Disk drill,recuva,Wondershare Data recovery,I-care nk
  • Education and simulator software,hizi ni programu kwa ajili ya elimu na kujifunza vitu mfano Utengenezaji wa sakiti
  • IDM na Downloader manager/utorrent/bit torrent /Youtube video downloader kwa ajili ya kupakua vitu kwenye mtandao
JE VITU GANI VYA KUANGALIA NINAPO TAKA KUNUNUA KOMPYUTA MPYA?
  • Vitu vya kuangalia unapotaka kununua kompyuta mpya ni kama vifuatavyo
  • Saizi ya RAM(random access Memory) inaangaliwa kwa uniti kama Gigabyete(GB) angalau iweze kuanzia GIGABYTE MBILI na kuendelea
  • Saizi au Spidi ya Procesor (CPU) ina pimwa GHZ
  • Hard Disk Drive kwa ajili ya kuhifadhi Data kuanzia Giga byte 100 na kuendelea
  • Idadi ya PORT au Matundu ya kuchomekea vifaa mfano hakikisha ina matundu mengi ya USB,VGA,HDMI,DVI na Audi jack
  • Saizi ya Kasha (Portability) umbo la kasha ili lisichukue nafasi kubwa
  • Brand ,kuna brand nyingi mfano Dell,Toshiba epuka kununua Brand ambayo utapata shida kupata vifaa vyake pindi kitakapo haribika
  • Mlango wa kuchomekea CD au DVD, chukua mlango unao weza kuchoma DVD au CD ,DVD R
  • Idadi ya Expansion Slot kwa ajili yaku upgrade kompyuta yako
  • Bei utakayo iweza
  • Warranty na Guarantees

MWISHO:
funguka changamoto uliyo ipata kutokana na ukosefu wa elimu ya msingi ya matumizi ya kompyuta

Imeandaliwa na kipenseli

 
Upvote 6
Back
Top Bottom