Fursa: Ufugaji wa Tombo (Quails Farming)

Entareyehirungu

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2006
Posts
488
Reaction score
471
Wakuu Malila, Chasha, Kubota, CONSULT, Mrimi, Franky, mito, Nyenyere, Mvaa Tai, MILLIONS MOVEMENT naomba ambaye ameanza kufuga hawa ndege atushirikishe maendeleo na matokeo.

::::::::::::::::::<<<<<<<<<<<<<>>>>>>>>>>>>>>>>>:::::::::::::::::::::::::::::: :
Part I
[video=youtube_share;sCd2BgCdr18]http://youtu.be/sCd2BgCdr18[/video]
Part II
[video=youtube_share;APjBvAu2cT4]http://youtu.be/APjBvAu2cT4[/video]
Kutokana na hali ya wimbi kubwa la mahitaji ya bidhaa za tombo katika miezi ya hivi karibuni kumelazimisha wafanyabiashara nchini Kenya kote kujiingiza katika biashara mpya ya ufugaji wa tombo.



  • [*=center]Madai kwamba ulaji wa bidhaa za tombo husaidia afya ya mtu ni sehemu ya sababu ya hivi karibuni ya kuongezeka kwa mahitaji nchini Kenya. [Bosire Boniface/Sabahi]



  • [*=center] Sam Ikwaye akionyesha ukusanyaji wake wa matombo katika shamba lake la ufugaji ndege huko Mombasa. [Bosire Boniface/Sabahi]
Mkaazi wa Kiambu Andrew Githinji aliiambia Sabahi kwamba ufugaji wa tombo hauna gharama kuendesha na unaleta mapato mazuri.

"Hauhitaji eneo kubwa. Tofauti na kuku ambao wanahitaji eneo kubwa, viota vya [tombo] vinaweza kuwekwa vibarazani," Githinji alisema.

Alisema kwa mara ya kwanza alivutiwa na mradi kama huo baada ya kusoma kwenye orodha ya vyakula katika hoteli yenye nyota tano huko Nairobi mwezi Januari 2012.

Alipata kuona kitu ambacho hakuwa anakijua: nyama ya tombo ya kubanika. "Nilifikiri kuwa tombo alikuwa aina ya chakula kinachotoka baharini, katika kuchunguza, nilimuuliza mhudumu na alisema ilikuwa ni ndege," Githinji mwenye umri wa miaka 33 alisema.

Githinji, ambaye pia anafuga sungura, alianza kufanya utafiti kuhusu tombo na kugundua kuwa watu wanamfuga ndege huyo. "Sikuwa najua kuwa ndege huyu, ambao wanapatikana kwa wingi kijijini kwangu, angeweza kufugika," alisema. Alinunua ndege wake 20 kwa mara ya kwanza kwa shilingi 250 kila mmoja (dola 2.85), Githinji alisema, akiongezea kwamba kwa sasa ana tombo 520. "Cha kusikitisha tu ni kwamba niligundua biashara hii kwa kuchelewa," alisema Githinji. "Lakini nitwafikia wengine na kwa muda wa miaka miwili nitakuwa na mashine yangu ya kutotolesha itakayosaidia kutotoleshea vifaranga." Mkaazi wa Mombasa Alex Mureithi, mwenye umri wa miaka 39, alisema alishangazwa kwenda katika shamba la tombo baada ya kutembelea katika duka la jumla mwezi Julai 2012.

Aliona dazeni za "mayai tofauti ya tombo" katika rafu ambalo alidhania ni nakshi ya jiwe la sabuni na kugundua kwamba walikuwa wakiuza kwa shilingi 650 (dola 7.43) ukilinganisha na trei la mayai 30 kwa bei ya shilingi 400 (dola 4.57). Mureithi kisha alizungumza na meneja wa duka ambaye alimwambia kwamba wafugaji wa tombo hawawezi kutosheleza mahitaji ya soko, ingawa tombo hutaga mayai karibia kila siku.

"Nilitambua kuwa yalikuwa ni matembezi yenye faida hivyo nilinunua ndege 10. Sasa ninao 900," Mureithi aliiambia Sabahi. "Sijui nini kitatokea katika ufugajii wa tombo kwa siku zijazo lakini sasa ninavuna faida ya juu kabisa."
Anaziuzia hoteli nne huko Mombasa na Nairobi, ambazo zinatoa agizo kwa kila mwezi kwa wafugaji kupata mayai na nyama ya tombo, alisema.

Anatoza mayai yake kwa shilingi hadi 60 (senti 68) kwa kila moja na tombo mzima kwa shilingi 800 (dola 9.14).
Mureithi pia anawafundisha na kuwatembeza wanaotaka kuwa wafugaji wa tombo katika shamba lake kwa kuwatoza shilingi 3,000 (dola 34.3), alisema.
Nzuri kwa afya ya kila mtu?

Mahitaji ya mayai na nyama ya tombo yamesababishwa na ripoti ambazo zinaeleza kwamba kula tombo una thamani ya kiafya.

Yunuke Nyanchama, mkaazi wa Kisii mwenye umri wa miaka 67, aliiambia Sabahi kwamba amekuwa akila mayai ya kituitui kwa miaka miwili iliyopita. Alipatikana na kisukari mwaka 2004 na amekuwa akitumia dawa nyingi bila kuwa na mabadiliko mazuri.

Wakati wa ukaguzi wa kawaida mwezi Mei 2011, hata hivyo daktari wake alipendekeza kwamba ajaribu mayai ya tombo. "Nilistaajabishwa na tiba hiyo, lakini baada ya kutumia mayai hayo na nyama ya ndege, kuna mabadiliko makubwa," alisema.

Vincent Juma, daktari wa Hospitali ya Wilaya ya Mbagathi, aliiambia Sabahi kwamba wakati kulikuwa hakuna utafiti kuhusu faida za kitabibu za mayai na nyama ya tombo, watu wengi wamethibitisha kuwa unafuu baada ya kuvitumia.
"Miongoni mwa wagonjwa ambao walirekodiwa [ni] wale waliopata unafuu mkubwa [ni] wale waliokuwa wakisumbuliwa na kifua kukuu na vidonda. Mgonjwa wa saratani alisema kwamba maumivu aliyokua nayo yamepungua baada ya kutumia mayai hayo," Juma alisema
Wafugaji wa tombo wanahitaji leseni

Kwa sababu tombo wanachukuliwa kama wanyamapori, wafugaji wa tombo kwanza wanahitaji kuomba kibali kutoka katika Huduma za Wanyamapori Kenya (KWS), msemaji wa shirika hilo Paul Udoto aliiambia Sabahi.

Kabla ya huduma hiyo kutoa leseni, viongozi wa KWS wanapaswa kukagua shamba lake kuhakikisha kwamba linakidhi mahitaji kwa ajili ya kufuga tombo, alisema Udoto.

Malipo ya mwaka kwa ajili ya leseni yanagharimu hadi shilingi 2,000 (dola 22.9), alisema, akiongeza kwamba kibali kinaweza kuhuishwa kwa mwaka kulingana na kukamilisha baadhi ya masharti, ikiwa ni pamoja na usafi.

KWS inaendesha ufuatiliaji na ukaguzi wa mashamba kwa vipindi, na hufuta leseni kutoka kwa wafugaji ambao wanakiuka masharti hayo, alisema Udoto. Huduma hiyo ina maombi mengi ya kibali kutoka kwa watu binafsi na vikundi ambavyo vinataka kufanya ufugaji wa tombo, alisema.

Serikali inahamasisha biashara iliyorekebishwa kama njia ya kuanzisha ajira na kuwapa Wakenya mbadala wa vyanzo vya chakula, alisema Udoto, akiongeza kwamba biashara ya tombo imeota mizizi katika mikoa ya Pwani, Mashariki na Kati pamoja na Kaunti ya Nairobi.

KWS pia inatoa leseni za kufuga wanyamapori wengine kama mamba ili kusaidia katika jitihada za utunzaji, alisema.
 
Mkuu Ni kweli na Bahati Nzuri kwa wiki nzima niko Kisumu Kenya na nimeweza kutembelea wafugaji wakubwa kabisa wa Kuku pamoja na Hawa Kware, mkuu huku wanafugwa sana na ni watamu aikuambie mtu,

Ilani kwamba wao huku wanapata sapoti ya Moja kwa moja kutoka KWS-Kenya wildlife Service hii ni TANAPA ya huku kwao, tofauti na Bongo ambako Viongozi wengi ni Conservative huku wameamka sana, na si Kware tu hata Mbuni wanafugwa na wanasoko kubwa sana na eggs shell ya mbuni inabei ya kufa mtu na inasafiliswa kwenda nje kutengeneza mapambo,

Mkuu Kuhusu kuanza Kufuga, Mimi binafisi sijaanza kwa sababu ya kibali, na asikudanganye mtu kwamba unaweza fuga bila kibali, kibali ni muhimu sana.

Upatikanaji wa Kibali ndo ishu, na kuna utaratibu mgumu sana na kupewa kibali cha kuguga Kware na sawa na kupewa kibali cha kufuga wanyama wengine kama Punba milia na kazalika sasa cheki hizo process,

Ila mkuu Kuna Mtu wanguyuko Lindi na kuna process moja au altenative tuliipata ya kuweza kupa kibali ndo tunakomaa na process na Mungu akipenda Kabla ya mwaka huu kuisha tutakuwa tumekipata, make tusha kamilisha kila kitu, Ila sitaweza ku expose hii njia mpaka hapo tutakapo fanikiwa.

SO MKUU UFUGAJI WA HAWA NDEGE NI DILI SANA ILA HATA HUKU HAKUNA ANYE FUGA BILA KIBALI, INGAWA WAO KIBALI KUPATA SI ISHU NI KAZI RAHISI SANA
 

Good,
Week jana nilipita pale Ubungo nikapata kipeperushi kimoja cha mkulima. anasema yy anafuga kware na kanga weupe mitaa ya Kibaha. Ngoja nitafute nimtwangie huyu ndugu.
 
Yes, indeed it is a very enterprising farming, it is growing fast and has a very good future

hata hapa Tanzania wafugaji wameanza kufuga, quail incubation takes only 16-18 days to hatch na kware huanza kutaga kuanzia wiki ya 6 tangu atotolewe

yai la kware linasaidia kiafya na kimagonjwa kwasababu lina kiasi kikubwa sana cha protein
 
Vibali vya Kisekta ni changamoto sana kwa Tanzania. Mfano mbao zimekuwepo toka kuundwa kwa Serikali ya Kwanza lakini hadi leo hatuna utaratibu unaoeleweka wa kutoa vibali vya kuvuna miti! Hali inakuwa ngumu zaidi hasa kwa shughuli mpya ya kiuchumi kama hii ya ufugaji wa Kwale Kibiashara. Utashangaa ya Musa pale utakapoambiwa kwamba kibali cha TANAPA pekee hakitoshi na badala yake unatakiwa kupata vibali zaidi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo (MoLD), Wizara ya Maliasili na Utalii (MNRT), Wizara ya Kilimo na Ushirika (MoAFC), Wizara ya Viwanda na Biashara (MITM). Na hapo ndipo biashara rasmi zinapokuwa ngumu kwa Watanzania.
 
kibali cha kufuga na kuuza kware unatakiwa uwe na
lesseni ya viwanda na biashara
NEMC (mazingira approval)
then Authoritative license from wildlife ministry
 
ontop of that utakapotaka ku cross.border lazima ministry ya livestock wakupe kibali, hawa wapi poa hakuna complications
 

mkuu TANAPA hawahusiki kabisa navibari kwa sababu hifahi zao zote ni full au total prtection, hakuna shughuri za kibinadamu zinaruhusiwa, wanao toa vibari ni Mkurugenzi wa Idara ya Wanyapori ambaye anasimamia Mapori yote ya Akiba ambapo ndo unawez winda au kukumata hao Ndege,

Mkuu ishu ni kwamba Hakuna upndeleo kwa wazawa ukitaka kibali, so wote tuna tunachukliwa sawa tu
 
Mkuu unauhakika na unacho ongea?

yes, ninauhakika .... hapa namaanisha wizara husika ya mwisho kutoa kibali baada ya kuidhinishwa na idara husika ni wizara ya maliasili
 
Mkuu Chasha kama ambavyo daima umekuwa generous kwenye masuala ya kuhabarishana na kubadilishana fursa, nakuomba utakapokuwa umekamilisha na kufanikisha urasimishaji wa shughuli hii, utusaidie kutupatia maelekezo ya hatua kwa hatua kuwezesha upatikanaji wa vibali. Hata sasa naamini unayo mengi ya kutushirikisha
 

Kimasha, Chasha na wengineo,

Mimi najilipua, naanza kuwafuga bila kibali, mpaka waje washituke mimi nishauza mara kadhaa. Hivi kama mimi kwetu kusini kule, na urasimu wote huu, ni gharama sana. hivi kifungo anachopata mtu anayefuga kware bila kibali kinaweza kuwa ni miezi mingapi? au faini sh ngapi?

Kuna mtu aligonga watu wakafa, akalipa laki saba tu. Jamani serikali yetu, urasimu unatulazimisha tutende dhambi na tushindwe kulipa kodi. Mko wapi watendaji wa serikali?
 
Yeah jamani hata kanga wanahitaji vibali lakini tunawafuga tuuu...fugeni na mtu akitaka kuwapata aniambie nimpe contacts
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…