Fursa ujenzi Wa Bomba la mafuta

mjenziwakale

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2015
Posts
954
Reaction score
1,469
Habari zenu wana jukwaa,

Ndo kama Leo tulivotangaziwa na tulivoona Leo ulikuwa ni uzinduzi Wa mradi mkubwa Wa Bomba la mafuta toka Hoima Uganda mpaka Tanga

Mimi kama mdau Wa sekta ya ujenzi ninatoa wito kwa wadau wote katika sekta hii wakiwemo wakandarasi, wahandisi, mafundi mama ntilie n.k tuweze kujadili kuona ni jinsi gani na sisi tutaweza pata nafasi za kuweza kushiriki katika mradi huu.

Naombeni hapa watu tupeane moja mbili tatu kuhusiana na jinsi gani twaweza kushiriki.Hii itatusaidia kujua ni wapi hasa twaweza kuanzia ili kuweza pata fursa kama mheshimiwa rahisi alivoshauri kwamba masubcontractor watawanywe route mzima ili kuweza kumaliza mradi kwa wakati na kwa haraka.

Ikibidi kwa wale waliokuwa tayari na wenye nia ya kushiriki katika mradi huu tuwe na group la whatsaap ili tuweze peana information zikiwemo za toka wizarani, wakandarasi wakuu, bodi ya wakandarasi , bodi ya wahandisi na pia taarifa kutoka site moja kwa moja.

Kupitia humu najua kuna watu wengi wenye uelewa katika huu mradi hivo ni rahisi tutaweza peana updates za kila kitu.

Nakaribisha maoni ya wadau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni mada nzuri na muhimu,kujadili.
Ninavyoona na ufahamu haya yatajitokeza.

Atachaguliwa mkandarasi wa kujenga bomba la mafuta- Huyu itakuwa ni kampuni kubwa ya kimataifa .

Kampuni itahitaji , kampuni ndogondogo ambazo zitakuwa kwa lugha rahisi , vibarua wa fundi mkuu.

Kampuni hizi ndogo ndogo, siyo ndogo ndogo za Kitanzania, kutokana na ukubwa wa kazi iliyopo ya kuchimba, kuweka, kutandaza, kuunganisha mabomba hayoo.

Hizo kampuni ndogo ndogo za nje, hazitaweza kufanya kazi hiyo peke yao, watahitaji watoa huduma mbalimbali ili waweze kufanya majukumu yao.

Hivyo wakandarasi wote hao juu, watakuwa katika taaluma tofauti tofauti, ikiwemo kuchomelea, umeme, kuunganisha nk.

Ili wote wafanye kazi, watahitaji watoa huduma mbalimbali, wakati kazi inaendelea .

Makampuni ya ulinzi na usalama, mafuta ya mitambo na magari, chakula, shughuli za burudani, huduma za afya na matibabu, usafirishaji na bima, kampuni za mawasiliano.

Watoa huduma za vifaa vya kuchomelea, ujenzi, vyuma nk nk .

Makampuni ya ajira , kufanyia usaili nk.


Serikali yetu inahusika, ili kuweza kusaidia kwa kuweka sera na utaratibu wa kusaidia watoa huduma wa Tanzania kufaidika na fursa zilizopo.

Watoa huduma watanzania, inabidi kujipanga kimkakati, ili kuweza kuhusika na fursa zilizopo mbele yetu.

Najua na wengine mna mchango, tusaidie kufafanua kwa ajili ya manufaa ya Taifa na watanzania. Nawasilisha.
 
ni wazo zuri kuna watu wanaitwa ATOGS wao wametengeneza blog kabisa na imezinduliwa tangu mwezi wa sita unalipia kiingilio milion 2 halafu wao wanasaka kila opportunities zitakazokuwa ndani ya OIL and gas lakini target ni bomba la mseveni then watakuwa wanashare na watu wanaruka nazo ila nimejiuliza why 2mil??? kwa nini wadau wenzangu na mie wanaoona 2mil kubwa tusiwe na kijigroup chetu cha whatsap au telegram au vinginevyo tukashare kila information kwa ukaribu na bureee?
 
Mkuu tiyari tushasajili group la whatsap watu washaanza kushusha nondo tiyari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…