Fursa ya biashara kwa mtu mwenye pesa na hajui awekeze wapi

Fursa ya biashara kwa mtu mwenye pesa na hajui awekeze wapi

nitazoea

Senior Member
Joined
Mar 15, 2017
Posts
195
Reaction score
237
Habari JF.

Kuna watanzania wengi wana pesa za kutosha na hawajui wawekeze wapi, Jibu ni hili Mtaani kuna graduates wengi wasio na mitaji na wana mawazo mazuri ya kibiashara.

Fursa ni kwako wewe mwenye pesa na hujui ufanye nini wakopeshe vijana kwa riba nafuu na waweke bond (Dhamana) vyeti vyao vya masomo,hakika ni moja biashara nzuri.

Hakika hakuna graduate atakaye kimbia deni na kuacha cheti chake labda kiwe na zero.Lakini pia wewe mkopeshaji si vema kukopesha pesa nyingi napendekeza maximum iwe 500,000/=. Kwa kufanya hivyo tutapunguza threads za watu kuomba kazi na pia tutaongeza wajasiriamali wengi. (Ewe mjasiriamali anzia sokoni).

Wakopeshaji karibuni na graduates pia karibuni

Uzi tayari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika hakuna graduate atakaye kimbia deni na kuacha cheti chake labda kiwe na zero.Lakini pia wewe mkopeshaji si vema kukopesha pesa nyingi napendekeza maximum iwe 500,000/=.
Wazo zuri.
 
Hakuna cheti chenye thamani ya laki tano,lakini ili kumsaidia mtu ambaye hana dhamana kama nyumba etc....Nina imani hakuna graduate ambaye atachezea hiyo golden chance...na mkataba ni muhimu pia
Dhamana cheti? Serious? Sa mm ukinipa cheti chako afu ukanizima 500k... mm cheti chako kitansaidia nn?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
biashara ya Kukopesha hasa kimtaani mtaani siyo masihara..

kuna rafiki yangu alikua anakopesha kwa kadi za gari
kaishia kuachiwa kadi na Mtu hakulipi..
Kuna mtu anakwambia umkopesha labda laki2. Kwa kuwa una wasiwasi nae unaamua kumpa 50 tu.
Sasa kuilipa hiyo 50 ni hadi mvutane mashati.
Unabaki kujiuliza ningempa laki 2 yote hali ingekuwaje
 
Kuna mtu anakwambia umkopesha labda laki2. Kwa kuwa una wasiwasi nae unaamua kumpa 50 tu.
Sasa kuilipa hiyo 50 ni hadi mvutane mashati.
Unabaki kujiuliza ningempa laki 2 yote hali ingekuwaje
yaani Vicoba vyenyewe huko mitaani vipo hoi..marejesho hakuna.

s
biashara ya kukopesha tuwaachie tunakopesha Ltd..

Bora hata ufungue vibiashara uwaajiri watengeneze mtaji kutokea hapo.
 
Back
Top Bottom