Fursa ya biashara kwenye seķta ya usafiri jijini Mwanza, usipitwe.

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Je wewe una fedha na hauna wazo la biashara, ila unatamani kufanya biashara?
Basi, tega sikio lako la thamani.
Halmashauri ya jiji la Mwanza inaenda kuondoa na kusitisha huduma ya vibasi vidogo vya kubeba abiria maarufu kwa jina la Hiace au vipanya.
Hii ni fursa yako sasa, kuingia kwenye biashara ya usafirishaji ukiwa na basi kubwa aina ya Coaster.
Cha kufanya, ni kitu kimoja. Nunua coaster used, lililo kwenye hali nzuri na uende ukalisajili kwenye njia/ route uitakayo.
Personally, mimi Bujibuji, nauza za gari yangu Toyota Coaster mayai, ya mwaka 1998, namba DER, magurudumu yote mapya, Engine 15B, inahudumu njia ya Makumbusho Mbezi 2.
Karibu ukague gari, njoo na fundi wako.
Tuwasiliane kwa namba 0767/0739-454 455
 
Mkuu, wewe utakuwa na Taaluma ya hali ya juu ya biashara hasa upande wa marketing/promotion. Yaani mbinu uliyotumia kutangaza gari yako ni ya kiwango cha PhD. Hongera Mkuu.
 
Mkuu, wewe utakuwa na Taaluma ya hali ya juu ya biashara hasa upande wa marketing/promotion. Yaani mbinu uliyotumia kutangaza gari yako ni ya kiwango cha PhD. Hongera Mkuu.
Sifa na utukufu ni kwa Yesu Kristo wa Nazareth, aliueniwezesha kutengeneza tangazo hili.
Pia ni yeye atayeenda kusimamia biashara hii.
 
Kuondoa vipanya kwa jiji la Mwanza litakuwa ni zoezi litalochukua miaka kumi! Kwanza abiria wenyewe wa kujaza Coaster wako wapi? Wakiondoa vipanya, Bajaj zita take over (which will be to increase a problem)! Mwanza hakuna movement ya kujaza Coaster kwa Urahisi.
 
Du! Hii tik Tak njoo ilalila-kayenze route mpya
 
Natofautiana na wewe abiria wapo mfano idadi ya watu Mbeya na Mwanza, Mwanza abiria ni wengi kulio Mbeya. Mbeya coaster zimechukua njia zote kuu na daladala ni chache na zinashindwa ushindani na siku si nyingi zitapotea. Vidalala kwa kweli vinaboa angalia viford Arusha jinsi vinavokuwa na usumbufu na hata daladala Mwanza. Nilikuwa Mbeya nilienjoy sana kupanda coaster kwa mishemishe za mjini, naona miji yote inayokuwa kwa kasi ukiacha Dar ambao washavuka stage hiyo waige mfano wa Mbeya kwenye kubadili kutoka daladala kwa wingi mpaka coaster kuwa nyingi.
 
Makonda namadereva wangapi watakosa kazi nakuingia katika uwizi
Tanzania yaviwanda vijana na fursa za ajira
 
Shikamoo braza Bujibuji, naona umejianzishia mpira,umelamba chenga na kujitangulizia mpira had mnele. umetoa wazo zuri sana tena bure kabisa ubarikiwe
 
Makonda namadereva wangapi watakosa kazi nakuingia katika uwizi
Tanzania yaviwanda vijana na fursa za ajira
Ndugu Sina demu sio kweli kwamba kuondoa hiace na kuleta coaster italeta upungufu wa ajira kwani kwa uzoefu ni kwamba hao hao wenye hiace watanunua coaster,na wengine watapeleka coaster zao mwanza so mtu atakayenunua coaster ya braza Bujibuji tayar atatengeneza ajira mbili ya konda na dereva. Hii imefanyika dar,mbeya nk
 
Du ni mbinu ya kumpa mtu sababu ya kununua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…