Unapotaka kufanya biashara na Comoro ni muhimu ukayajua haya
1. Idadi ya watu kule ni takriban laki 8. Hivyo unapoangalia business volume uwe muangalifu, nimeona kwenye post no 71 kuna mtu anataka peleka tani 5 za matunda, Zinaweza zikawa nyingi sana au kidogo
2. Kuna baadhi ya bidhaa wanaoruhusiwa ku import kule ni wenyewe tu, hivyo ili uweze kufanya hiyo biashara lazima ujiunge nao. Katika kujiunga nao usibweteke kuwaamini, kuna mtu aliulizia mambo ya Culture tukambeza humu lakini ni muhimu saana, hawa jamaa kimuonekano ni kama Wazanzibar lakini linapokuja swala la mahusiano ya kifedha wengi wao si waaminifu. Be extra careful
3. Sehemu ya karibu ukitokea Tz kwenda Comoro kwa maji ni Lindi ambapo ni Km takriban 320 mpaka 350
Mpaka mwaka juzi kulikuwa na Meli inafanya trip mara 2 kwa wiki kwenda na kurudi Comoro ikitokea Lindi lakini inaonekana hiyo trip imekufa na ni lazima kutakuwa na changamoto
4. Competitive advantage ambayo tunayo na Comoro ni hiyo ya distance kutoka Lindi kuelekea huko ukilinganisha na Suppliers wengine kama Brazil, China, South Africa, UAE na France
Competitive advantage nyingine ni hiyo ya COMESA na muingiliano wa kiutamaduni na kihistoria
5. Competitive Disadvantage: Our poor brains and Attitudes towards Business
Sent using
Jamii Forums mobile app