Fursa ya juice ya matunda

Fursa ya juice ya matunda

Gluk

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
1,859
Reaction score
3,008
Kwa hapa kwetu Tanzania hii biashara wengi hawaitilii maanani sana na hata wale wanaoifanya wengi wao wanaifanya kawaida sana.
Ila hii ni biashara ambayo ukiwa serious na ukaamua kuifanya kwa kuzingatia kanuni zote unatengeneza faida kubwa.
Na biashara hii haihitaji mtaji mkubwa sana kwa kiasi cha M4 au 5 unaweza kufanya biashara hii ikawa ya kuvutia zaidi.

ZINGATIA HAYA.
Tafuta eneo zuri lililochangamka.
Kodi fremu na uifanye iwe nzuri na ya kuvutia zaidi.
Tafuta mashine za kutengeneza juice ya matunda.
Tengeneza juice ya matunda halisi bila kuchanganya na chochote kile.
Nunua matunda safi na mazuri achana na matunda mabovu na yaliyooza.

Hizi ni baadhi ya juice ambazo ukizitengeneza kwa ufasaha utapiga pesa.

KUMBUKA KUWA HUTAKIWI KUONGEZA MAJI KWA BAADHI YA JUICE.

Juice ya tende hii hutengenezwa kwa.
Kwa maziwa, tende na korosho au karanga pekee, (usiweke maji)

Juice ya tikiti maji pia hutakiwi kuweka maji hata kidogo.

Juice ya miwa
Hii pia hutakiwi kuweka maji hata tone.

Juice ya nanasi: hii hutakiwi kuweka maji hata tone.

Juice ya embe, parachichi, pasion hizi unaweka maji kidogo sana yaliyochemshwa kisha kupozwa ili kulinda afya ya mnywaji kumbuka kuwa huweki sukari bali unatumia asali kiasi.
Kuna aina nyingi za juice ila nimeangalia zile ambazo zimezoeleka kwa wengi na mambo kadhaa ya kuzingatiwa ili kuleta radhaa ya tofauti kwa mtumiaji

Kama una swali au nyongeza unakaribishwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiongozi wewe mwenyewe unatuchanganya kwenye andiko lako, kuna mstari umeandika (Tengeneza juice ya matunda halisi bila kuchanganya na chochote kile)

Halafu kuna mstari umeandika (Juice ya Tende hii hutengenezwa kwa....Kwa Maziwa, Tende, Korosho, na Karanga) sasa mbona hiyo Tende umeichanganya na vitu vingine?

Hapa ndio umenifurahisha! (Juice ya Embe, Parachichi, Pasion hizi unaweza kuweka maji kidogo)

Swali langu kwako: Umeandika juice ya miwa haitakiwa kuwekwa maji hata tone. Je mteja akitaka juice ya baridi tufanyeje au miwa tuweke kwenye Friji?
 
Juice ya miwa inawekwa kwenye friji na si kuwekewa mabarafu kama wengi wanavyofanya maana unakuwa umeondoa radha halisi ya juice ya miwa.

Kwenye juice ya matunda walio wengi huweka radhaa za kimikali fulani ili kuongeza radha sasa mimi nimeandika ili usitumie hizo kemikali badala yake utumie mchanganyiko asili pekee bila kuchanganya vingine visivyo asili.
Karibu kwa swali lingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sauti hiyo unasikika, ila kama juice ya miwa ikiwekwa kwenye friji ambayo ulishauri isiwekwe maji kipimo kitaanza kuuzwa kwa bei gani?

Juice ya miwa inawekwa kwenye friji na si kuwekewa mabarafu kama wengi wanavyofanya maana unakuwa umeondoa radha halisi ya juice ya miwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: apk
Back
Top Bottom