Fursa ya Kilimo cha Korosho Manispaa ya Lindi

Negrodemus

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2010
Posts
2,318
Reaction score
684
Habari njema kwa wakulima wenye ndoto za kuingia kwenye kilimo cha korosho.

Mkurugenzi wa manispaa ya Lindi anawaalika watanzania wote wenye nia ya kulima korosho kuja katika halmashauri yake na kuunga mkono jitihada hizo.

Mpaka sasa Halmashauri imetenga heka 45,000 kwa ajili hiyo mnaweza kuwa mnajiuliza inakuwaje mjini kukawa na mashamba naomba muelewe kuwa manispa ya lindi ndiyo manispaa inayoongoza kwa ukubwa tanzania jiji la Mwanza lenye halmashari mbili linaingia zaidi ya mara mbili jiji la Dar es Salaam lenye manispaa tatu limeizidi kidogo sana manispaa hii.

Kilichofanyika manispaa iliongezewa maeneo ambayo yalikuwa ni Land bank mashamba ya korosho yaliyotelekezwa hifadhi ya misitu n.k ili ikidhi vigezo vya kuwa manispaa kutoka halmashauri ya mji.

Hivyo pamoja na ukubwa wake wote huu eneo linalotumika ni dogo sana eneo kubwa lililobaki ni pori au mashamba yasiyoendelezwa. Sasa manispaa imeamua kufanya mambo yafuatayo kwanza kutumia sheria za ardhi na mazingira misitu n.k kuanzisha program hii mashamba haya yamepimwa sasa tutaondoa mapori yasiyo na faida na kuanzisha misitu ya miti ya korosho hapo tutakuwa tumehifadhi mazingira lakini tumeendeleza ardhi.

Taratibu za kupata mashamba haya unatakiwa kuandika barua kwa mkurugenzi wa manispaa kuomba shamba kulingana na heka unazoona utawez kuzihudumia pia uelewe kuwa kazi ya kuendeleza mashamba haya inaanza mwezi wa pili mwaka huu hakuna kulala.

Manispaa itakupa shamba itakupatia miche ya korosho bure kwani mpaka sasa miche 1,000,000 imeoteshwa na ipo tayari kwa ajili hiyo. Miche hii itasafirishwa na manispaa mpaka eneo la shamba kazi yako ni kusafisha shamba na kupanda.

Shamba hili litamilikishwa kwako baada ya kuendeleza na kuhudumia.

Unatakiwa uelewe kuwa hawatoi mashamba kwa ajili ya kuhodhi bali kwa ajili ya kilimo katika mashamba.

Manispaa itakuletea umeme na maji shambani na njia baada ya kuendeleza.

Heka moja ya shamba inapatikana kwa tsh 10,000 kwa mzawa wa Lindi na 50,000 nje ya Lindi hakuna dalali wa hii kazi msije kuibiwa bure na fedha hii inalipwa katika akaunt ya deposit ya manispaa.

Mkija huku mje na mawazo ya kulima na baada ya hapo ku-process korosho viwandani na si kupeleka minadani lengo la manispaa ni kuwa na uchumi mkubwa wa kilimo cha korosho wenye viwanda vyenye kuchakata malighafi za korosho.

Hii ni plan B baada ya serikali kuchukua kodi za majengo minara ardhi sasa manispaa inataka kupata mapato yake kwenye fursa hii.

Ukipanda korosho mwaka 2018 mwezi wa 2 unauhakika wa kuanza kuvuna mwaka 2020.

Msiseme hatujawaambia karibuni kusini kwa maelezo ya ziada njooni inbox.

Kama uki copy acknowledge basi.

Pamoja tunaweza

Korosho Dhahabu ya kijani

Mawasiliano

Mkurugenzi wa manispaa
Halmashauri ya manispaa Lindi
S. L. P 1070
Lindi
 
Korosho nazo zitakuja kuwa kama ufuta, Bei itashuka Sanaa maana watu wameikimbilia
Mahitaji ya soko ni tani 1000000 uwezo wa nchi ni tani 300,000 kingine tanzania msimu wa korosho ni wa pekee wakati huku zipo wazalishaji wakubwa ivory coast brazil wanakuwa bado fursa bado ipo saana na kama tukawekeza kuwa na viwanda, faida ita triple zaidi ya bei ya mibadani na hili ndiyo lengo.
 
Ungeweka at least na namba za simu pamoja na adress ya kutuma hyo barua ya maombi. Kwa mkurugenzi.
 
Tupe basi dondoo tuanze process za kupata maeneo. umeutelekeza huu uzi Mkuu
 
Nashukukuru kwa kuleta mnyumbuliko mzuri pamoja na abcd kuhusu kilimo cha korosho Lindi.

Je, kwa mfano umelima heka moja, na kilimo kikakubali unaweza vuna wastani wa kiasi gani? Bei ikoje?
Je mpaka nifike kipindi cha mavuno kwa wastani wa heka moja ninaweza kutumia kiasi gani cha hela? Hapa namaanisha gharama za kukodi,kusafisha shamba, mbolea, palizi, dawa n.k
 
swali la msingi sana hili, mkuu majibu tafadhali.
 

Kwa kawaida heka moja linapandwa mikorosho 20 mpaka 25 kitaalamu ila 25 ndiyo inapendekezwa miche bora ya sasa inachukua miaka 2 mpaka kuanza kuzaa na kadri unavyohudumia miaka inavyoenda ndipo mti unazidi kukua na mazao yanaongezeka.

Uzalishaji wa mti mmoja unategemea pia huduma kusafisha shamba kupiga madawa sulphur booster n.k so kadiri unapo upa huduma nzuri basi na mazao pia yanaongezeka.

Huduma ya mkorosho mwanzoni huku miaka miwili ya mwanzo itakua migumu ndiyo maana unashauriwa kupanda na mazao mengine upate fedha za kuhudumia shamba pia ukipanda mazao mengine unapoyahudumia basi na miti ya mikorosho inapata huduma.

Katika project hii kuhudumia shamba jipya la heka moja haizidi 360,000 gharama zitapungua au kuongezeka kulingana na uamuzi wako labour force n.k.

Ila kama mkorosho umeanza kuzaa kadirio la juu kilo tano kutoka kwenye kila mkorosho inatosha kuhudumia mti mmoja ws korosho mti mmoja unatoa kilo 10 - 30 za mikorosho kulingana na uduma unazolipa shamba lako umri mazao yanaweza ongezeka au kupungua.

Na kwa makadirio heka moja inatoa tani 0.28 mpaka 0.40 inategemea huduma unazoupa mti au shamba na umri wa mikorosho yako inaweza zidi au pungua.

Sokoni kwa kilo moja unaweza pata 1000-4000 inategemea hali ya soko mfano kwa siku hizi sote tumeshuhudia kuwa bei katika minada imefika mpaka 3800-4080 kwa kilo ukitoa gharama hapo za uendeshaji kama ushuru n.k unapata si chini ya 3400-3680.

Soko ni la uhakika coz hapa watu wanapeleka minadani kama watu wakaungana wakatengeneza viwanda tusipeleke mnadani tukapeleka kiwandani basi fedha inaongezeka maana wote tunajua huko mitaani korosho iliyobanguliwa inauzwa vipi kwa kilo moja inafika 30,000.
 
Asee, ni jambo zuri. Sasa sijui endapo manispaa ikikua mwenye shamba ataruhusiwa kuuza kama viwanja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…