Fursa ya Kilimo cha Korosho Manispaa ya Lindi


"Katika project hii kuhudumia shamba jipya la heka moja haizidi 360,000 gharama zitapungua au kuongezeka kulingana na uamuzi wako labour force n.k" chief hapa umemaanisha hii gharama ya 360,000 kwa heka moja ni kwa muda wa miaka miwili hadi mkorosho utakapoanza kuzaa au ni zile gharama za mwanzo tu??
 
Mkuu kuna maeneo mawili mkoani Lindi natamani sana nifanye kilimo maeneo hayo 1) Mingoyo 2) na karibu na lake Mkoe.
Nikitaka kupata ardhi maeneo hayo nipeleke maombi hapo mkoani.
 
Sina cha kuandika nimeshapata Eka 10 zangu tayari.Nilibandika uzi siku kadhaa zilizopita kuhusu hii fursa lakini kuna watu walinipinga
 
Mkuu kuna maeneo mawili mkoani Lindi natamani sana nifanye kilimo maeneo hayo 1) Mingoyo 2) na karibu na lake Mkoe.
Nikitaka kupata ardhi maeneo hayo nipeleke maombi hapo mkoani.
Mingoyo ni halmashauri ya manispaa so peleka huko maombi yako ila kwa asilimia kubwa itakua ndiyo haya ambayo wanagawa ktk bproject hii
 
Sina cha kuandika nimeshapata Eka 10 zangu tayari.Nilibandika uzi siku kadhaa zilizopita kuhusu hii fursa lakini kuna watu walinipinga
Pole.
Mi nipo huku lindi so ni uhakika na mashamba yameisha umeshaenda kuoneshwa?
 
Gharama ya kuanzia baada ya hapo ni kusafishia tu mikorosho wengine wanapiga dawa ya kuua magugu wengine wanapanda mazao mengine kunde xhoroko isipokuwa mbaazi n.k wanapohudumia hayo mazao na shamba pia linahudumiwa mpaka likianza kuzaa so ikishakua gharama zinakuwa ndogo sana ni madawa tu
 
Mkuu mkorosho unatumia madawa na mbolea ya aina gani ili uzae vizuri?
 
Korosho ina faida nyingi sana kula korosho nyeupe za kuchemshwa ni bora mara 100 kuliko kula pweza au mihogo mibichi. Ongeza heshima ya ndoa kula korosho nyeupe
Mkuu kwanza nakupongeza kwa kutangaza fursa hiyo japo mimi lo ndo naona....nimechelewa...
mimi nipo Dar ila huwa nafika sana maeneo ya Mtwara na lindi pia....kuna suala moja ambalo nashindwa kulipatia majibu nalo ni WIZI wa korosho pale ambapo zimeshakomaa,niliuliza wenyeji wa huku wenyewe wanaibiwa,wengine wanaamua kufuga nyoka shambani,wengine inabidi ujenge kajumba umuweke Mtu hapo...wewe hili unalizungumziaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…