james msasa
Member
- Sep 27, 2015
- 11
- 6
Tunaomba ushare namba yako ya biashara jaman if private ni issue, kwa wale kina sisi amabo tunahitaji muongozo zaidi. Asante.Soko lipo la uhakika kikubwa ni uthubutu umoja ni nguvu.
Changamoto gani kwa ujimla zilizopo katika zao hili? Hasa gharama za kuhudumia heka moja kwa kipindi cha mwaka mzima?Kwa kawaida heka moja linapandwa mikorosho 20 mpaka 25 kitaalamu ila 25 ndiyo inapendekezwa miche bora ya sasa inachukua miaka 2 mpaka kuanza kuzaa na kadri unavyohudumia miaka inavyoenda ndipo mti unazidi kukua na mazao yanaongezeka.
Uzalishaji wa mti mmoja unategemea pia huduma kusafisha shamba kupiga madawa sulphur booster n.k so kadiri unapo upa huduma nzuri basi na mazao pia yanaongezeka.
Huduma ya mkorosho mwanzoni huku miaka miwili ya mwanzo itakua migumu ndiyo maana unashauriwa kupanda na mazao mengine upate fedha za kuhudumia shamba pia ukipanda mazao mengine unapoyahudumia basi na miti ya mikorosho inapata huduma.
Katika project hii kuhudumia shamba jipya la heka moja haizidi 360,000 gharama zitapungua au kuongezeka kulingana na uamuzi wako labour force n.k.
Ila kama mkorosho umeanza kuzaa kadirio la juu kilo tano kutoka kwenye kila mkorosho inatosha kuhudumia mti mmoja ws korosho mti mmoja unatoa kilo 10 - 30 za mikorosho kulingana na uduma unazolipa shamba lako umri mazao yanaweza ongezeka au kupungua.
Na kwa makadirio heka moja inatoa tani 0.28 mpaka 0.40 inategemea huduma unazoupa mti au shamba na umri wa mikorosho yako inaweza zidi au pungua.
Sokoni kwa kilo moja unaweza pata 1000-4000 inategemea hali ya soko mfano kwa siku hizi sote tumeshuhudia kuwa bei katika minada imefika mpaka 3800-4080 kwa kilo ukitoa gharama hapo za uendeshaji kama ushuru n.k unapata si chini ya 3400-3680.
Soko ni la uhakika coz hapa watu wanapeleka minadani kama watu wakaungana wakatengeneza viwanda tusipeleke mnadani tukapeleka kiwandani basi fedha inaongezeka maana wote tunajua huko mitaani korosho iliyobanguliwa inauzwa vipi kwa kilo moja inafika 30,000.
Hbr me naomba msaada Wa no yakoHabari njema kwa wakulima wenye ndoto za kuingia kwenye kilimo cha korosho.
Mkurugenzi wa manispaa ya Lindi anawaalika watanzania wote wenye nia ya kulima korosho kuja katika halmashauri yake na kuunga mkono jitihada hizo.
Mpaka sasa Halmashauri imetenga heka 45,000 kwa ajili hiyo mnaweza kuwa mnajiuliza inakuwaje mjini kukawa na mashamba naomba muelewe kuwa manispa ya lindi ndiyo manispaa inayoongoza kwa ukubwa tanzania jiji la mwanza lenye halmashari mbili linaingia zaidi ya mara mbili jiji la dar es salaam lenye manispaa tatu limeizidi kidogo sana manispaa hii.
Kilichofanyika manispaa iliongezewa maeneo ambayo yalikuwa ni Land bank mashamba ya korosho yaliyotelekezwa hifadhi ya misitu n.k ili ikidhi vigezo vya kuwa manispaa kutoka halmashauri ya mji.
Hivyo pamoja na ukubwa wake wote huu eneo linalotumika ni dogo sana eneo kubwa lililobaki ni pori au mashamba yasiyoendelezwa. Sasa manispaa imeamua kufanya mambo yafuatayo kwanza kutumia sheria za ardhi na mazingira misitu n.k kuanzisha program hii mashamba haya yamepimwa sasa tutaondoa mapori yasiyo na faida na kuanzisha misitu ya miti ya korosho hapo tutakuwa tumehifadhi mazingira lakini tumeendeleza ardhi.
Taratibu za kupata mashamba haya unatakiwa kuandika barua kwa mkurugenzi wa manispaa kuomba shamba kulingana na heka unazoona utawez kuzihudumia pia uelewe kuwa kazi ya kuendeleza mashamba haya inaanza mwezi wa pili mwaka huu hakuna kulala.
Manispaa itakupa shamba itakupatia miche ya korosho bure kwani mpaka sasa miche 1,000,000 imeoteshwa na ipo tayari kwa ajili hiyo. Miche hii itasafirishwa na manispaa mpaka eneo la shamba kazi yako ni kusafisha shamba na kupanda.
Shamba hili litamilikishwa kwako baada ya kuendeleza na kuhudumia.
Unatakiwa uelewe kuwa hawatoi mashamba kwa ajili ya kuhodhi bali kwa ajili ya kilimo katika mashamba.
Manispaa itakuletea umeme na maji shambani na njia baada ya kuendeleza.
Heka moja ya shamba inapatikana kwa tsh 10,000 kwa mzawa wa Lindi na 50,000 nje ya Lindi hakuna dalali wa hii kazi msije kuibiwa bure na fedha hii inalipwa katika akaunt ya deposit ya manispaa
Mkija huku mje na mawazo ya kulima na baada ya hapo ku process korosho viwandani na si kupeleka minadani lengo la manispaa ni kuwa na uchumi mkubwa wa kilimo cha korosho wenye viwanda vyenye kuchakata malighafi za korosho.
Hii ni plan B baada ya serikali kuchukua kodi za majengo minara ardhi sasa manispaa inataka kupata mapato yake kwenye fursa hii.
Ukipanda korosho mwaka 2018 mwezi wa 2 unauhakika wa kuanza kuvuna mwaka 2020.
Msiseme hatujawaambia karibuni kusini kwa maelezo ya ziada njooni inbox.
Kama uki copy acknowledge basi.
Pamoja tunaweza
Korosho Dhahabu ya kijani
Mawasiliano
Mkurugenzi wa manispaa
Halmashauri ya manispaa Lindi
S. L. P 1070
Lindi
duh mimi nipo nyangao huku,kuna kazi maalumu naifanya hapa hospital,weekend huwa nakuja sana hapo mjini kupata upepo wa nahari,vipi weekend hii nikutafute mumu?Karibuni Lindi wakuu,.
Oh,.me napendela kuwa oceanic beach weekend nyingi...karibu sana au mitema beach pia.duh mimi nipo nyangao huku,kuna kazi maalumu naifanya hapa hospital,weekend huwa nakuja sana hapo mjini kupata upepo wa nahari,vipi weekend hii nikutafute mumu?
Santorini ndio kiwanja changu hapo..
shemeji sio mkali lkn?Oh,.me napendela kuwa oceanic beach weekend nyingi...karibu sana au mitema beach pia.
Hahahaa njoo kwa heshma na taadhima...kule ni national housing labda kama unapafahamu mitufuni bar piashemeji sio mkali lkn?
maana sikawii kujifanya naleta umjini wangu wa kukufuata hapo kota nikaishia kuvunjiwa vioo vya Brevis yangu..
si hizo nyumba karibia na kanisa la RC?
Mmmh kumbe upo Lindi na we.......mwenyewe nipo Lindi napatikana mtaa wa jamhuriOh,.me napendela kuwa oceanic beach weekend nyingi...karibu sana au mitema beach pia.
Weeee jamhuri kule stadium?!Mmmh kumbe upo Lindi na we.......mwenyewe nipo Lindi napatikana mtaa wa jamhuri
Noo ukitoka crdb kuna njia inaelekea ofisi za VSO.....napatikana kadogoo hotelWeeee jamhuri kule stadium?!
sio mwenyeji kiviile ila najua utamtoroka,nitakupa codes then tukutane,tukikubaliana nataka ukanitembeze mbali zaidi ukiwa kama mwenyeji wangu....nataka kuifahamu zaidi Lindi,hasa nikipata mwenyeji wa jinsia yako!Hahahaa njoo kwa heshma na taadhima...kule ni national housing labda kama unapafahamu mitufuni bar pia
njia hiyo si ndio imezibwa inawekwa kiwango dhaifu cha lami mkuu?Noo ukitoka crdb kuna njia inaelekea ofisi za VSO.....napatikana kadogoo hotel
Aaah,kadogoo napafahamu,.niko hapa kidia kwa mama Royal napata breakfast karibu[emoji4]Noo ukitoka crdb kuna njia inaelekea ofisi za VSO.....napatikana kadogoo hotel
Sio ile sasanjia hiyo si ndio imezibwa inawekwa kiwango dhaifu cha lami mkuu?
Ahsante mwaya karibu na wwAaah,kadogoo napafahamu,.niko hapa kidia kwa mama Royal napata breakfast karibu[emoji4]
Hahahaa karibu sana Lindi kuchele,.sio mwenyeji kiviile ila najua utamtoroka,nitakupa codes then tukutane,tukikubaliana nataka ukanitembeze mbali zaidi ukiwa kama mwenyeji wangu....nataka kuifahamu zaidi Lindi,hasa nikipata mwenyeji wa jinsia yako!
Ahsante pia,.Ahsante mwaya karibu na ww