Wadau, chekini taarifa ya fursa hiyo hapo chini kutoka TCCIA;
Ndugu Viongozi wa TCCIA,
Tunapenda kuwajulisha kuwa tumepokea barua kutoka Wizara ya Viwanda,Biashara na uwekezaji kwamba Ofisi ya RAS-Songwe kwa kushirikiana na TCCIA walifanyia kazi fursa ya kuuza mazao ya chakula huko DRC kwa upendeleo maalum na kufanikiwa.
Kufikia makubaliano na Uongozi wa Jimbo la Haut-Katanga umetoa Kibali cha miezi minne(4) kuanzia tarehe 1 Desemba,2018 hadi Machi31,2019 kwa wafanyabiashara wa Tanzania kuuza chakula katika jimbo hilo kwa kiwango chochote walichonacho pasipo kulipa ushuru.
Makubaliano hayo yameeleza kuwa,baada ya kipindi hicho hawataruhusiwa kuuza kwa utaratibu wa kawaida ikiwa ni pamoja na kulipa ushuru.
Hivyo kwa makubaliano hayo,Tani moja(1) ya mahindi itauzwa kwa USD350,Unga wa Mahindi USD 400,Maharage na Mchele USD1,120.Bei hizi ni pamoja na gharama za uchukuzi.
Hivyo wafanyabiashara wote mnashauriwa kutumia fursa hii.
Asanteni sana kwa ushirikiano.
For more enquiries
hq@tccia.com
TCCIA