mwagito25
JF-Expert Member
- Aug 11, 2013
- 633
- 352
Habarini wana jamvi.
Kutokana na kukua kwa kasi ya kuridhisha kwa jiji la Dodoma, kuna mahitaji yanayoongezeka kutokana na umuhimu wake kwa maisha ya binadamu ya kila siku.
Uhitaji wa mboga mboga na matunda unakua kwa kasi kubwa.
Uhitaji huu ni wa wote, yaani wauzaji na wazalishaji.
Kwa wale waliopo au watakaopata mazingira mazuri kwa mjini katikati hii ni biashara nzuri saana endapo huduma yako itakuwa ina ubora mkubwa, yaani mboga zako ziwe katika ubora wa kumvutia mlaji. Mfano kuna sehemu kama majengo sokoni kando ya njia akina mama wanauza mchicha, figili na mnafu ambao hata kama hukuwa na wazo la kununua utanunua.
Upande wa mkulima, nimeona pale magereza (isanga) wanajitahidi kuzalisha mboga nzuri inayopendwa na walaji kwa kuzingitia viwango hasa matumizi ya samadi kwa wingi kuliko mbolea za dukani. Pamoja na jitihada zao lakini hawakidhi mahitaji hata kwa mbali, ukizingatia pamoja na wimbi la wakazi lakini pia uwepo wa wanafunzi wa vyuo mbalimbali nao ni chachu katika hili.
Maoni yangu ni kwamba kwa mtu ambaye anaweza kutatumia maeneo yenye maji ya kutosha yaliyopo karibu na Dodoma mjini mfano Hombolo kutokana na uwepo wa bwawa hii yaweza kuwa fursa nzuri katika kujipatia chochote kitu.
Kila la kheri kwa wapambanaji.