Fursa ya ufugaji wa nyoka

Fursa ya ufugaji wa nyoka

The Initiator huru

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Posts
1,993
Reaction score
2,635
FURSA YA KILIMO CHA NYOKA

Kilimo cha nyoka ni moja ya kilimo chenye faida sana ,mmoja anaweza akaanzisha kilimo hichi ukizingatia thamani ya "snake venom" ipo juu sana. Sumu ya nyoka inatumika kwa wingi kwenye viwanda vya famasia na viwanda vya vipodozi hivyo thamani ya "snake venom " ipo juu sana kutokana na uhitaji wake.

Gram moja ya "snake venom " kwa soko la kimataifa inauzwa $1880, na kwenye soko la Afrika kusini inauzwa kwa makadirio ya Rand 25,000

*Kama unafikiria kuanzisha shamba lako la nyoka ,yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia ili uweze kupata faida ya kutosha kutokana na venom wanayozalisha Nyoka

1. Zingatia hali ya joto na hewa.
Nyoka wanahitaji joto ya kiwango cha 24-29 degrees Celsius nyakati ya siku na 21-24 nyakati za usiku.

2. Mabanda na nyumba za nyoka zinahitaji kusafishwa mara kwa Mara
Hali hiyo itasaidia kukuza uzalishaji wa nyoka kwa wingi. Nyoka wanahitaji kuwekwa mahali salama kuzuia matatizo yeyote ile ya kiafya kuwapata.

3. Nyoka kwa kawaida hula panya 3-4 na hulishwa kwa wiki 3-4 .Nyoka hula panya walio hai lakini wanaweza kula waliokufa pia ,Nyoka hupenda kucheza na panya mwanzo kabla ya kuwala hivyo ni vema kuwapatia walio hai.

Faida za ufugaji wa nyoka
1. Uzalishaji wa venom ambayo ukiuza unapata kiasi kikubwa cha pesa.

2. Hupunguza na kutokomeza wadudu waharibifu kama panya nk.Nyoka chakula chao kikuu ni panya hivyo husaidia kutusafishia shamba au nyumba kwa kuwamaliza wadudu hawa.

Mwisho nawashauri ndugu zangu sio kila tukiwaona nyoka tunawaua ,nyoka ni rafiki zetu na sio maadui.Tuwatumie ipasavyo watatusaidia sana.

Cc; @jifunze_kilimo_na_ufugaji
 
Mkuu hongera Ila Waulize maswali wote wameuliza maswalo muhimu
Shamba liko wapi
Unasafishaje banda?

Mimi nauliza

Unaishije na hao nyoka wenye sumu?
 
Kuna Kipindi kinaitwa
SNAKE IN THE CITY
Kipo Channel Ya
NATIONAL GEOGRAPHIC
 
Maelezo ya Mleta uzi hayajitoshelezi kabisa.

Hilo soko la venom lipo nchi gani? na nikivuna hiyo sumu naipaki vipi kuifikisha kwa Mnunuzi?.

Sio Nyoka wote wana sumu, sasa unaposhauri tu juu juu Mtu afuge Nyoka huoni kwamba Mtu atajaza banda ili hali ajikute hana hata Nyoka mmoja mwenye sumu inayohitajika sokoni? hivyo Mtu huyo atakuwa amepoteza muda na pesa?.
 
Kuna fursa zibakie tu kwenye makaratasi ya mafunzo ila kufanya am sorry.
 
Kuna yule host wa Snake in the City ya Nat Geo, Simon Keys yeye anafuga aina nyingi za venomous snakes ila kuna jamii moja wapo anafanya exchange na kampuni yenye shamba la zabibu anawapa nyoka kwa ajili ya kula panya na yeye hupewa pipa za mvinyo in return..bongo sijui kama inawezekena hii!
 
Back
Top Bottom