Fursa za biashara nchi ya Thailand

Fursa za biashara nchi ya Thailand

Tena wa Thai ni watu waungwana kweli,hakuna uwizi,jiji la Bangkok lina watu wengi na msongamano wa watu ni mkubwa hasa kwenye maduka na zile sehemu za kusalula nguo mpya kwa mafungu,wala hutasikia mtu anakusachi,nguoza madukani nyingi zipo kama display ukitaka mzigo unatoa oda,lakini zile za kuuzwa mezani sehemu ya wazi ndio bei rahisi sana,Ila kaa macho macho ma Ladyboy wapo wengi sana,huwezi kutofautisha kati ya mwanaume au mwanamke,huko zile sheria za M7 hazitafika milelel.Vyakula vipo vingi na matunda ya kumwaga,ila kuna harufu kali ya vyakula ambayo ni kama uvundo na kitimoto kwa wingi ingawaje kuna samaki na matunda mbalimbali,pia kuna migahawa uswahilini ambayo ni Halal.
Na mwisho jiepushe na waNaija ukiwa huko wako wengi na wengi wameo wanawake wa Kithai na wana biashara zao ,lakini biashara zao nyingine ni za sembe so ukienda ujihadhari
 
Nimecheka sana hapa kaka kuhusu ladyboy umenikumbusha mbali.
Lastime jamaa yangu alichukua ladyboy akijua ni demu kuingia nae room demu kusaula viwalo kumbe ni ladyboy jamaa alikimbia akaja kunigongea room kwangu.
Kuweni makini na ladyboy ni wazuri kama wanawake kabisa.
 
Hata jf tuna ladyboy mmoja namjua anyways safi sana money stunna
 
Chukua Like Mkuu! Vijana tuache kusumbuliwa na siasa zinazopotosha, maendeleo yetu yanaletwa na sisi wenyewe, huwezi kukaa umebweteka ukitegemea maendeleo yako yatatokea tu yenyewe, wewe ndie unaepaswa kuyasababisha kwa constructive ideas za kujikwamua na si majungu na matusi ya kijiweni. Mwanzisha thread umenifumbua macho and Im thinking so hard on how to pursue this great opportunity! Tutatafutana PM

Mkuu nakubaliana nawe hapo kwenye red. Lakini sidhani kama watu wanaweza kuendelea wasipokuwa na siasa safi na uongozi bora. ndio maana hata humu ndani watu wanahofu na TRA, TFDA, TBS nk. ndio maana wengine wanauliza uwezekano wa kupitishia bidhaa zao Uganda au Kenya. ndio maana watu humu wanataka kujua habari za usalama wao huko Thai na habari kama kuna ubaguzi au la. hayo yote yanathibitisha umuhimu wa kuwa na uongozi bora unaoweza kuwawezesha wananchi kutumia fursa kama hizi bila kuwakwaza kwa makodi makubwa yasiyoeleweka, pasipo ucheleweshaji wa bidhaa bandarini kwa sababu za kiurasimu tu nk. lakini mwisho nakubaliana na wewe kuwa inatubidi tubalance matumizi ya muda wetu katika kujadili siasa na kutekeleza majukumu yetu ya kimaendeleo nje ya mijadala ya kisiasa.
 
Nimecheka sana hapa kaka kuhusu ladyboy umenikumbusha mbali.
Lastime jamaa yangu alichukua ladyboy akijua ni demu kuingia nae room demu kusaula viwalo kumbe ni ladyboy jamaa alikimbia akaja kunigongea room kwangu.
Kuweni makini na ladyboy ni wazuri kama wanawake kabisa.

Thats why they call it bangkok..........
 
Nami najiandaa vizuri panapo maajaliwa mwezi Nov. Nitatia timu Thailand kibiashara zaidi
 
Nchi ya Thailand ni kama unavyoona china imepiga hatua kubwa kwa viwanda na leo nitawaonyesha fursa ili kusaidiana hasa kwa wale wajasiriamali.

Kwanza kabisa wana hotel nyingi na nzuri na kwa bei rahis sana .mfano wa hotel hizo ni Airy resort bei yake ni tzsh 21,000 kuna silva gold garden bei tzsh 23,000 etc hizo zipo karibu na airport na hizo room kuna wifi, simu, maji, vitanda safi, room kubwa etc.

Mji wao mkuu ni Bangkok. Kwa wale wenye maduka ya nguo ya kuuza shirts,blouses,skirts, jackets, ties, bags etc ni fursa nzuri kwenu sababu kule vitu bei ni sawa na bure ata nguo nyingi na viatu zinazouzwa Marekani zimetoka Bangkok Thailand, China na Korea.

Sababu kuu ya bei yao kuwa ndogo ni kuwa wanatumia cheap labor na wana viwanda vingi sana.

Unaweza kununua bidhaa zako kwenye shopping mall au kwenye masoko ya bei rahis mfano kuna soko la weekend linaitwa "chatuchak weekend market " hapo wakuu vitu bei ni sawa na bure na nguo mpya quality nzuri.

Mfano bei za tshirt, jeanz unaweza pata kuanzia 50baht sawa na dolla 1.60 adi 100 baht hizi bei ninazokutajia ni kama ukinunua kwa bidhaa moja moja kwa maana hiyo ukinunua kwa jumla bei inakuwa chini ya hapo.

Kwa bei ya kitu kimoja moja kiatu kizuri cha 60,000 bangkok utanunua kwa dolla 3 au 4.

Pia unaweza kubageini kwa maana hiyo ukinunua kwa uwingi unapunguziwa.

Pia kuna market nyingine kama Prutunam market.

Kwa wale wenzangu mnaopenda kufanya shopping kwenye mall

Kuna shopping mall kama Terminal 21 ,shopping mall mbk etc.

Kwa hiyo ni jukumu lako kuamua kama unafanya shopping kwa market za kawaida ambazo bei uwa cheap zaidi kutokana ufanyika sehemu ya wazi. Na ukipenda shopping mall sawa pia.

Pia kule bidhaa za heleni za kina dada na cheni zipo kule bei ya cheni ya silver ni rahis zaidi kuliko tz.

Tiket za ndege bei utegemea umekata ndege gani na umekata mapema au ...
Hivo unaweza kufatilia ilo.

Kuna wafanyabiashara wa maduka wengi kariakoo nawajua kama 3 waliotajirika kupitia kufata mzigo uko.

Mwenye kuongezea ujuzi ruksa pengine kuna vitu nimesahau pia kama nimeandika kiswahili kibovu samahan.

Kazi kwenu sasa

Duh kujikwamua c ndio huku
 
Asante sana kwa taarifa vp kuusu smartphone na tablet upo zpo kwa bei nzuri
 
Mimi mwenyewe hilo lilikua swali langu nlkua nataka kuuliza cjajua inakuaje ila nafkiri kupitia mombasa inakua more better
 
Mkuu Dolevaby umesomeka sana japo ndio kwanza tuko kwenye utungaji wa mimba kama ingewa ni mtoto. Ila kwa kuwa tunaamini inawezekana then yatatimia muda c mrefu na ikishakuwa hivyo ni haki ya jukwaa hili kupewa mrejesho.
Wkuu vipi mlishafanikisha safari? tunaomba feedback please.
 
tusisahau na uzalishaji jamani taifa la kichuuzi ni genge la bidhaa za wengine tusiwaachie tu wageni waje kufungua viwanda nasi tukamate fursa sio kubakia kuwa machinga wa wenzetu hatutaendeleza taifa.
 
Mimi binafsi nilifanikisha na nitazidi. Sijui wengine
Mkuu nashukuru sana. Binafsi nahitaji kununua used Tractor na attachments zake kama plough, harrow rotervetor na reck. Preferably aina ya KUBOTA au John Deere. Najua naweza kuagiza kupitia kwenye mtandao, lakini nina hofu ya kutapeliwa. Nimesearch kwa mfano nikalipata Kubota M7040 for sale - Price: $23,489, Year: 2009 | Used Kubota M7040 tractors 60-79 hp - Mascus USA. I needed a cheaper option na nilidhani labda nikienda physically nitaweza kufanikiwa.
 
Back
Top Bottom