Fursa za biashara nchi ya Thailand

Fursa za biashara nchi ya Thailand

Mkuu nilienda mwezi April nilitembelea maeneo yote aliyosema stuna.

Gwishaga ma-mihayo lulu!

Je, fursa alizozisema Money Stunna ulizionaje? Je, ulienda kibiashara au kutalii? Tunaomba maelezo zaidi ya hiyo sentensi yako 1!!
 
Vipo hivyo
Kuna hii ishu ya hawa TBS kwa hapaBongo vp bidhaa gani z umeme kwa maana ya product maana hapa vingi ni product za liper, tronic, havells India na Ornesto sasa hivyo vya ki Thai itakuwaje na vipi kuhusu bei zao na mtaa ambao vinapatikana kwa wingi
 
Nasikia kuna baadhi ya makampuni wanahonga TBS ili watu wengine wasilete vifaa vya umeme
 
Gwishaga ma-mihayo lulu!

Je, fursa alizozisema Money Stunna ulizionaje? Je, ulienda kibiashara au kutalii? Tunaomba maelezo zaidi ya hiyo sentensi yako 1!!

Niliienda kimasomo fursa ni nyingi sana hasa mambo ya nguo na electronics bei zipo chini sana. currency ni 1bhat=50.9 tshs. hotels ni nzuri kwa bei ya chini ila usikae jirani na Airport. Nilifikia hotel moja ipo katikati ya Bangkok inaitwa i-resident kuna stesheni kwa hiyo nilikuwa na access ya kwenda popote kwa bei nafuu. mfano kwa bei ya rejareja tshirts na mashati mazuri ya viwango ni wastani 150 hadi 200 bhat ambayo hapa utanunua kuanzia 25000.
 
Hii nakubaliana nayo asilimia mia moja...nlikua Bangkok for two weeks.. nlipitia night market kama ASIA TIQUE, huwez kuamini bei ya vitu huko. Ni nadra kukuta simu za nokia huko ni IPHONE kwa sana hata watoto wa primary wanatumia smart phone huwez amini but its true and cheap..You guys nawapa go ahead kwenye hii fursa.
Santeee mkuu kwa hii taarifa,je ni kama bei gani hizo IPHONE?
Nalog off
 
Nchi ya Thailand ni kama unavyoona china imepiga hatua kubwa kwa viwanda na leo nitawaonyesha fursa ili kusaidiana hasa kwa wale wajasiriamali.

Kwanza kabisa wana hotel nyingi na nzuri na kwa bei rahis sana .mfano wa hotel hizo ni Airy resort bei yake ni tzsh 21,000 kuna silva gold garden bei tzsh 23,000 etc hizo zipo karibu na airport na hizo room kuna wifi, simu, maji, vitanda safi, room kubwa etc.

Mji wao mkuu ni Bangkok. Kwa wale wenye maduka ya nguo ya kuuza shirts,blouses,skirts, jackets, ties, bags etc ni fursa nzuri kwenu sababu kule vitu bei ni sawa na bure ata nguo nyingi na viatu zinazouzwa Marekani zimetoka Bangkok Thailand, China na Korea.

Sababu kuu ya bei yao kuwa ndogo ni kuwa wanatumia cheap labor na wana viwanda vingi sana.

Unaweza kununua bidhaa zako kwenye shopping mall au kwenye masoko ya bei rahis mfano kuna soko la weekend linaitwa "chatuchak weekend market " hapo wakuu vitu bei ni sawa na bure na nguo mpya quality nzuri.

Mfano bei za tshirt, jeanz unaweza pata kuanzia 50baht sawa na dolla 1.60 adi 100 baht hizi bei ninazokutajia ni kama ukinunua kwa bidhaa moja moja kwa maana hiyo ukinunua kwa jumla bei inakuwa chini ya hapo.

Kwa bei ya kitu kimoja moja kiatu kizuri cha 60,000 bangkok utanunua kwa dolla 3 au 4.

Pia unaweza kubageini kwa maana hiyo ukinunua kwa uwingi unapunguziwa.

Pia kuna market nyingine kama Prutunam market.

Kwa wale wenzangu mnaopenda kufanya shopping kwenye mall

Kuna shopping mall kama Terminal 21 ,shopping mall mbk etc.

Kwa hiyo ni jukumu lako kuamua kama unafanya shopping kwa market za kawaida ambazo bei uwa cheap zaidi kutokana ufanyika sehemu ya wazi. Na ukipenda shopping mall sawa pia.

Pia kule bidhaa za heleni za kina dada na cheni zipo kule bei ya cheni ya silver ni rahis zaidi kuliko tz.

Tiket za ndege bei utegemea umekata ndege gani na umekata mapema au ...
Hivo unaweza kufatilia ilo.

Kuna wafanyabiashara wa maduka wengi kariakoo nawajua kama 3 waliotajirika kupitia kufata mzigo uko.

Mwenye kuongezea ujuzi ruksa pengine kuna vitu nimesahau pia kama nimeandika kiswahili kibovu samahan.

Kazi kwenu sasa

downloadimage.raw


Kwa madini haya you guy have to be exempted from tax!
 
uzi huu umenifungua macho sana na umenifanya nising'ang'anie kufanya biashara sehemu moja kumbe fursa ziko nyingi asanteni sana kwa kunielimisha hapa nimepata kitu wewe na Money Stunna kweli jf kuna mambo mazuri ya ya kibiashara

mkuu ulifanikiwa kwenda? Tafadhali Toa mrejesho ili watu wengine wapate amani na wafanikiwe PIA.
 
Last edited by a moderator:
hapa ndo utajua wabongo na roho za korosho, no feedback, au wale mliokuwa mnajikusanya ndo mbwembwe zilikuwa, ziliishia ukikongoni huku kwetu tunaita mizuka.

safi stuna kwa roho safi ila wengi wetu hatuna iyo roho

Mkuu sio roho ya korosho, ykiona kimya ujue bado vibubu havijajaa....

Tutarudi tu hapa!
 
uzi huu umenifungua macho sana na umenifanya nising'ang'anie kufanya biashara sehemu moja kumbe fursa ziko nyingi asanteni sana kwa kunielimisha hapa nimepata kitu wewe na Money Stunna kweli jf kuna mambo mazuri ya ya kibiashara

Cousin.. Mir tangu nilipouona huu uzi nimeanza kuweka akiba kwenye kibubu na Mungu akipenda November naweza tia maguu hukoo!!

Hebu tuwasiliane kwa maelezo zaidi kama utapenda kwenda!!
 
Last edited by a moderator:
Cousin.. Mir tangu nilipouona huu uzi nimeanza kuweka akiba kwenye kibubu na Mungu akipenda November naweza tia maguu hukoo!!

Hebu tuwasiliane kwa maelezo zaidi kama utapenda kwenda!!

kweli umepania yaan mpaka kieleweke
 
Back
Top Bottom