Fursa za biashara zipo, vijana wa Dar es Salaam ni wazembe tu

Fursa za biashara zipo, vijana wa Dar es Salaam ni wazembe tu

Uchukue asali dar ukauze tabora na singida??? Mkaa uutoe dar ukauze morogoro doh..😄 Au umemaanisha vice versa mkuu
 
Mimi nilipoanza kulima ndipo niliona Dar kuna vijana wazembe sana yaani wamekaa na wanawaza kuuza viatu na nguo tu hakuna mawazo mbadala yaani hawawazi mambo makubwa.

Nimetoka Dar na nimefanikiwa katika kilimo ila Dar wanawaza tu kufungua maduka ya nguo, viatu na simu. Mfano kijana hapo Dar kuna magunia mengi ya mkaa yanaingia kila siku kutoka maeneo mbalimbali ukichukua magunia yako 10 na Canter upeleke Morogoro au Tanga ndani ya siku 3 mkaa umeisha unarudi Dar kufunga mzigo mwingine.

Basi achana na hilo la mkaa, chukua zako asali lita kuanzia 100 weka kwenye vibebeo safi na nembo yako pia, ingia Tabora au Singida uza ndani ya muda mfupi unarudi kufunga mzigo mwingine hiyo kumbuka ni chini ya wiki moja unaweza kuuza lita 100 za asali.

Chukua mafuta ya Alizeti kiasi cha kutosha ingia Mwanza piga biashara usisubiri serikalini ikuambie fursa, fursa ni nyingi sana hapo Dar ila wengi wamekariri fursa aina moja tu.

Kama kuna yeyote atakuwa tayari nitamsaidia alete biashara yake huku nitamsaidia kutafuta masoko. Pia mjaribu kwenye kilimo sio biashara tu.



Sent using Jamii Forums mobile app

Si kwa wanaume tu wa Dar bali hata wanawake wa huko wako hivyo....yaani bongo fleva imewaharibu sana vitoto vya ule mji, hawafanyi kitu mpaka waambiwe na msanii wa fleva.
 
Wee jamaa itakuwa una matatizo ya akili...! Yani utoe mkaa dar upeleke mikoani??????[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
😂😂😂😂😂 Hata wale jamaa wa vibali wakikutana na wewe watasema huyu mtu ni chizi na watakuacha, wala hawatakukamata
 
Huyu mwenzenu anawafanya nyie HAMNA AKILI.
yaani ana waambia mchukue asali DAR-ES-SALAAM MUENDE MKAUZE SINGIDA NA TABORA.,[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
i think he meant viceversa ili upate kufikiria na ww, .. maana tabora ndo inakopatikana asali kwahyo unaleta dar!! ametumia mfumo wa kutuelewesha kama yule mwalimu anaewambia natoka sasa mpige kelele.. ila anamaanisha ole wenu mpige kelele!.
Hivi kweli ununue mkaa kutoka dar upeleke morogoro mtoa mada uko serious kweli?

Utoe asali dar upeleke tabora au singida hiyo faida utaipataje sasa.

Mada uliyoleta ni nzuri ila punguza utani mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom