Fursa za biashara zipo, vijana wa Dar es Salaam ni wazembe tu

[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Ulivyo maliza darasa la Saba ukaenda Dar kusaka maisha ukamuomba mjomba Wako akutafutie kazi hata ya udaktari. Ukaja kupata kazi ya utanesco, mbona hukuchangamkia fursa? JUST KIDDING

Tatizo la vijana wanajipa vyeo ambavyo hawana, kazi wanachagua, mawazo hawana.mapya.

Sent using LEAGOO M12
 
waliosoma tu alimradi kuona akichoandika watabaki kumuona mtoa mada ni mjinga ila kwa waliofikiria mpka ndani ya mistari hyo watamuelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajuwa kuandika au kuzungumza ni rahisi sana. Je amefikilia mtaji ametoa wapi hyo kijana wa mtaani. Anajuwa changamoto za kusafiri biashara zilivyo au anaona mtu anashusha mzigo wake yeye anahisi simple tu kama mjomba ake anavyofanya hiyo kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilipoanza kulima ndipo niliona Dar kuna vijana wazembe sana yaani wamekaa na wanawaza kuuza viatu na nguo tu hakuna mawazo mbadala yaani hawawazi mambo makubwa.

Nimetoka Dar na nimefanikiwa katika kilimo ila Dar wanawaza tu kufungua maduka ya nguo, viatu na simu. Mfano kijana hapo Dar kuna magunia mengi ya mkaa yanaingia kila siku kutoka maeneo mbalimbali ukichukua magunia yako 10 na Canter upeleke Morogoro au Tanga ndani ya siku 3 mkaa umeisha unarudi Dar kufunga mzigo mwingine.

Basi achana na hilo la mkaa, chukua zako asali lita kuanzia 100 weka kwenye vibebeo safi na nembo yako pia, ingia Tabora au Singida uza ndani ya muda mfupi unarudi kufunga mzigo mwingine hiyo kumbuka ni chini ya wiki moja unaweza kuuza lita 100 za asali.

Chukua mafuta ya Alizeti kiasi cha kutosha ingia Mwanza piga biashara usisubiri serikalini ikuambie fursa, fursa ni nyingi sana hapo Dar ila wengi wamekariri fursa aina moja tu.

Kama kuna yeyote atakuwa tayari nitamsaidia alete biashara yake huku nitamsaidia kutafuta masoko. Pia mjaribu kwenye kilimo sio biashara tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mku uko Mkoa gani.
Kwani nipo Dar natafuta biashara mbadala
 
Yani utoe mkaa dar upeleke moro? Hii ni moja ya maajabu saba ya dunia ni sawa na kutoa maji kisimani kwenda kujaza baharini
 
Anifochunatiri mleta mada kaukimbia uzi wake maana si kwa matango pori haya aliyoyaleta.
 
Sasa hapo si we ni kujiongeza tuuu
Mkaa toa mkoani leta dar Asali chukua tabora Singida leta dar unaafunga hesabu
 
Mimi nilipoanza kulima ndipo niliona Dar kuna vijana wazembe sana yaani wamekaa na wanawaza kuuza viatu na nguo tu hakuna mawazo mbadala yaani hawawazi mambo makubwa.

Nimetoka Dar na nimefanikiwa katika kilimo ila Dar wanawaza tu kufungua maduka ya nguo, viatu na simu. Mfano kijana hapo Dar kuna magunia mengi ya mkaa yanaingia kila siku kutoka maeneo mbalimbali ukichukua magunia yako 10 na Canter upeleke Morogoro au Tanga ndani ya siku 3 mkaa umeisha unarudi Dar kufunga mzigo mwingine.

Basi achana na hilo la mkaa, chukua zako asali lita kuanzia 100 weka kwenye vibebeo safi na nembo yako pia, ingia Tabora au Singida uza ndani ya muda mfupi unarudi kufunga mzigo mwingine hiyo kumbuka ni chini ya wiki moja unaweza kuuza lita 100 za asali.

Chukua mafuta ya Alizeti kiasi cha kutosha ingia Mwanza piga biashara usisubiri serikalini ikuambie fursa, fursa ni nyingi sana hapo Dar ila wengi wamekariri fursa aina moja tu.

Kama kuna yeyote atakuwa tayari nitamsaidia alete biashara yake huku nitamsaidia kutafuta masoko. Pia mjaribu kwenye kilimo sio biashara tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
kila mtu anaishi apendavyo,usifosi wat kufanana kama umefanikiwa kwenye kilimo ni wewe,hao wanaoza nguo au viatu ni biashara zao
 
Back
Top Bottom