Fursa za kufundisha watu Kiswahili ni zenu Watanzania

Fursa za kufundisha watu Kiswahili ni zenu Watanzania

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Hii fursa ya kufundisha watu Kiswahili duniani na Afrika ni kwenu wa Tanzania ninyi ndo watu ambao mnaongea Kiswahili sanifu tofauti na Wakenya pamoja na sisi Wakongo.

Lakini kwenye makundi ya promote Kiswahili to the world na le swahili c'est la fierté de l'Afrique sijawahi kuona Watanzania kwenye kundi hata moja hapa zaidi ya Wakenya tu.

Pia kuna watu wengi wanataka kufundishwa Kiswahili, Wakenya wana changamkia fursa hizo kwenye mitandao ya kijamii. Hizi zote ni fursa kwenu au ninyi sio watu wakuchangamana na watu wengine.
 
Tatizo letu watz tuliowengi kuzungumza kiingeleza ni shida na tumeshupaza shingo kwenye kuchenji mfumo wetu wa elimu.

Eti tunajifananisha na wachina
Ndiyo ajabu!
Wanasemaga Kiswahili kilizaliwa Tanzania, kikakulia Kenya, kikafia Uganda, kikapelekwa kuzikwa Kongo..
Huko Kongo kilipozikwa wanakifundisha duniani Watanzania wamelala tu🙄
 
Mkuu hizo fursa tunazihitaji tatizo la huku Tanzania hatupati taarifa , Mkuu ukipata taarifa za fursa jaribu kutuletea .
Huu ndiyo utanzania wenyewe.

Nani aje kukugongea nyumbani kwako kukuletea taarifa ya fursa ya kiswahili ?kwa mtazamo huu Wacha wakenya wazidi kutupiga bao.
 
Huu ndiyo utanzania wenyewe.

Nani aje kukugongea nyumbani kwako kukuletea taarifa ya fursa ya kiswahili ?kwa mtazamo huu Wacha wakenya wazidi kutupiga bao.
Kama Una taarifa it is could be nice ungefanya Ku-share hapa .
 
Back
Top Bottom