Fursa za mikopo, wakopeshaji na wakopaji tukutane.

Wakuu kwa mtu anayetoa mikopo naomba anicheki tafadhali..nipo g/mboto na nahitaji 300k..pia mnaweza kunielekeza wapi naweza pata huu mkopo.
 
Ntawezaje kuwakopesha watu vijijini ambao uwezo wao wa kupata pesa ya marejesho ni mdogo?
asante kwa swali zuri, kabla ya kumkopesha mtu yeyote lazima umfanyie tathimini, tathimini hii inaweza kuwa na scope tofauti, tathimini hii ni uwezo wa kukopa, anaweza asiye na uwezo wa kukopa ila akawa na wadhamini wenye uwezo wa kulipa lolote likitokea. Watu wa kijijini si kwamba hawana uwezo, wanao, wana mashamba na wana mifugo, hizi ni mali. Kifupi mbinu zipo nyingi, unaweza kuwabana kuweka dhamana ya mali zao kama mashamba au kuwa na wadhamini wenye uwezo wa kulipa, siku hizi pia kuna mikopo ya vikundi, hii ni moja ya njia nzuri ya kuwabana na pia kupata watu sahihi, maana moja ya misingi ya kukopesha ni pamoja na kupata watu sahihi, hivyo watu wakikubali kuwa kikundi inasaidia sana kubana wao kwa wao. Mkuu swali lako ni pana japo nimejitahidi kutoa mbinu. Pia kwa wakulima unaweza kuwabana mazao yao waliyolima yakawa dhamana, ukaweka udhibiti wakati wa kuvuna ili upate chako, yote kwa yote hakuna biashara isiyo na risk.
 
mkuu umejibu vyema.
 
wakopeshaji nashangaa hawajitokezi kuja kupata wateja humu.
 
Wakuu kwa mtu anayetoa mikopo naomba anicheki tafadhali..nipo g/mboto na nahitaji 300k..pia mnaweza kunielekeza wapi naweza pata huu mkopo.
nashangaa wamekuwa wazito kujitokeza.
 
Mkuu umenifungua! Hii kitu nilikuwa naiona kama fursa ili nilikuwa nashindwa kujua nitafanyaje. Asante sana. Long live JF!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…