Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
asante kwa swali zuri, kabla ya kumkopesha mtu yeyote lazima umfanyie tathimini, tathimini hii inaweza kuwa na scope tofauti, tathimini hii ni uwezo wa kukopa, anaweza asiye na uwezo wa kukopa ila akawa na wadhamini wenye uwezo wa kulipa lolote likitokea. Watu wa kijijini si kwamba hawana uwezo, wanao, wana mashamba na wana mifugo, hizi ni mali. Kifupi mbinu zipo nyingi, unaweza kuwabana kuweka dhamana ya mali zao kama mashamba au kuwa na wadhamini wenye uwezo wa kulipa, siku hizi pia kuna mikopo ya vikundi, hii ni moja ya njia nzuri ya kuwabana na pia kupata watu sahihi, maana moja ya misingi ya kukopesha ni pamoja na kupata watu sahihi, hivyo watu wakikubali kuwa kikundi inasaidia sana kubana wao kwa wao. Mkuu swali lako ni pana japo nimejitahidi kutoa mbinu. Pia kwa wakulima unaweza kuwabana mazao yao waliyolima yakawa dhamana, ukaweka udhibiti wakati wa kuvuna ili upate chako, yote kwa yote hakuna biashara isiyo na risk.Ntawezaje kuwakopesha watu vijijini ambao uwezo wao wa kupata pesa ya marejesho ni mdogo?
mkuu umejibu vyema.Kila mtu anajua alikopata mtaji wake namaanisha kwamba huenda na wenyewe walikopa sehem ili waje watoe iyo huduma, wengine wawekezaji ni pesa zao za mfukoni, wengine hawazingatii lolote kama wamekopa au ni mtaji wanajipangia tu wanachokiangalia ni faida itakayo patikana basi.
Mkuu umenifungua! Hii kitu nilikuwa naiona kama fursa ili nilikuwa nashindwa kujua nitafanyaje. Asante sana. Long live JF!asante kwa swali zuri, kabla ya kumkopesha mtu yeyote lazima umfanyie tathimini, tathimini hii inaweza kuwa na scope tofauti, tathimini hii ni uwezo wa kukopa, anaweza asiye na uwezo wa kukopa ila akawa na wadhamini wenye uwezo wa kulipa lolote likitokea. Watu wa kijijini si kwamba hawana uwezo, wanao, wana mashamba na wana mifugo, hizi ni mali. Kifupi mbinu zipo nyingi, unaweza kuwabana kuweka dhamana ya mali zao kama mashamba au kuwa na wadhamini wenye uwezo wa kulipa, siku hizi pia kuna mikopo ya vikundi, hii ni moja ya njia nzuri ya kuwabana na pia kupata watu sahihi, maana moja ya misingi ya kukopesha ni pamoja na kupata watu sahihi, hivyo watu wakikubali kuwa kikundi inasaidia sana kubana wao kwa wao. Mkuu swali lako ni pana japo nimejitahidi kutoa mbinu. Pia kwa wakulima unaweza kuwabana mazao yao waliyolima yakawa dhamana, ukaweka udhibiti wakati wa kuvuna ili upate chako, yote kwa yote hakuna biashara isiyo na risk.