Kaudunde Kautwange
JF-Expert Member
- Nov 15, 2011
- 1,644
- 1,648
Habari wana board!
Namshukuru Mungu kwa uzima aliotukirimia, sifa, heshima na utukufu ni kwake Yeye Pekee!
Miaka 5 iliyopita nilianza kupata hamasa ya kujifunga mambo ya kuunda tovuti, hii ilichochewa na kuwepo kwa fursa nyingi sana ambazo mimi binafsi niliziona kwenye upate wa IT (Information Technology) hivyo kwa bidi sana nikaanza kujifunza mambo ya “Coding”.
Kwa kweli ilikuwa safari ngumu sana na ndefu, yaani ukiacha kujifunza siku moja tu, unajikuta umesahau kila kitu, Mungu mkubwa, nilitia nia na bidi haswa!
Project yangu ya kwanza kabisa ilikuwa ni kuunda tovuti ambayo itawawezesha wenye guest house, lodges na huduma zote za malazi kuweza kutangaza huduma zao, fursa hii niliipata hapa hapa JF baada ya kuona wapo watu ambao wamekuwa wakiulizia sehem nzuri za kufikia kwenye maeneo mbalimbali waliyokuwa wakienda.
Hii project haikufanya vyema sana, ingawaje idea yake ilikuwa po asana, lakini nilikosa sponsor maana by that time nilikuwa nipo nipo tuu mtaani.
Leo nimefanikiwa kuwa na 5 Online Projects ambazo natamani sana wewe msomaji uzipitie na utie neno. Nashindwa kuweka link kwa ajili ya sharia ngumu za JF, ila kama utahitaji maelezo Zaidi ntatoa..
Hii ndio orodha ya mifumo ambao nimeweza kuiunda. Nakaribisha maoni, maswali na namna ambavyo unadhani natakiwa kufanya ili mifumo iwafikie walengwa!

- Marketplace kwa ajili ya bidhaa za wajasiriamali – Hii ni platform ambayo wajasiriamali wanapata fursa ya kutangaza bidhaa zao. Ni bidhaa halisi kabisa za wajasiriamali wa Kitanzania
- Online Printing – Hii idea aisee hata mimi mwenyewe nimeipenda. Hii ni platform ambayo wenye huduma za kuchapisha mabango, documents, banners, images wanajisajiri kulingana na location zao. Hii itaokoa mda wa kusubiria kazi yako iwe printed, maana utakachotakiwa kufanya ni ku search service providers kulingana nae neo, kisha utaona bei zao, ukiridhika utawatumia kazi, waki print tu, utapata notification, ukifaka kwenye stationery uta provide OTC ili kuweza kupata kazi yako. No More Queues, No More Time Wastage!
- Online POS and Stcok Management – Huu ni mfumo wa online wa utunzaji wa mahesabu ya biashara na kumbukumbu. Hapa mwenye duka, au mtoa huduma atakuwa na uwezo wa ku track mauzo, stocks, sales return, credit customer, na kila kitu kihusucho biashara, lakini pia atakuwa na uwezo wa ku generate reports mbalimbali, mfano profit and loss kwa period Fulani, cash flows na kadhalika. Kuongeza wafanyakazi wa duka pia!
- Expense Management and tracking – huu ni mfumo wa kufuatalia matumizi yako binafsi on daily basis
- Car Parking solution – Huu ni mfumo ambao kimsingi unatumiwa na Parking Solution. Kazi yao kubwa ni ku feed parking slots za maeneo mbalimbali ya Dar au Mkoa husika. Mwenye gari yeye kabla ya kuanza safari kuelekea eneo husika, basi ataangalia sehem aendayo kama kuna empty parking slot, ataweka booking akionesha muda atakao wasili, booking ikiwekwa yule parking attendant wa eneo husika atapata notification via email, na muda ukifika ile parking husika itaji mark kuwa occupied, ila kama muhusika atatokea ndani ya daki 10, basi parking automatically itaji mark kuwa available.
- E Learning System – Huu ni mfumo wa Online Learning ambao ni maalumu wa kutumiwa na learning institutions. Huu mfumo utamuwezesha tutor/instructor ku upload notes kwenye mfumo wa document au pdf, reference link kwa course husika. Lakini pia utamuwezesha ku post matangazo kwa course husika. Mwanafunzi atachagua course husika na masomo husika ambayo ame opt ili kuweza kupata notes na kuona matangazo mbalimbali. Pia mfumo huu unaruhusu CR’s Ku post matangazo kwa watu wa course zao husika
Hii ndio orodha ya mifumo ambao nimeweza kuiunda. Nakaribisha maoni, maswali na namna ambavyo unadhani natakiwa kufanya ili mifumo iwafikie walengwa!